Mke kuleta ndugu likizo kupumzika na kukaa miezi bila dalili ya kuondoka

Mke kuleta ndugu likizo kupumzika na kukaa miezi bila dalili ya kuondoka

Miaka 15 si mtoto huyo jamani, yaani unaona shida kuishi na binti wa miaka 15😳
Wewe kiboko aiseeeeee!
Sio shida unaishi vip na bint wa Umri huo wakat baba na mama wapo hai wanaishi na kutafuta rizki yaan wao wastarehe niwalele alafu mtoto akibadilika kitabia niangushiwe zigo mim kwamba nilimg'ang'ania kukaa nae
 
For as long as ana baba na mama akakae kwa wazazi wake... miezi mitatu ni mingi sana

Wewe rudi na tiketi, wakati wa chakula cha jioni acha maagizo keshokutwa yake aende. Asiyeridhika aende nae

Wanaume wa siku hizi mpo soft sana, diplomasia ikigoma tumia authority yako as a man
 
Angekuwa mwanamke ndio kaanzisha huu uzi, ungesikia wanawake wana roho mbaya hawapendi ndugu wa mume, wanapenda ndugu zao tu ndio wawatembelee
Mipaka na iheshimiwe regardless ya jinsia... huwezi sukuma mwanao akakae kwa watu 3 months, wazazi wa binti ni washenzi
 
Wakuu hii imekaaje mke kuleta ndugu bila taarifa kuja kukaa likizo nakusalimia nakukaa miezi bila kuondoka..mke akiulizwa anasema anaogopa kumwambia atamwambiaje ataona amfukuza
Kwani kabla ya ndoa walikubaliana vipi?
 
Na wewe hujui kama familia nyingi anayefanya kazi za nyumbani ni mama, au unadhani hachoki kuwafanyia watu hizo kazi kila siku, upeo wako mkubwa uko wapi hapo

Familia nyingi ni extended na sio Mama pekee anayefanya shughuli za nyumbani. Wapo watoto, ndugu n.k.

Bado UPEO wako upo chini.
 
Dah,kuna jirani yangu hapa nadhani mwanaume ameamua ajiweke pembeni.
Kila kukicha ni wageni yaani nyumba haipoi kila siku mguu utadhani hawana makwao.
Ukioa mwanamke mswahili na wewe sio mswahili jua hamtawezana.
 
Familia nyingi ni extended na sio Mama pekee anayefanya shughuli za nyumbani. Wapo watoto, ndugu n.k.

Bado UPEO wako upo chini.
Kwenye familia nyingi ndugu wa mume huwa hawasaidii hizo kazi za nyumbani, mara nyingi kazi yao huwa ni kula kulala kuangalia tv na kupiga story, nimekuambia nioneshe huo upeo wako mkubwa uko wapi
 
Ndugu alikuja kukaa nae likizo ya shule Ile yakumaliza shule ya miezi3 ...tumekaa nae miezi3 Sasa anatokea nyumbani kwangu nawazazi wake wote wapo hai Sasa mke unamuhoji ananuna anakwambia mbona mfanyakazi wandani ye anakaa kwanin ndugu yake wa damu asikae nabakia kumshamgaa tu
Wanawake akili zao wanazijua wenyewe huyo mkeo atasabasha wewe uonekane una roho mbaya iwapo huyo nduguye akigundua keleko lako juu ya uwepo wake hapo kwako cha kufanya wewe kausha tu ila anza kubana matumizi kama ulikuwa mnakula milo 3 kwa siku fanya miwili ila usimuoneshe dalili zozote huyo nduguye
 
Kwenye familia nyingi ndugu wa mume huwa hawasaidii hizo kazi za nyumbani, mara nyingi kazi yao huwa ni kula kulala kuangalia tv na kupiga story, nimekuambia nioneshe huo upeo wako mkubwa uko wapi

Familia nyingi zipi?
Wakati Mtoa Mada ni Moja ya mashuhuda kuwa ndugu za mkewe ndio wapo nyumbani.

Kingine siku hizi nyumba nyingi zina housegirl hao Wamama wanaofanya Kazi za nyumbani Hadi ziwachoshe wako wapi?

Tatizo UPEO mdogo.
 
Ni nyumba gani hizo ambazo mke ni mama wa nyumbani halafu bado kazi zote za nyumbani anafanya housegirl pekee, maana kwa mujibu wako ni kwamba familia nyingi anayehudumia ni baba hivyo umeassume kuwa kina mama hawafanyi kazi wala biashara hivyo hawaingizi kipato, sasa kama unasema hakuna kina mama wanaofanya kazi za nyumbani kiasi cha kuchoka hebu tuambie basi hao kina mama huwa wanafanya nini..bado sijaona huo upeo wako mkubwa uko wapi!!
 
Familia ya Mtoa Mada ni kielelezo na jibu la swali Lako.

Hilo swali Majibu mnayo ninyi Wanawake.
Kwani ninyi mnavyotaka mna- housegirl na hapohapo mnataka kuhudumiwa kwa kila kitu huwa mnafanyaga nini nyumbani?
 
Hoja ni kwamba kwanini akilalamika mwanaume inaonekana ni sawa ila akilalamika mwanamke inaonekana ana roho mbaya, kwahiyo unataka kusema mke akitaka housegirl na hapo hapo bado anataka kuhudumiwa basi mume anakubali na kutekeleza yote hayo kirahisi tu, ni wanaume wa wapi hao na kama wapo wanaofanya hivyo sasa hapo nani mjinga na wa kulaumiwa kati ya mke au mume
 
Kuna mshua mmoja namjua, huyo ukienda kwake lazima akuulize utakaa siku ngapi.

Yeye akirudi usiku kutoka mishe zake, mkiwa mmekaa labda unampa taarifa za kijijini zinaendaje, lazima utakutana na swali. Unakaa siku ngapi?
Hatarii na nusu.
 
Back
Top Bottom