Mkataba wa sportpesa na Yanga unaruhusu haya?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Visit Tanzania ni tangazo ambalo linapaswa kufanywa na idara ya utalii na tanapa ili kuvutia wageni kuja Tanzania kuona vivutio vyetu. Matangazo kama haya huwaga na bajeti yake tena kubwa TU kwenye sekta husika.

Je, mkataba unamruhusu sportpesa kuichagulia Yanga nini Cha kuweka kwenye jezi yake zaidi ya maandishi yake ya sportpesa inapotokea tukio kama hili?

Je, udhamini wa sportpesa umezingatia gharama za timu kushiriki mashindano ya caf?

Je, sportpesa inapata hasara gani kama Yanga wakivaa jezi yenye maandishi ya Hailer kwenye michuano ya CAF tu? na Je, kuvaa visit Tanzania kutafidiaje hasara hasara hiyo (kama ipo)?

Je, mkataba una kifungu kinachoruhusu au kukataza sportpesa kubuni nini Yanga ivae kama ikitokea hali kama hii ya CAF kukataa jezi za timu zenye wadhamini wasiowataka?

Hii ni mara ya kwanza kutokea kwenye Soka letu lazima tuijadili kwa kina na usahihi ili iwe reference kwa kesi kama hizi huko mbeleni.
 
Visit Tanzania ni tangazo ambalo linapaswa kufanywa na idara ya utalii na tanapa kuvutia wageni kuja Tanzania kuona vivutio vyetu. Matangazo kama huwa haya Yana bajeti yake tena kubwa TU.
Je, mkataba unamruhusu sportpesa kuichagulia Yanga nini Cha kuweka kwenye jezi yake zaidi ya maandishi ya sportpesa?

Je, udhamini wa sportpesa umezingatia gharama za timu kushiriki mashindano ya cat?

Je, sportpesa inapata hasara gani kama Yanga wakivaa jezi yenye maandishi ya Hailer kwenye michuano ya CAF tu?

Itaisha tu hiyo.
 
Maswali yako haya yoooote yanajibiwa na jibu moja toka kwenye swali hili:

Kwanini Yanga waliomba ridhaa ya Sportspesa juu ya kuweka logo nyingine kwenye jezi katika mashindano ya kimataifa hatua ya makundi?
 
Kuna wale watu hubishana bila kusikiliza hoja za upande wa pili. Kwa hiyo anakuwa haelewi hata maelezo unayompa. Ndio mashabiki wa Yanga
 
Utopolo mmefungua nyuzi nyingi Katika hili halafu mnaihusisha Simba....Sasa hapa Simba inaingiaje..?

Huyo Tarimba Mbona ni MTU Wenu, nyie Pambaneni Na Hali Zenu ili Msionekane 'Hamnazo' Kama Manara alivyowabatiza Jina La ' Hamnazo'...!
 
Ntajibu swali namba mbili. Ndio sportpesa inamchagulia yanga cha kuweka mbele ya jezi. Ntakupa mfano kuna kipindi yanga walivaa jezi zinazoonesha menyu ya sportesa nikimaanisha zile namba za kupiga kubeti kwenye kitochi.
 
Sportpesa ndiye mwenye Hatimiliki na kifua cha Yanga ( mdhamini mkuu).
Si yanga tena, umiliki wake ulikata pale alipo chukua Bil 12.
Sawa, lakini anaruhusiwa kuichagulia Yanga nini Cha kuandika kifuani? Kwanini asiishie kusema kifua kiwe wazi ili asione chochote pale. Yaani huko ni sawa na kumchagulia mkeo mume wa kulala nae chumbani wakati ukiwa safarini. Je, mume anayo mamlaka hayo kwa mkewe?
 
Maswali yako haya yoooote yanajibiwa na jibu moja toka kwenye swali hili:

Kwanini Yanga waliomba ridhaa ya Sportspesa juu ya kuweka logo nyingine kwenye jezi katika mashindano ya kimataifa hatua ya makundi?
Kwakuwa kifua kitakuwa wazi kwasababu za CAF. Sportpesa hawana mamlaka ya kuwaamuru Yanga wavae visit Tanzania. Tanapa ndio wanaoweza kuomba Yanga wavae visit Tanzania.
 
Nimeacha kusoma baada ya kuona neno mashindano ya cat nikajua tu we nyoka wa kibisa huna akili
Wewe ni akili ndogo, unahangaika na error ndogondogo TU.
 
Ntajibu swali namba mbili. Ndio sportpesa inamchagulia yanga cha kuweka mbele ya jezi. Ntakupa mfano kuna kipindi yanga walivaa jezi zinazoonesha menyu ya sportesa nikimaanisha zile namba za kupiga kubeti kwenye kitochi.
Visit Tanzania Ina uhusiano gani na sportpesa? Hatujali kama sportpesa wangesema huweke picha ya mshindi wa sportpesa jackpot, lakini sio kitu kingine. Kesho watakwambia tuweke picha ya mo au pkipiki ya boxer, tutakubali?
 
Endeleeni kuwa wabishi, mtarudi kucheza vifua wazi.

Kwa maswali yako hayo utakuwa mgeni kwenye masuala ya mpira. Hatukudhani mmeathirika hivi kisaikolojia kwa kutokuwa kwenye makundi toka enzi Nyerere akiwa hai.

Kama hamtaki kutangaza utalii, wekeni matangazo ya kuwaambia watu wavae barakoa maana bado mko nyuma sana.
 
Sawa, lakini anaruhusiwa kuichagulia Yanga nini Cha kuandika kifuani? Kwanini asiishie kusema kifua kiwe wazi ili asione chochote pale. Yaani huko ni sawa na kumchagulia mkeo mume wa kulala nae chumbani wakati ukiwa safarini. Je, mume anayo mamlaka hayo kwa mkewe?
Umeandika nini sasa hapa? 😂😂😂😂. Nimesoma comment zote, yaani wewe ndio huelewi chochote kabisa😂😂😂
 
Back
Top Bottom