Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Habari za leo? Sisi ni wakazi wa Sanawari, Arusha mtaa wa Moivo. Tunaomba utusaidie kupaza sauti ili ndugu zake wapatikane. Huyu ni jirani yetu, ameuawa kwa kuchomwa kisu na mkewe juzi usiku baada ya kutoka kazini. Anaitwa Dominic Pius alikuwa dereva wa magari madogo ya mizigo, Soko Kuu Arusha.
Baada ya mkewe kufanya tukio hilo la kinyama alitoroka na kumwacha na watoto wadogo. Watoto walishuhudia tukio hilo la kinyama kabla ya mama yao kutoroka. Mwanae mdogo alipomuona baba yake ameanguka alikimbilia kumuamsha kumbe ameshafariki.
Sasa tangu tukio hilo litokee ndugu zake hawajapatikana. Tunaomba utusaidie kupost huenda ndugu zake wakapatikana ili waweze kuchukua mwili kwenda kuzika, na hawa watoto waweze kulelewa. Inasemekana alikuwa mwenyeji wa Mazimbu, Morogoro.
Endapo kuna ndugu, jamaa, marafiki au mtu yeyote anayemtambua marehemu, tafadhali awasiliane na rafiki wa familia kwa namba 0753-168752 au Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Moivo kwa namba 0769-714118. Tunatanguliza shukrani