Mkataba wa sportpesa na Yanga unaruhusu haya?

Mkataba wa sportpesa na Yanga unaruhusu haya?

Visit Tanzania ni tangazo ambalo linapaswa kufanywa na idara ya utalii na tanapa kuvutia wageni kuja Tanzania kuona vivutio vyetu. Matangazo kama huwa haya Yana bajeti yake tena kubwa TU.

Je, mkataba unamruhusu sportpesa kuichagulia Yanga nini Cha kuweka kwenye jezi yake zaidi ya maandishi yake ya sportpesa?

Je, udhamini wa sportpesa umezingatia gharama za timu kushiriki mashindano ya cat?

Je, sportpesa inapata hasara gani kama Yanga wakivaa jezi yenye maandishi ya Hailer kwenye michuano ya CAF tu?

Je, mkataba una kifungu kinachoruhusu au kukataza sportpesa kubuni nini Yanga ivae kama ikitokea hali kama hii ya CAF kukataa jezi za timu zenye wadhamini wasiowataka?

Hii ni mara ya kwanza kutokea kwenye Soka letu lazima tuijadili kwa kina na usahihi ili iwe reference kwa kesi kama hizi huko mbeleni.

Nilijua unaweka huo Mkataba, kumbe ni blah blah tu[emoji2097]
 
Visit Tanzania Ina uhusiano gani na sportpesa? Hatujali kama sportpesa wangesema huweke picha ya mshindi wa sportpesa jackpot, lakini sio kitu kingine. Kesho watakwambia tuweke picha ya mo au pkipiki ya boxer, tutakubali?

Sportpesa ndio wanaamua ilo liwekwe hapo. Wao ndio wata collide na visit Tanzania kutengeneza resolution.
 
Visit Tanzania ni tangazo ambalo linapaswa kufanywa na idara ya utalii na tanapa kuvutia wageni kuja Tanzania kuona vivutio vyetu. Matangazo kama huwa haya Yana bajeti yake tena kubwa TU.

Je, mkataba unamruhusu sportpesa kuichagulia Yanga nini Cha kuweka kwenye jezi yake zaidi ya maandishi yake ya sportpesa?

Je, udhamini wa sportpesa umezingatia gharama za timu kushiriki mashindano ya cat?

Je, sportpesa inapata hasara gani kama Yanga wakivaa jezi yenye maandishi ya Hailer kwenye michuano ya CAF tu?

Je, mkataba una kifungu kinachoruhusu au kukataza sportpesa kubuni nini Yanga ivae kama ikitokea hali kama hii ya CAF kukataa jezi za timu zenye wadhamini wasiowataka?

Hii ni mara ya kwanza kutokea kwenye Soka letu lazima tuijadili kwa kina na usahihi ili iwe reference kwa kesi kama hizi huko mbeleni.
Kweli Mkuu Kavulata lazima tupate kitu kinaitwa Precedent kwenye sheria.
 
Sports pesa wanachekesha, yaani ni sawa umpangishe mtu kwenye nyumba yako halafu umchagulie mtu wa kuishi nae hata kama ni jambazi
 
Sportpesa ndiye mwenye Hatimiliki na kifua cha Yanga ( mdhamini mkuu).
Si yanga tena, umiliki wake ulikata pale alipo chukua Bil 12.
Haki yake Ina mipaka.pale anapozuiwa na waandaaji wa mashindano.hakuna kipengele kinachomzuia Yanga kumuweka mdhamini mwingine.asiye mshindani wa Sportpesa pesa.
 
Yanga bado inaitangaza sp kipindi hiki. Sp angeeleweka kama Yanga ndio iliyokataa kuvaa SP kwenye caf tonaments. Pili ingekuwa na hoja kama Hailer ingekuwa kampuni ya kubet, ingeeleweka kama sp ingebeba gharama za timu kusafiri na kuhudumia timu kwenye mashindano ya CAF. Hiyo bonus na pesa za CAF zote zinakuja mwisho wa mashindano (to late to help the team). Sp ingeeleweka pia kama ingeamuru jezi zibaki wazi kifuani badala ya kulazimisha wavae visit tz. Siku nyingine watakulazimisha uvae jezi yenye picha ya kondom ya kike kama kampeni ya kuzuia magonjwa.
Una kichwa kigumu sana.
 
Rudisheni B 12 za sportpesa..muandike mnachotaka..
Yaani watu watoe pesa kulipia tangazo kwa misimu mitatu alafu..kihuni muwape watu wengine haki hiyo katikati ya mkataba..
Vipi watu wakiacha kuvaa jezi zenye sportpesa wakaanza kuvaa jezi hizi mpya kwenye mechi za ligi kuu (wanayanga wanasema Ni nzuri kuliko za ligi kuu)
Uoni yanga mnafifisha malengo ya sportpesa kuonekana..
Yanga wanaandika wanachotaka kwenye kifua Cha jezi zao kwa mechi 3 TU za mechi za makundi baaaaasi!! Usiwe zuzu. Caf ndio iliyoiondoa sp kwenye vifua vya Yanga, wapeleke kesi caf. Lakini sp hawana ubavu wa kuiamuru Yanga iandike visit Tanzania kwenye Jez zao. Au sp iimevuta pesa kutoka tanapa? Wacha Royal tour na jitihada nyingine za bodi ya utalii vilete wageni Tanzania.
 
Mkuu kavulata mimi nakuheshimu sana mtani wangu, ila katika andiko lako unaonesha wasiwasi wako juu ya vipengele vya mkataba wenu na Sportpesa.

Hasa kwenye kipengele cha nini kitafanyika kwenye eneo lao la kuweka tangazo endapo kanuni za mashindano hazitaruhusu wao kukaa hapo.

Unataka kusema mlisaini mkataba bila kuweka kipengele hiki sawa sawia ?

Je, katika mazingira hayo, sisi "watesi wenu" tukiutumia mwanya huu kusema kwamba mlisaini mkataba bila kuuelewa (wote) tutakua tunawaonea ?
Yanga waliuelewa mkataba lakini Ni loop hole kwa Yanga kukosekana kipengele hi cho kweñye mkataba. Ndio maana Yanga wananufaika kwa mapungufu hayo
 
Niwie radhi ndugu mtoa mada kama utakwazika lakini kwa namna ulivyoandika hoja zako....na namna unavyojibu ni dhahiri kuwa huna ufahamu na masuala ya mikataba kama hii........

Pengine unasukumwa na hisia za upenzi Kwa klabu yako pendwa........

Kwa mujibu wa mkataba wa Yanga na sportpesa ni kuwa wao ndio wenye haki ya kukaa kifuani mwa jezi za Yanga mpaka pale mkataba wao utakapomalizika........

Ikitokezea kuwa kuwa kuna namna ambayo sportpesa hawawezi kukaa kwenye kifua Cha Yanga kama mdhamini kutokana na kanuni za mashindano husika basi Yanga watalazimika kuomba ridhaa ya sportpesa ili kuweka mbadala wake na sio vinginevyo........

Ndio maana inavyosemekana klabu ilikwenda kuomba ridhaa ya sportpesa juu ya hilo..........

Lakini kwa namna mambo yanavyokwenda ni kwamba Yanga hawakufikia muafaka na Yanga wameamua vinginevyo...........

Mpaka sasa inawezekana sportpesa wamepata hasara kwa kuwa jezi zimeshauzwa na zinavaliwa kinyume na madhumuni ya mdhamini mkuu..........lakini nadhani watatafuta namna ya kuyaongea na kuyamaliza........
Kama hiyo jez ingeandikwa visit Tanzania sp wangeizuiaje hasra iliyoletwa na Hailer kwenye jez?
 
Safi, hii inaitwa kukabia juu.
Halafu wabongo tunakesha kuangalia mipira ya Ulaya but hatujifunzi. Lile eneo Sp wamelinunua kama Sportfy walivyonunua la Barca, ndiyo maana Barca washawahi kuvaa neno Shakira na OVO (label ya Drake) siku mbili tofauti kwa maelekezo ya Spotify sababu wao ndy owner wa kifua cha Barca. Sasa uto wamekubali kuolewa then wanataka kulala na chupi.
Mkataba wa Barca na sportfy una kipengele hicho, lakini huu wa sp hauna kifungu hicho. Mambo hayawezi kuwa automatic au kwa assumptions.
 
Wale mikia fc wamefeli kuvuruga Yanga kupitia Mzanzibari sasa wameibukia kwenye matukio naamini hili nalo litapita, Yanga itabaki imara nyuma mwiko
 
wangese nyie iyo visit tz ya kazi gani timu yenyewe ni kiwakilish tosha kama mnataka visit kawekeni man city huko ulaya mbwa nyie
 
Caf kuanzia makundi wana mdhamini wao ambae ni kampuni ya betting ambayo ni 1×bet sasa ukivaa sportpesa unachanganya madawa maana yule ni mshindani wa 1x bet, sp inatoa bonas kama yanga wakifanya vzr kwenye mashindano haya sasa mtu anaekupa bonas, mshahara, usafiri chakula nk nk leo unaendaje kuvaa mdhamini mwingine.
Ndio, sp wanawapangia yanga nani awe mbadala wao kwenye hatua hii ya makundi kwa kuwa fedha zitaendelea kutolewa na sp kwani visit tz hawatoi hata buku, sp wana umiliki wa kifua cha yanga hadi 25,
Shida walikataa kuvaa visit tz kwamba wataonekana wameiga simba,
Kumbuka jezi za haier ziko mtaani na zimeuzwa na pembeni kuna nembo ya yanga basi tayari soko la sp lishaaribika...
Feisal anaambiwa aheshimu mkataba wakati club yenyewe haieshimu mikataba ya wenzao
Bonus haizingatii gharama za kushiriki mashindano. Timu inahitaji kukaa siku 6 kule Tunis kabla ya mechi kama mbinu ya vita, sp inachangia sh. ngapi kwenye gharama ya namna hii? Wapenzi na mashabiki wanaweza kuichukia sp milele kama itaonekana kama vile inataka kuihujumu Yanga kwa kushirikiana na Simba kuwatoa mchezoni.
 
Upo sahihi pale hata akisema waandike "Tarimba" ni sawa tu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Tumieni akili kuwaza. Walioikkataa sp ni CAF sio Yanga. Na bahati mbaya hawataki mtu, biashara au kitu chochote chenye uhusiano na betting (kamali) kwenye Jez ya Yanga wakati wa mashindano yake. Bahati mbaya sana mkataba wa sp hauna nguvu kisheria ya kuiamuru Yanga ivae nini mbadala wa sp na bidhaa zake zote. Sportpesa inawezakuishia kusema msiweke chochote kifuani lakini sio kuiamrisha Yanga ivae visit Tanzania, mo, babra, tarimba, Bashite au kitu chochote kisheria. Hivyohivyo, sp Haina jukumu la kimkataba la kuisaidia Yanga kumudu gharama za kushiriki mashindano ya CAF, inatoa bonus (bahashish) TU kwa kufika makundi au robo, nusu au final.

Sportpesa iwaonbe radhi Yanga kwa kuwapotezea focus Yao kuelekea mashindano yaliyoko mbele yake kuhangaika kujibu hoja yake dhaifu,
 
Visit Tanzania ni tangazo ambalo linapaswa kufanywa na idara ya utalii na tanapa kuvutia wageni kuja Tanzania kuona vivutio vyetu. Matangazo kama huwa haya Yana bajeti yake tena kubwa TU.

Je, mkataba unamruhusu sportpesa kuichagulia Yanga nini Cha kuweka kwenye jezi yake zaidi ya maandishi yake ya sportpesa?

Je, udhamini wa sportpesa umezingatia gharama za timu kushiriki mashindano ya cat?

Je, sportpesa inapata hasara gani kama Yanga wakivaa jezi yenye maandishi ya Hailer kwenye michuano ya CAF tu?

Je, mkataba una kifungu kinachoruhusu au kukataza sportpesa kubuni nini Yanga ivae kama ikitokea hali kama hii ya CAF kukataa jezi za timu zenye wadhamini wasiowataka?

Hii ni mara ya kwanza kutokea kwenye Soka letu lazima tuijadili kwa kina na usahihi ili iwe reference kwa kesi kama hizi huko mbeleni.
5653717F-E06D-4319-912E-6FBC07299B99.jpeg
0F80626D-171A-4AB8-8F55-DD1A0FFE1FE0.jpeg
 
Back
Top Bottom