Mkataba wa SportPesa: Hans Pope wa Simba SC abwaga manyanga

Timu za kitanzania zinanichosha hivi hivi!!
Man U kule Hawanifurahishi
Leo huku nyumbani Simba ananipa msongo wa mawazo!!
Kazi kwenu sasa
 
We fikilia tu kuwa aliyekuwa Rais wa Yanga mkuu Talimba abassy ndiye mdhamini wa simba kupitia sports Pesa ...Je hapo hamuoni kuwa inakuwa ni style ya "kampa kampa tena".

Mo na Hans Pope wameona mbali, we subiri tu kina Aveva na Kaburu watakuja kuwapigia magoti wana msimbazi wakiomba toba.

Watani wangu wakumbuke kuwa " Zimwi likujualo halikuli ukakwisha".
 
"I have put blood for the club..." MO DEWJI

Alichangia damu wachezaji wenye majeraha?
 
kinge m cost nini hanz pope kusubiri kwanza ligi iishe ndiyo abwage manyanga? Je uamuzi wake kwa sasa hauta athiri wachezaji kwa kipindi hiki cha lala salama! hivi tukiita hii ni 'technical' hujuma tutakuwa tumekosea kweli?
 
Hili ndio soka la bongo, watu wanasaka 10% kuliko maslahi ya timu. Hii michezo ndio viongozi wanaiweza kuipanga na kuikamilisha kuliko mipangilio ya timu.
Ni hawahawa pesa za club ziliwekwa kwenye account ya kiongozi binafsi na sakata likazimwa kimyakimya.
Teamwork ya viongozi wa soka la bongo kama teamwork ya sisiemu, manyamera watupu.
 
Ukiangalia hizi Politics za hawa watu unajiuliza maswali mengi sana..Hivi simba kuwa na hawa watu imepata nini?? Imesogea hatua ngapi??? Ni kituko team iko Hoi haina uwanja haina programm ipo ipo for years...jengo lenyewe la miaka 19 Kweusi hata rangi hawapaki...hata uwanja wa zoezi tu hawana sasa wao wanafanya siasa za hovyo tu....kwann wasingejenga hata uwanja wa uongo tu...
 
Hawachelewi kusema Yanga ndo wamesababisha huu mgogoro....
 
bora niendelee kuwa mshabiki wa chelsea ulaya kwakweli..... viongozi wababaishaji...mpira wa bongo hauna vision...viongozi vision hawana...wanawaza kucheza na ndanda na majimaji na lipuli na kuchukua kataji ka million 70....shame on them... i real like simba but for this kwaheri kwakweli nahamia rasmi ulaya
 
Da bongo hakuna mpira. Mi figisu figisu tu. Bora niendelee kushabikia ze blues
 
Mimi ni mwanachama na shabiki wa Simba S.C. Mara tu baada ya kuelezwa rasmi mambo ya sport pesa, nilikosoa na sikukubaliana na hilo.... Nasikitika wenzangu walinisakama sana juu ya ukosoaji wangu.

Nashukuru kwa hapa lilipofikia, na natoa rai kwa viongozi wengine wenye mapenzi mema na simba wafuate njia ya Hans Pope.

HONGERA SANA ZAKARIA, WEWE NI SHUJAA NA UMETHIBITISHA SIO MNAFIKI..
 
Sioni tatizo lolote Simba kudhaminiwa na SportPesa .Timu za ulaya kama man united wana sponsors zaidi ya wanne AON,Chevrolet, Adidas.Timu ya Taifa ya Ufaransa wana sponsors mpaka wa maji.Kinachotakiwa kizingatiwe tu ni kuwa Timu isiwe na sponsors wanaofanya biashara au wenye maslahi yanayofanana kwamfano huwezi kukuta Timu inadhaminiwa na Pepsi na CocaCola at the same time.Ila inawezekana timu ikadhaminiwa na CocaCola na Castle Lager at the same time.
 
Mo hakuwa exclusive and solely sponsor wa Simba na hakukuwa na makubaliano rasmi kwamba yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu udhamini wa Simba sasa alitaka ashirikishwe kivipi wakati hao wadhamini wengine wanafanya biashara tofauti isiyofanana na zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…