Mke na mume tumeleta mashtaka kwenu

Mke na mume tumeleta mashtaka kwenu

Nitapata mjinga mwenzangu,huyu mwenye akili kama zako simuwezi,kwa jinsi ulivyonikomalia nimeshajua wewe ni mwanamke wa namna gani,kama umeolewa basi mumeo ni bwege fulani hivi unampelekesha tu utakavyo.
Tatizo lako unapenda kusifiwa yaani niandike hiyo roho yako ya ubaguzi ni nzuri umeniuzi ulipo sema mtoto wao mkuu acha ROHO MBAYA
 
Kwanzani serious kuwa mkeo yupo humu na anatumia IDs gani mnk naona Kama utani tu
 
Wewe ndio mwenye matatizo, muache huyo mama endelea na maisha Yako.

Kama huwezi kuishi na mwanamke mwenye mtoto ni heri umuache! Ulijua ana mtoto tangu mwanzo, uchumi umebadilika unasema huwezi kumlea mtoto wake. Je ingekuwa ni wanao wote wawili na uchumi umebadilika ungefanyaje?

Huwezi kujisimamia kimaamuzi, umelazimisha mwenyewe waanze kuwasiliana.

Mwisho mwanamke mwenye mtoto hata umpe Kila kitu ila mtoto wake hapati huduma, hawezi kuridhika kuona yeye anaishi vizuri mtoto wake haishi vizuri au hajui kesho ya mwanae. Labda kama mwanamke asiyejitambua.

So wanaume kama hamuwezi kuwatunza wanawake wenye watoto ni heri muwaache tu, msiwaongeze mizigo ya watoto wengine Kisha muanze kuwageuka.
Uko sahihi Kabisa. Hakuna mwanamke anaetelekeza mtoto
 
Jipeni likizo kila mmoja aende kwao, baada ya miezi 6 muanze kutafutana tena. Wakati wa likizo we gonga huko nje kadiri uwezavyo, na mwenzako naye agongwe huko nje kwa namna awezavyo. Mkija kukutana, akili itakuwa imekaa sawa
 
Kwakuwa naye anasoma hizi comments naamini atalifanyia kazi,aniache aendelee na maisha yake,mzazi mwenzake anapotaka kutoa huduma kwa mwanaye sio lazima awasiliane na yeye,kaka yake ambaye anaishi na mtoto yupo kwanini asiwe anawasiliana na huyo? Mke ni ni mume mmoja tu kuwasiliana na wanaume wawili hiyo ni ndoa ya wanaume wawili mimi sipo tayari.
wewe huna kosa,ila mkeo siyo mstarabu na ameshindwa kujiongeza,kama ulimpenda pamoja na kuwa ana mtoto kwa mwanaume mwingine,haitakiwi yawepo mawasiliano ya moja kwa moja,ya yeye na baba wa mtoto,awe anawasiliana na eiza,,anko,babu,bibi nk.
 
Ana ubaguzi wa watoto inaonesha alibagua sana huyo mtoto kisa baba yake ana wasiliana na Mama yake
Unakurupuka tu ,nitambaguaje hali ya kuwa siishi naye nyumbani kwangu?
 
Kama kweli huyo mkeo yupo humu basi anisome hapa....

Kifupi hujawahi kumpenda, ulimtamani tu ukamuoa na bahati mbaya umeshamchoka. Na upo kumtafutia sababu.

Kama zinamtosha kichwani ajiongeze, atulize akili ajue namna ya kulea wanae na asiweke kipaumbele mambo ya ndoa.

Ni wanaume wachache sana wanahimili mwanamke mwenye mtoto, wengi hawawezi kiasi kwamba hata mwanamke akikosea kitu ambacho mwanamke asiye na mtoto/watoto angekosea linakuja jibu la ndio tatizo la single mothers.

Sasa wewe mwenye huyu mume, na wengineo, akili zenu ziwe kwenye kulea watoto wenu sio kuwaza ndoa mwisho wa siku muishi Kwa masimango yasiyoisha.
single mother jiongezeni,ukienda kwa mtu,nenda mazima,usigeuke geuke nyuma,,nimemaliza.
 
Sema jambo la kulea mtoto asiyo wako nacho kipaji ujue,harafu mapka unajiweka kwa single mother unafuata Nini ela au?ujui alikotoka kimemtoa Nini,

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Bro si tulielewana single mama hawaolewi, una zaanae tu hukohuko unahudumia, hata akiwa cha wote haina neno lakn unaoa kabisaa,
Pia tulisema tu utaoa kama umeona sheti ya kifo cha baba na umeonyeshwa kaburi vinginevyo pole, sana umekiuka katiba hakuna rangi utaacha kuona sasa
Nilioa mjane mkuu,nilijua mtoto aliyekuwa ni wa Marehemu kumbe alishazaa kabla hajaolewa.
 
Tulioana miaka kadhaa iliyopita na tumejaaliwa watoto wawili. tTulioana mke wangu akiwa na mtoto mmoja aliyezaa akiwa kwao. Miaka ya mwanzoni uchumi uliruhusu kutoa huduma hata kwa mtoto wake ambaye anaishi na mjomba wake, baada ya uchumi kuyumba nikamwambia mwenzangu ongea na shangazi yake mtoto amwambie kaka yake aanze kumhudumia mtoto wake.

Nilifanya hivyo kwasababu sikutaka mke wangu awasiliane moja kwa moja na mzazi mwenzake, mke wangu akakataa akasema hawezi kufanya hivyo. Miezi kadhaa akaja akaniambia alishamtafuta mzazi mwenzake ila alimjibu vibaya, hivyo hana mpango wa kumtafuta tena na namba zake amefuta.

Nikamuuliza mbona nilikwambia umtafute dada yake ukakataa, ilikuwaje ukaanza kuwasiliana na mhusika moja kwa moja? Akajitetea yakaisha, lakini moyoni nikawa na mashaka. Ikabidi nianze kufanya uchunguzi kimya kimya nijue kinachoendelea,

Mungu sio mwanasiasa, kuna siku alikuwa ameenda shamba halafu akasahau simu nyumbani. Nikaanza kuipekua ndipo nikakuta simu ambazo yeye alikuwa akimtafuta mzazi mwenzake, pia nilikuta jumbe alizomtumia wifi yake akilalamika kwamba mzazi mwenzake hapokei simu, na baadaye jumbe ambazo zinaonyesha kwamba tayari wamewasiliana na jamaa na kakubali kwamba atakuwa anatoa hela za ada pamoja na mahitaji mengine.

Aliporudi nikamuuliza kwanini unarudia kosa lile lile mara ya pili, mimi ndiye niliyekupa ushauri halafu hutaki kunishirikisha kwanini? Je, nikisema unamtafuta kwa ajili ya usaliti nitakuwa nakosea? Kama kawaida yake akaanza kujitetea, lakini utetezi wake haukuiniingia moyoni, ikabidi nifanye maamuzi haya;

Nikamwambia hivi, "Sitolala na wewe bila kutumia condom usije ukaniletea maradhi, hawa watoto wawili wanatosha ukitaka mtoto kazae na huyohuyo mzazi mwenzako, na mimi nikitaka nitamfuta wa kuzaa naye".

Sasa yeye anadai namnyanyasa, namuonea kwasababu ana mtoto aliyezaa na mwanaume mwingine, na hataki kukubaliana na maamuzi yangu. Ila mpaka sasa wanaendelea kuwasiliana na mzazi mwenzake kuhusiana na masuala ya mtoto wao.

Je, nani mwenye kosa hapo, mimi au yeye?
Wivu ukizidi, mapenzi hupungua!. Umezidi sana wivu!. Ukioa mwanamke mwenye mtoto, lazima wazazi wenza wazungumze wellfare ya mtoto. Usiwe na wivu, mwamini mkeo ni wanazungumza tuu issues za mtoto na sio kukumbushia!.

P
 
Hapo Kaa chini mtafute suluhu ya namna hii,aongee na mzazi mwenzie amchukue mtoto akaenae yeye Tena kwako aje likizo tu kuwaona ,sasa hapo Kama bado watakuwa wanawasiliana basi kaka huna chako mruhusu aende akae nae nawewe uwee unafuatilia tarifa za watoto wako aone inavyouma.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
nae inabidi abaki na wanae
 
Back
Top Bottom