Mke amuunguza mumewe sehemu za siri na maji ya moto kisa wivu wa kimapenzi

Nyamesocho

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2023
Posts
487
Reaction score
1,287
Mwalimu anayefundisha shule ya sekondari Kebogwe iliyopo Wilaya ya Tarime, ameunguzwa na mke wake na maji ya moto sehemu mbalimbali za mwili hasa sehemu za siri kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi

Shuhuda wa tukio wanadai siku ya Jumatano jioni mwalimu alimkuta mke wake duka fulani na kuanza kumpiga mke wake mpaka nyumbani kwake.

Baada ya ugomvi kuisha mwalimu aliingia kitandani kulala huku amevua nguo na huku mke wake akibaki jikoni akichemsha maji

Baada ya maji kuchemka ipasavyo, mke wake aliweka kwenye ndoo na kwenda chumbani na kummwagia mume wake aliyeungua vibaya sana na kutoroka kusikojulikana

NB: Wanandoa epukana na ukatili
 
Watu wa Mara wanaonaga kupiga ni sifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…