HSE Officer
JF-Expert Member
- Apr 10, 2023
- 665
- 892
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leo naomba mumsaidie rafiki yangu kumshauri, mimi ni nimeshashauri kwa upande wangu lakini nataka kuona fikra za watu zaidi.
Jamaa ana mke na watoto, hivi karibuni kaka yake alipoteza kazi ndugu wakamuomba asaidie kulea mtoto mmoja ambaye alikuwa kidato cha pili. Jamaa alimshirikisha mke wake kuhusu mgeni huyo mke akakubali lakini inaonekana alikubali kwa shingo upande.
Kwa sasa sio siri tena mwanamke kasema wazi kabisa hataki kuishi na huyo mtoto tena akaenda mbali zaidi kampigia simu mama wa mtoto kumueleza yeye hawezi kuishi na mtoto wake. Habari zikamfikia jamaa akashangaa sana aliporudi kumlaumu mwanamke kwanini amefanya hivyo mwanamke kaja juu na kusema hata yeye ana maamuzi kwenye familia na msimamo wake ndio huo, hataki kuishi na huyo mtoto.
Jamaa kabembeleza sana mke akawa kama kaelewa kumbe bado. Hivi juzi kalianzisha tena na sasa amefika mbali kamwambia mume wake achague moja aidha kuishi na yeye(mke) ama mtoto wa ndugu yake........
Mzozo uko hapo, mimi nilimshauri kama hana uwezo wa kumlea huyo mtoto amrudishe kwao lakini si kwasababu ya kukataliwa na mke wake maana hata yeye hajui kesho yake. Jamaa alinijibu uwezo anao maana mtoto anasoma shule za serikali halipi ada hata mia zaidi ya uniform na vifaa vya shule.
Kama nimekosea naombeni sababu, bado tuna nafasi ya kumsaidia jamaa. Kwa ndugu upande wa mume na narafiki zake wanashangaa sana maamuzi ya mwanamke lakini kwa ndugu wa mke anasema zaidi ya
apeleke msaada kila mwezi lakini mtoto akae kwao na wazee wake. Siku hizi mambo ya kubeba ndugu yaishe, kila mtu abebe mzigo wake.Je, kitu hiki kimeshatokea walipokuja ndugu wengine?
Kama jibu ni hapana
1. Akae na mke wake sehemu tulivu ikibidi nje ya nyumbani apige nae story, kujua changamoto ni nini kuishi na huyo mtoto
Huyo mtoto anaingia foolish age, umri ambao majority wanakuwa watukutu sana, viburi, dharau. Na kwa vile si mtoto wake na wazazi wake wapo hawezi kupata uhuru wa kumuadhibu anapokosea
Kama itaonekana mtoto ndo changamoto
Arudishwe kwao then baba yake mdogo sijui mkubwa awe anatuma hela za kusapoti
Kwenye ndoa kunahitajika hekima sana
There is no one answer fit all
Lakini kama ni tabia ya mkewe, inahitajika uvumilivu na maamuzi ya busara
Vinginevyo ajipange kwa ugomvi, mabishano, kununiwa, kukosa amani, kukosa hamu ya kurudi nyumbani