Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Unatia hurumaEdo njia hiyooooo....tutaelewana tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unatia hurumaEdo njia hiyooooo....tutaelewana tu.
Mkuu huyo katoka ukoo wa mchwa.Hivi ni kwanini huyo mtoto wa rais mstaafu anahusishwa na mambo mengi ya kashfa kuliko kusifiwa kwa kutenda mambo mema?hivi marehemu jk nyerere mbona alikuwa na watoto lkn hadi leo hii hatujasikia mambo ya maovu kama ya huyu?
Anahitaji mtu wa kumfanyia ushauri nasaha vinginevyo atahama nchiMkuu huyo katoka ukoo wa mchwa.
Huyu Balozi Adadi Rajabu alikuwa DCI wa Jeshi la Polisi,hizi mashine za Finger Print zina uhusiano mkubwa sana na ofisi ya DCI sababu ya aina ya makosa ya jinai ambayo vielelezo vyake hutokana na mashine hizo.Haiwezi kuwa ajabu kuwa ununuaji wa mashine hii uliishirikisha pia ofisi ya huyo bwana,hivyo ni mgao wa 10% basi ulipita kote
Mimi nigeshauri kamati ya PAC igome kuendelea na ukaguzi kwani hakuna sababu ya wao kuingiliwa.
Huu mkataba una mengi sana huu,huu ni mtihani kwa JPM na harakati zake.Hakuna ubishi kuwa kwa kupelekwa kwenye kamati ya Adadi "kashfa" hii inaenda kufa kifo cha mende[/QUOT
Nitashangaa sana kama JPM atakubali hizi zifanyike naye akae kimya na wananchi walio mwamini kauli zake waanze kumtilia shaka bila yeye kujali.Kitendo cha mkataba kupelekwa kwa mwingine na sio aliyeomba yaani kamati ya PAC hapo mjue tumeishapigwa changa la macho , mwenye akili na afahamu.
Sikuteia mghoshi!Nenda maktaba ya usajili wa ndoa ili kidhungudhungu kikutoke
Inaonekana Mwalimu wako shuleni alikuwa anapata taabu sana hata 1+1 hujui jibu lakeHoja yako ipo wapi sasa? Kwani ni makosa kwa DCI kuwa mbunge?
mkuu upo sahihi, sina uhakika record ya JPM inaweza kuvulugwa na jambo dogo hivi, kwanza itakuwa dharau,Nitashangaa sana kama JPM atakubali hizi zifanyike naye akae kimya na wananchi walio mwamini kauli zake waanze kumtilia shaka bila yeye kujali.
Hata miezi sits bado tayari anaingia kwenye kundi la kusema uongo? Hapana, kama kuna watu wanapitia hapa na wako karibu naye na wanampenda wamwambie kuwa unachafua dhamira yako na hata hayo maombi unayoomba wakuombee hawatafanya maana hustahili
Ohooo! hili tena jipya na kesi ime kwisha, sasa imesha kuwa ni salad.Namna iliyopo balozi na igp mstaafu ni mtu na shemejie
Endelea kuweka kumbukumbu zako vizuri...Tuwe na subira. Hapana chezea serikali ya Magufuli
Roho imeniuma sana! Halafu watanzania wanategemewa kuwa wazalendo. Sio kwa staili hii. Magufuli ingilia kati kama ulivyofanya Shinyanga. Tunataka kujua ukweli. Ukiwafilisi hawa tutajenga madarasa mengi.Kitendo cha mkataba kupelekwa kwa mwingine na sio aliyeomba yaani kamati ya PAC hapo mjue tumeishapigwa changa la macho , mwenye akili na afahamu.
Riz,Freddy,Sioi ni vijana waliotumia nafasi za wazazi wao kupiga.Hivi ni kwanini huyo mtoto wa rais mstaafu anahusishwa na mambo mengi ya kashfa kuliko kusifiwa kwa kutenda mambo mema?hivi marehemu jk nyerere mbona alikuwa na watoto lkn hadi leo hii hatujasikia mambo ya maovu kama ya huyu?
Mambo yote yanayohusu ulinzi na usalama hii ndio kamati yake,pia ina wabunge wa upinzani sio tabu.Tusubiri.Hii ndio Tanzania.
Hii habari imeandikwa na gazeti la mtanzania la leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Balozi Adadi Rajabu amethibitisha mkataba huo kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises kuwasilishwa mbele ya Kamati yake siku ya jana.
===============
Njama nzito kuficha mkataba wa Lugumi
MKATABA tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara Said Lugumi, umezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kushindwa kuendelea na sakata hilo kutokana na kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Hatua hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia ya ‘kulindwa’.
Wiki iliyopita PAC ilipokutana na jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ilibainika kuwa mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.
Lakini hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee na kampuni hiyo kulipwa Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za makubaliano ya mkataba.
Kutokana na hali hiyo, PAC ambayo ilibaini kuwapo viashiria vya ufisadi katika tenda hiyo, iliwaagiza watendaji wa jeshi hilo kuwasilisha taarifa za mkataba huo pamoja na vielelezo vyake ili wajumbe waweze kuupitia pamoja na kutoa maagizo.
Chanzo cha kuaminika kiliambia MTANZANIA kuwa katika sehemu ya mkataba huo kati ya Jeshi la Polisi na Lugumi, imebainika kampuni hiyo kufanya mafunzo kwa watu watano ambayo wametumia Sh bilioni 5, huku mshauri mwekelezi akilipwa Sh bilioni 46 nje ya fedha zilizopo kwenye mkataba.
Hatua ya mkataba huo kupelekwa mbele ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, inadaiwa kuwa njia ya kutaka kuwalinda baadhi ya vigogo ambao wanatajwa kuhusika na kashfa hiyo ambayo imelitia doa Jeshi la Polisi nchini.
“Hapa kuna kulindana tu, hakuna namna yoyote. Kama uchafu umebainika mbele ya Kamati ya PAC inakuwaje wengine wanadaka kitu ambacho hakikuanza kwao?
“Kuna kila dalili ya wingu na shaka, ila ukweli utajulikana tu, haiwezekani watu wanatumia fedha za walipakodi vibaya halafu inapokuja wanataka kushughulikiwa wanatafuta kivuli cha kujifichia,” kilisema chanzo chetu.
Mkataba huo uliibuliwa na PAC wiki iliyopita ambapo watendaji wa Jeshi la Polisi walishindwa kutoa maelezo ya kutosha ndipo ikawataka kuwasilisha taarifa juzi.
Pamoja na kutakiwa kufanya hivyo, hadi kufikia jana saa 10 jioni Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote kuhusu Kampuni ya Lugumi hivyo wameliandika barua Jeshi la Polisi liwasilishe mkataba huo ndani ya siku tatu.
Alisema barua hiyo wamemuomba Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, ili aweze kuwaandikia Polisi ili wawasilishe mkataba huo kwa mujibu wa utaratibu kama kamati ilivyoagiza.
“Hadi muda huu ninapozungumza nawe sijapata taarifa yoyote, kwa hali hiyo tumelazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge ili awaandikie barua polisi walete mkabata huo ndani ya siku tatu kutoka leo (jana) kama walivyotakiwa na kamati yetu,” alisema Hilaly.
BALOZI ADADI
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, alithibitisha mkataba huo kuwasilishwa mbele ya kamati yake.
“Mimi kama mwenyekiti wa kamati ninapenda kukiri kwamba tumepokea mkataba kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi na tutaufanyia kazi kwa kina.
“Tunahitaji kuona kama kuna wizara zilizohusika na mkataba huu na kama tutaukuta ni mbaya, tutatoa taarifa kwa umma. Kikubwa tunawaomba Watanzania wawe watulivu, hatuko kwa ajili ya kumlinda mtu wala kikundi cha watu, tunasimamia masilahi ya Watanzania wote,” alisema Balozi Adadi.
RIDHIWANI AKANA
Taarifa za mkataba huo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwahusisha baadhi ya vigogo wa Serikali akiwamo Waziri wa Serikali ya Rais Magufuli pamoja na kumtaja Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM).
Hata hivyo, Ridhiwani alivunja ukimya na kukanusha taarifa hizo zilizodai yeye ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Lugumi pamoja na Said Lugumi na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.
Akizungumza na gazeti moja la kila siku (Si MTANZANIA), Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, alisema hahusiki na Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo.
“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe, na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.
Alisisitiza kuwa hana uhusiano wa kibiashara na mtu huyo na kwamba hafahamu ni kwanini amehusishwa na Kampuni ya Lugumi.
“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani.
Chanzo: Mtanzania
MuhuniUncle siyo issue, mawe 3 mwepesi mno, jaribu la magu ni yule mtoto wa mfalme wa msoga ni kisiki, magu hapawezi pale.
Ndugu yangu, JPM hana rafiki wa kudumu "mark my word"JPM hebu tia neno....majipu hayo yatumbuke.