Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,221
- 2,359
Wakati fulani Mheshimiwa Zitto kabwe alijaribu sana kutoa ufafanuzi kuwa Kamati zote za Bunge zina umuhimu na nguvu iliyo sawa. alifanya hivi baada ya fununu kuwa yeye mara hii babada ya uchaguzi wa 2015 kuna uwezekano wa njama za kuondolewa kwenye kamati ya PAC ambayo yeye na Marehemu Filikunjombe waliitumikia kwa umahili mkubwa.
Kamati ya Bunge ya mahesabu Serikali na Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama zote mbili ni kamati za bunge "zenye nguvu na umuhimu ulio sawa" lakini kwa maelezo ya gazeti lililokaririwa hapo juu na kuungwa mkono na wachangiaji wengi katika jukwaa hili ni kuwa Mkataba kuhamishiwa katika kamati nyingine ndani ya Bunge hilohilo la JMT ni njama za kuuficha!!!!
Mkataba huu ambao chanzo chake kujulikana ni Ripoti ya CAG sasa tunaambiwa kuna njama za kupotea pamoja na kupitia vyombo vyote hivi vitatu, maana yake wakati utakapofika wa kuijadili ripoti hii ya CAG Bungeni ishu ya mkataba huu itakuwa imefichwa na hata kwenye makablasha ya CAG itakuwa imenyofolewa hivyo hautajadiliwa!!!
Najaribu kutafakari vyombo vya habari na mitandao ya kijamii inatupeleka wapi, sababu mkataba huu wa Ligumi Enterprises unajadiliwa na kamati za Bunge kutaka kujua nini kilitokea hata hayo ya kafanyika, hata kabla ya kupata majibu ya kamati hizi (ambayo ni lazima itolewe wakati wa kujadiliwa ripoti ya CAG Bungeni) zimeanza kutolewa hukumu!!!
Mpaka sasa kamati zote mbili zinaonyesha kutaka maelezo toka kwa chombo cha Polisi na wala si "Wakurugenzi" wa kampuni na wala hawajaitwa mbele ya tume wala kupewa masharti yoyote wakiendelea kutafuta ukweli huu lakini leo mmoja wa wakurugenzi anaendelea na shughuli zake za maisha tunaambiwa 'Katotoka". Na hata kama kweli ameondoka kuogopa mjadala huu kwa sheria ya Makampuni ni lazima kampuni iwe na zaidi ya mkurugenzi mmoja, maana yake mmoja akisafiri kuna wengine wanaoweza kutoa majibu. Sheria inayosema hata kama kuna ulazima wa kufilisiwa itafanyika hivyo kwa mali za Kampuni na wala si mali binafsi za wakurugenzi, ni nini waandishi wanataka kutuaminisha?
Binafsi naona jambo hili linashadadiwa kisiasa zaidi na mihemuko isiyo na subira.