Mkataba wa SportPesa: Hans Pope wa Simba SC abwaga manyanga

Mkataba wa SportPesa: Hans Pope wa Simba SC abwaga manyanga

Njaa ya viongozi wa Simba... Wanavurugana hukooo mwisho wa siku mchawi wao Yanga....na TFF.. Ndani ya Simba wapiga dili ni wengi... Na haohao viongozi wanawalaghai wanachama kwamba Yanga inabebwa,. Wao wenyewe ndio wachawi..
 
Chanzo ni nini cha mtabe huyu kubwaga manyanga kwa ninavyojua huyu jamaa bora awe ndani kuliko nje maana ataanza kuipiga nyumba na mawe (simba) msim ujao hali itakayosababisha simba kukosa ubingwa kama inavyoelekea kukosa mwaka huu
 
Tutaona mengi raundi hii ila hawa jamaa wamesaini mkataba mapema sana sijui hata umepitiwa saa ngapi umesaini mkataba Alhamisi Ijumaa unavaa Nembo za Mdhamini kwanini wafanye haraka hivyo?

Inahitaji busara sana kuwazua hili jambo.
Na jezi zikachapwa haraka ,wkt wangesubiri ligi iishe,wajua km wamefuzu ,kisha watammbulishe mdhamini na jezi mpya,hii ingesaidia kupata muda wa kifikiri na kujadili mkataba
 
Soka la Bongo ni shida sana na ndio maana timu zetu zinashindwa kushindana vilivyo kwenye mechi za kimataifa. Ukizoea figisufigisu ni shida sana
 
Yeye na Mo hawatakiwi karibishwa tena Simba waende zao wao wanataka simba iwe na shida ili wao wafaidi baadae, ili waonekane miungu
 
Figisu kilakona, matimu yenu ya siasa. Tunaposema ni wakati muafaka wa hizi timu kuuzwa serikali inakataa.
 
WEE KATULIA HIVO MAANA KAONA YANGA ANAENDA KUWA BINGWA BILA UBISHI SASA HANA CHA KUWADANGANYA MASHABIKI WA SIMBA KAMA AMBAVYO ANAFANYA SASA BORA AKIMBIE SIKUSIKIA TANGU MWANZO AKILIKATAA HILI BAADA YA KUONA MAJI KWA SHINGO BASI AKATUMIA SABABU YA SPORT PESA SASA NATAKA KUSEMA HAKUNA SPORT PESA HAPA WALA SPORT SHILINGI TATIZO UBINGWA HANA CHA KUDANGANYIA NA PUNCH LINE ZILE ZAKE ATATOA WAPI?
 
Mchezaji gani alicheza akiwa na kadi tatu? Unavuruga bandiko lako kwa kuleta ushabiki usiotija. Timu mojawapo ilifoji nyaraka kulazimisha kadi tatu, get your arcs together brother. Tusitetee ujinga.

Kwa hilo la Hanspope, kwani kujiuzulu kwake kutafanya mkataba na Spotipesa uvunjike na mkataba wa awali wa Mo kuwa honoured?

Nakukumbusha tu sababu za simba kukataliwa rufani yake ni kutuiwasilisha kwa muda na kulipia gharama zake. Kadi 3 zilidhibitika. Asante
 
Kuna kitu sijakielewa hapa!
Klabu inapata mkataba wa +5 bilions, alafu 'mfadhili' na baadhi ya viongozi wanakuwa against bila hata ya kutuelewesha mapungufu ya huo mkataba
 
Mkuu mbona nilisikia ni tetesi..imeshakuwa rasmi?
Ni rasimi mkuu...
Hii hapa taarifa:
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe ameachia ngazi.




Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi akiona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo.




“Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa,” kilieleza chanzo.

"Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka automatically katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya usajili.

"Kilichomchukiza, kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimya kimya na Hans Poppe amesema kama Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo."
 
Kuna kitu sijakielewa hapa!
Klabu inapata mkataba wa +5 bilions, alafu 'mfadhili' na baadhi ya viongozi wanakuwa against bila hata ya kutuelewesha mapungufu ya huo mkataba
Hawakushirikishwa kwenye mchakato mzima!
 
Back
Top Bottom