Mke na mume tumeleta mashtaka kwenu

Mke na mume tumeleta mashtaka kwenu

Wewe hapo ndio una Makosa kwa mtazamo wangu. Makosa kivipi?

1. Kuoa (Sijui umri wako ila under 40 mapema sana)
2. Kuoa tayari mtu anamtoto hafu BABA YAKE yupo hai na mzima (inabidi awe alifariki au yupo Milembe)
3. Kumchunguza mke wako.
4. Kutumia condom kwa mkeo iyo dharau aisee. Sijaona lakini mh iyo dharau kubwa.
5..
😂Akitoka Milembe ndio utamjua vizuriq
 
Una fikra kwamba baba wa hyo mtoto anamtafuna mke wako ingawa inaonesha ushahidi huna...jiamini acha kuwa wasiwasi mpaka pale utakuwa umejihakikishia pasipo na shaka kuwa mkeo anakusaliti

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mkuu ,kama hataki kutafunwa kwanini hakufuata maelekezo yangu na kwanini alimtafuta kinyemela? Nilimwambia amtafute wifi yake ambaye ni dada wa mzazi mwenzake yeye hakufanya hivyo,kwanini?
 
Kwangu mimi inaweza ikawa suluhisho la kudumu sijui upande wa mwenzangu,nikiachana naye sioi tena mwanamke mwenye mtoto ni wasumbufu sana.
Iki unachokiongea mkeo pia anasoma ,hivi unahisi anajisikiaje ndo upendo umeisha kiasi icho??

Aisee single mamaz ifike pahala tujue kuwa ndoa kwetu si kipaumbele tena na ukibahatika basi ijue na kuitambua mipaka yako na baba mtoto wako ili usimkwaze uyo alie kusitiri na kuhatarisha ndoa

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Wewe ndiye unamatatizo makubwa au ukosefu wa Akili Kabisa.

Mwanamke mwenye mtoto sio Mkeo pekee yako.
Ukioa mke mwenye mtoto elewa kuwa mzazi mwenzake pia ni Mumewe, mzazi mwenzake, Baba WA m/watoto wake.
Hivyo ni halali yake kuwasiliana Naye Kama sio kumpa haki zake za kindoa.

Usioe single mother Kama wewe sio single father.
Mtalaka hatongozwi.

Mengine yote ni kujifariji kama binadamu
Kuna majibu yana ukweli hadi umashindwa ufanye maamuzi gani.
 
Wewe hapo ndio una Makosa kwa mtazamo wangu. Makosa kivipi?

1. Kuoa (Sijui umri wako ila under 40 mapema sana)
2. Kuoa tayari mtu anamtoto hafu BABA YAKE yupo hai na mzima (inabidi awe alifariki au yupo Milembe)
3. Kumchunguza mke wako.
4. Kutumia condom kwa mkeo iyo dharau aisee. Sijaona lakini mh iyo dharau kubwa.
5..
huyu jamaa apelekwe mirembe nimeshangaa yuko huku JF wakati akina ROBERT HERIEL , JokaKuu wakitumia nguvu kubwa kuwaonya na kuwaasa vijana kama wanataka kuharibu maisha yao waoe masingle mother alikuwa wapi huyu?
 
Kwakuwa naye anasoma hizi comments naamini atalifanyia kazi,aniache aendelee na maisha yake,mzazi mwenzake anapotaka kutoa huduma kwa mwanaye sio lazima awasiliane na yeye,kaka yake ambaye anaishi na mtoto yupo kwanini asiwe anawasiliana na huyo? Mke ni ni mume mmoja tu kuwasiliana na wanaume wawili hiyo ni ndoa ya wanaume wawili mimi sipo tayari.
uko sahihi hata maandiko yanasema mke ni kwa mume Mmoja tu. sasa wewe huoni ulioa mke wa mtu? kiukweli mkuu ni Mateso sana hawa viumbe hasa ukikikuta na kiumbe ambacho kilishazaliwa huko kabla yako balaa huwa kubwa zaidi. nadhani ulikuwa na nguvu ya pesa kwa wakati huo. kama ulivyosema. ukasahau maisha huwa yanabadilika leo mambo yameenda sivyo ndivyo unasema mwanae atafutwe baba yake atume matumizi ya mwanae!

sasa unadhani hapo hawatarudiana kwenye kufanya ile zinaa kwa kuwa hao ni kitu kimoja tayari? kuoa mwanamke mwenye mtoto ni Kitanzi kwa kweli.
 
Kwangu mimi inaweza ikawa suluhisho la kudumu sijui upande wa mwenzangu,nikiachana naye sioi tena mwanamke mwenye mtoto ni wasumbufu sana.
pole jamaa umejifunza kitu. kiukweli mimi nilikuwa na mpenzi single mother ila kila nikitaka kumuoa nikawa sina amani kumbe anawasilianaga na mtu wake haipiti wiki mbili kama hawajawasiliana. kumbe kwangu ni shida tu zilimletaga. yaani nilikasirika lakini nikajiona mimi ndio mkosefu. siku moja akawa anamwongelea shit huyu mzazi mwenzake.
iko siku nyingne akawa anamwongelea kwa huruma kwa kusema fln sahivi mambo yake ni mabaya nilichoka. kumbe kuna saa anajifeel huruma kwake licha ya kuachana.
Single Mother hafai kuolewa.
 
Kama kweli huyo mkeo yupo humu basi anisome hapa....

Kifupi hujawahi kumpenda, ulimtamani tu ukamuoa na bahati mbaya umeshamchoka. Na upo kumtafutia sababu.

Kama zinamtosha kichwani ajiongeze, atulize akili ajue namna ya kulea wanae na asiweke kipaumbele mambo ya ndoa.

Ni wanaume wachache sana wanahimili mwanamke mwenye mtoto, wengi hawawezi kiasi kwamba hata mwanamke akikosea kitu ambacho mwanamke asiye na mtoto/watoto angekosea linakuja jibu la ndio tatizo la single mothers.

Sasa wewe mwenye huyu mume, na wengineo, akili zenu ziwe kwenye kulea watoto wenu sio kuwaza ndoa mwisho wa siku muishi Kwa masimango yasiyoisha.
 
Tulioana miaka kadhaa iliyopita na tumejaaliwa watoto wawili. tTulioana mke wangu akiwa na mtoto mmoja aliyezaa akiwa kwao. Miaka ya mwanzoni uchumi uliruhusu kutoa huduma hata kwa mtoto wake ambaye anaishi na mjomba wake, baada ya uchumi kuyumba nikamwambia mwenzangu ongea na shangazi yake mtoto amwambie kaka yake aanze kumhudumia mtoto wake.

Nilifanya hivyo kwasababu sikutaka mke wangu awasiliane moja kwa moja na mzazi mwenzake, mke wangu akakataa akasema hawezi kufanya hivyo. Miezi kadhaa akaja akaniambia alishamtafuta mzazi mwenzake ila alimjibu vibaya, hivyo hana mpango wa kumtafuta tena na namba zake amefuta.

Nikamuuliza mbona nilikwambia umtafute dada yake ukakataa, ilikuwaje ukaanza kuwasiliana na mhusika moja kwa moja? Akajitetea yakaisha, lakini moyoni nikawa na mashaka. Ikabidi nianze kufanya uchunguzi kimya kimya nijue kinachoendelea,

Mungu sio mwanasiasa, kuna siku alikuwa ameenda shamba halafu akasahau simu nyumbani. Nikaanza kuipekua ndipo nikakuta simu ambazo yeye alikuwa akimtafuta mzazi mwenzake, pia nilikuta jumbe alizomtumia wifi yake akilalamika kwamba mzazi mwenzake hapokei simu, na baadaye jumbe ambazo zinaonyesha kwamba tayari wamewasiliana na jamaa na kakubali kwamba atakuwa anatoa hela za ada pamoja na mahitaji mengine.

Aliporudi nikamuuliza kwanini unarudia kosa lile lile mara ya pili, mimi ndiye niliyekupa ushauri halafu hutaki kunishirikisha kwanini? Je, nikisema unamtafuta kwa ajili ya usaliti nitakuwa nakosea? Kama kawaida yake akaanza kujitetea, lakini utetezi wake haukuiniingia moyoni, ikabidi nifanye maamuzi haya;

Nikamwambia hivi, "Sitolala na wewe bila kutumia condom usije ukaniletea maradhi, hawa watoto wawili wanatosha ukitaka mtoto kazae na huyohuyo mzazi mwenzako, na mimi nikitaka nitamfuta wa kuzaa naye".

Sasa yeye anadai namnyanyasa, namuonea kwasababu ana mtoto aliyezaa na mwanaume mwingine, na hataki kukubaliana na maamuzi yangu. Ila mpaka sasa wanaendelea kuwasiliana na mzazi mwenzake kuhusiana na masuala ya mtoto wao.

Je, nani mwenye kosa hapo, mimi au yeye?
...mke kama huyo unamuhamisha kabisa chumba(kama mnavyo viwili atabanana na wanae huko huko) na harakati za nyumba ndogo ya malengo zinaanza chap.
 
Kama kweli huyo mkeo yupo humu basi anisome hapa....

Kifupi hujawahi kumpenda, ulimtamani tu ukamuoa na bahati mbaya umeshamchoka. Na upo kumtafutia sababu.

Kama zinamtosha kichwani ajiongeze, atulize akili ajue namna ya kulea wanae na asiweke kipaumbele mambo ya ndoa.

Ni wanaume wachache sana wanahimili mwanamke mwenye mtoto, wengi hawawezi kiasi kwamba hata mwanamke akikosea kitu ambacho mwanamke asiye na mtoto/watoto angekosea linakuja jibu la ndio tatizo la single mothers.

Sasa wewe mwenye huyu mume, na wengineo, akili zenu ziwe kwenye kulea watoto wenu sio kuwaza ndoa mwisho wa siku muishi Kwa masimango yasiyoisha.
Acha kuwa negative, makubaliano yao yalikuwa asiwasiliane na mwenza wake moja kwa moja bali apitie kwa dada ake, kwanin huyo mama alifanya kinyume? Tuanze hapo
 
Kama kweli huyo mkeo yupo humu basi anisome hapa....

Kifupi hujawahi kumpenda, ulimtamani tu ukamuoa na bahati mbaya umeshamchoka. Na upo kumtafutia sababu.

Kama zinamtosha kichwani ajiongeze, atulize akili ajue namna ya kulea wanae na asiweke kipaumbele mambo ya ndoa.

Ni wanaume wachache sana wanahimili mwanamke mwenye mtoto, wengi hawawezi kiasi kwamba hata mwanamke akikosea kitu ambacho mwanamke asiye na mtoto/watoto angekosea linakuja jibu la ndio tatizo la single mothers.

Sasa wewe mwenye huyu mume, na wengineo, akili zenu ziwe kwenye kulea watoto wenu sio kuwaza ndoa mwisho wa siku muishi Kwa masimango yasiyoisha.
umeandika nini wewe? umesoma vizuri mada? MKe anawasiliana na Mume wa kwanza kwa siri! je hilo nalo linavumilika kama ambvyo unataka kutuaminishia wewe. kuhusu hawa masingle mother?
 
Ulimtuma kwa wifi yake eeeeh[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wewe buana unzingua sana..... yaani sijui upoje[emoji849][emoji849][emoji849]
Ulitaka nimtume kwa nani?
 
Back
Top Bottom