Kwa wale ambao wamejiunga na JF majuzi, napenda kuwafahamisha kuwa mambo ya Meremeta yalizimwa kwa staili hii hii...kwamba kampuni hiyo iliyoanzishwa kifisadi, kwa kuwa ulidaiwa ni mradi uliolihusisha JWTZ, mjadala ukafungwa.
Kwa ufahamisho zaidi ni kwamba kulikuwepo na wakati hata mambo ya CCM yalikuwa marufuku kujadiliwa na Bunge kwa sababu eti Chama ndicho kilishika hatamu na hata Bunge, pamoja na kuwakilisha wananchi wote, lilikuwa chombo cha CCM!
Kwa ufahamisho zaidi ni kwamba mali zote zilizokuwa mikononi mwa wananchi pamoja na mali zote zilizokuwa mikononi mwa serikali kwa niaba ya wananchi pamoja na vyombo vyote vya dola, mmiliki mkuu kilikuwa ni Chama cha Mapinduzi!
Adui mkubwa wa taifa hili ni CCM...!