Mkataba wa SportPesa: Hans Pope wa Simba SC abwaga manyanga

Mkataba wa SportPesa: Hans Pope wa Simba SC abwaga manyanga

Nina mashaka na elimu za viongozi wanaoongoza vilabu vyetu. Magufuli pitisha fagio la ukaguzi wa vyeti
 
Heri atoke Aveva kuliko Hans. Toka amekuwa Rais wa Timu hakuna chochote
 
Wakae Meza moja na MO wayamalize hao ni wadhamini, na MO alijinasibu kuwa mwekezaji kuna vitu viwili hapo! Mwekezaji anakuwa na time flame ya miaka zaidi ya 10 au 20/ ila mdhamini ankuwa na muda mfupi, nafikiri wamuoneshe mkataba walioingia na yeye aone kama hauna ukakasi basi waendelee na kuijenga simba sport club, migogoro hii haitasaidia kitu,
 
Mo hakuwa exclusive and solely sponsor wa Simba na hakukuwa na makubaliano rasmi kwamba yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu udhamini wa Simba sasa alitaka ashirikishwe kivipi wakati hao wadhamini wengine wanafanya biashara tofauti isiyofanana na zake.
MO sio sponsor ni MMILIKIKI MWENZA au mmesahau mlimpa 51% ya shares za Simba!!!!..... Na mkataba wa awali mkaingia... MO halalamiki kama mdhamini analalamika kama mmiliki MWENZA
 
MO sio sponsor ni MMILIKIKI MWENZA au mmesahau mlimpa 51% ya shares za Simba!!!!..... Na mkataba wa awali mkaingia... MO halalamiki kama mdhamini analalamika kama mmiliki MWENZA
Teeeeeeeeeeh teeeeeeeeeeh teeeeeeeeee
 
MO sio sponsor ni MMILIKIKI MWENZA au mmesahau mlimpa 51% ya shares za Simba!!!!..... Na mkataba wa awali mkaingia... MO halalamiki kama mdhamini analalamika kama mmiliki MWENZA
MO ni mchumia tumbo, hana lolote, alitaka yeye akiwa kama mmiliki wa simba ndiyo aingie mkataba na sportpesa kisha mafungu yote ayatie mfukoni! Sasa huo kama sio ukanjanja ni nini?
 
Upuuzi wa soka la bongo unaendelea, TFF wapuuzi sasa mpaka klabu yangu na nyie mnakua wapuuzi......
 
MO ni mchumia tumbo, hana lolote, alitaka yeye akiwa kama mmiliki wa simba ndiyo aingie mkataba na sportpesa kisha mafungu yote ayatie mfukoni! Sasa huo kama sio ukanjanja ni nini?
Kuwa na adabu MO avitamani 4.8B?kweli ????
 
Mkia ***** wewe ****

Naamini mashabiki wa Simba na Yanga humu na kokote pale hawaishi kutaniana kwa kila namna ya utani, kama hauwezi kupokea utani, basi hili jukwaa halikufai. Kwa maana sioni mantiki ya kunitukana ili hali tupo katika ushabiki wa mpira kati ya hizi klabu kongwe. Ikiwa ni muungwana utaomba msamaha lakini otherwise have a blessed day.
 
Kassim Dewji hawezi kamwe kujiuzulu. Yeye na Aveva lao moja. No watu wa kupiga dili. Walitumia pesa nyingi kuhakikisha wanaingia madarakani na sasa wako kwenye kurudisha mapesa yao na faida juu. Mkataba na MO haukuwa na manufaa kwao kwa sababu pesa ya MO ilikwenda moja kwa moja kwenye matumizi yaliyokusudiwa kama kulipa mishahara au kuweka kambi, hivyo uwezo wa kuipiga dili ilikuwa vigumu. Sasa hawa watu wa kamari wanaleta pesa halafu kina Aveva waipangie matumizi, ni neema kubwa kwa wapiga dili hawawezi kamwe kuiacha. Kumbukeni pesa za Okwi kuingia tu Aveva akazihamishia kwenye akaunti yake na wakadai kuwa ni kulipia manyasi bandarini. Wote tunafahamu mambo ya hayo manyasi mpaka juzi tu TRA wakataka kuyapiga mnada. Kumbe zile pesa za Okwi kazikwenda kwa manyasi na hakuna maelezo. Of course inasikitisha sana tena mno TAKUKURU walionyesha kufuatilia hilo swala kwa kina Aveva lakini sasa inaonyesha nao wamepoozwa. Sasa wanasimba ndio wanaona kweli sura ya kina Aveva!!!
 
Nasikia mo ameshachachagua na jengo la kuchukua kati ya yale mawili amechagua lile la kona duh mjanja kweli poleni sana watani
 
Wakae Meza moja na MO wayamalize hao ni wadhamini, na MO alijinasibu kuwa mwekezaji kuna vitu viwili hapo! Mwekezaji anakuwa na time flame ya miaka zaidi ya 10 au 20/ ila mdhamini ankuwa na muda mfupi, nafikiri wamuoneshe mkataba walioingia na yeye aone kama hauna ukakasi basi waendelee na kuijenga simba sport club, migogoro hii haitasaidia kitu,
Na kama una ukakasi je? Lakini kama kuna haja ya Mo kuuona huo mkataba hivi sasa, hakukuwa na haja ya kuuona kabla ya kusainiwa? Wakati upi ungekuwa mwafaka zaidi kuuona huo mkataba?
 
MICHEZO

BREAKING: “Hans Pope amefuta uamuzi wa kujiuzulu uongozi Simba

Kupitia Instagram Haji Manara ameandika >>> Rasmi Hanspope arejea kundini, afuta uamuzi wake wa kujiuzulu, na ndio maana fans wetu nawaomba mtulie, hakuna kitakachoharibika, ni upepo mbaya ulipita na sasa umetulia, Karibu tena kamanda Pope<<< –Manara
 
Back
Top Bottom