Mke wa balozi Daraja auawa; Mfanyakazi wa nyumbani atafutwa

Kocha Wenger...mbona umemkomalia sana huyo msaidizi? Yaani huoni uwezekano wa wengine....unaanza kunikumbusha yale ya akina Malvo na mwenzake maana jamaa walikomalia na profile za ma serial killer huku wakiwaacha jamaa waendelee kufanya uhalifu wao...
 
kama ni vitasa vya namna hiyo ilikuwaje balozi na dereva wake washindwe kufungua toka nje?
mie naona balozi pia angetaja mda kamili (late evening) angeweza kusaidia kidogo kutoka na hali halisi ya pirika za mtaani zinavyoendelea lazima majirani wangeona matukio ambayo sio ya kawaida yanendelea kwa muheshimiwa sana sana swala la ujambazi.
 
alikimbiaje halafu akafunga mlango kwa ndani?
Uwezekano ni kwamba huyo jamaa aliruka ukuta. hata hivyo mbona mama alikutwa amefungiwa katika garage? Je huyo mama alijifungiaje humo? Hapa kuna walakini mkubwa sana!
 
Pole sana kwa wafiwa na mwenyezi mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.


d. The story:

Wacha we... .... MM Mwanakijiji mimi naona nisiseme maana kama wale walio ughaibuni wanaangalia FBI Files documentaries hapo iko kazi.

Bandugu angalieni hizo programmes ni muhimu sana kwa wale wanaoweza hasa walio USA, UK na popote pale ambako zinatolewa na hata askari polisi wetu ili kujua mbinu na mienendo ya uhalifu na jinsi ya kupata evidence etc.
 
Mh balozi aliwapigia simu watu gani siku hiyo ya tukio! conspiracy nyingine huenda aliwasiliana na wauwaji....mkewe alimpigia kuhakikisha job well done!
 
kinacho nifanya nimkomalie msaidizi kwa vile inaonekana ni wao wawili tu ndio waliokuwa kwenye nyumba.na yeye ndio anaweza kutoa ufumbuzi zaidi wa hii kesi la sivyo hapa hii issue haitopatiwa jibu.

sijamng'ang'ania kwa kumuhukumu lakini kama kuna mchezo mchafu wowote umefanyika ambao sio ujambazi yeye ndio mwenye jibu kamili na hawa wasaidiz mara nyingi hawana power kabisa na labda kaogopa hata akisema ukweli anaona kesi atatupiwa yeye.
 
Mh balozi aliwapigia simu watu gani siku hiyo ya tukio! conspiracy nyingine huenda aliwasiliana na wauwaji....mkewe alimpigia kuhakikisha job well done!
Jamani, this is NOT fair! Unauhakika gani?
 
Binafsi sitaki kumshuku mtu yeyote wakati huu wa msiba; ninachojaribu kuonesha ni kuwa simulizi lilivyo sasa (aidha kwa bahati mbaya au makusudi) lina matundu mengi kuliko pakacha. Ni matumaini matundu hayo yatazibwa ili tuweze kupata picha kamili kwa sababu..

Kama nimempigia mke wangu simu na baadaye nikajaribu sana kumpata siwezi.. nisingelala huko nilikokuwa hasa ukizingatia ni mtu mzima.. hata kama ingekuwa si ujambazi ingekuwaje kama ameanguka bafuni na hakuna mtu wa kumsaidia?
 
Tatizo media za bongo nazo haziaminiki kivile.Najaribu kujiuliza kuwa walimwona kuwa yumo garage wakiwa nje au baada ya kufungua mlango wa garage?Maana habari inaelekeza kuwa ni walimwona kabla ya kufungua mlango.Either pana dirisha hapo garage(huwa sio kawaida) au walichungulia chini ya mlango(inategemea na mlango ulivyo).Pia kama main gate ni la kufunga hata kwa nje then possibly muuaji alipita hapohapo na akafunga akiwa nje.Je simu ya mkononi ya marehemu imepatikana?Sijaona ikiongelewa kwani wanasema ni hizo tsh 2 mil(how accurate is this figure??).
 
Ni kifo cha kusikitisha sana, but naungana na yule ambaye ametaka tusitoe hukumu kwa houseboy, tusubiri kazi ya polisi. Poleni sana wafiwa.
 
.....
Kama nimempigia mke wangu simu na baadaye nikajaribu sana kumpata siwezi.. nisingelala huko nilikokuwa hasa ukizingatia ni mtu mzima.. hata kama ingekuwa si ujambazi ingekuwaje kama ameanguka bafuni na hakuna mtu wa kumsaidia?


Ki bongo bongo mbona kawa tu kumkosa mtu kwenye simu na ukalala usingizi. Labda huyo mpigiwaji awe mgonjwa mwenye kuhitaji uangalizi wa karibu. Vinginevyo watu kibao walala usingizi mnono wanapowapigia wake zao simu bila kuwapata.

Labda niulize, je simu ya marehemu ipo? Hiyo simu inaweza kutoa clue ya timeline ya tukio au kama kulikuwa na mawasialino yanayohusiana na tukio.

Pili, what if huyo mama balozi alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msaidizi wa nyumbani, ikapelekea kukorofishana na hata kufikia kumuua?

What if mama balozi alikuwa katili sana kwa msaidizi kiasi kufikia kijana kutaka kumkomoa dizaini ya wa wanavyofanya watu wa Mara?
 
what a sad day, for the family of the Daraja. Our prayers and grief are with you, as you go through this tough time. We will always remember you, as one of the respectable and warm hearted ladies during your time here in DC. May u rest in peace.
 
Polisi wa Tanzania sina imani nao ni wazembe sana utakuta tayari hata evidence nyingi zimekuwa tempered au hawakuchukua vitu ambavyo viko obvious. Utakuta wako more political aligned kuliko kufanya kazi zao kwa uadilifu.
 
Ki bongo bongo mbona kawa tu kumkosa mtu kwenye simu na ukalala usingizi. Labda huyo mpigiwaji awe mgonjwa mwenye kuhitaji uangalizi wa karibu. Vinginevyo watu kibao walala usingizi mnono wanapowapigia wake zao simu bila kuwapata.
kwa mke wako ni vigumu sana kupuuzia na kwenda kulala kama hajawapokea simu unless ni kawaida yenu kwamba mmoja wenu asipopekea simu nikawaida tu.kitu ambacho nakataa kuwa hivyo kwa mke wako lazima utakuwa na wasi wasi na kufanya juhudi zakujua kama yuko salama au hapana wakati huo huo.


maswali mengine ya nyongeza hapa,katika maongezi yao ya mchana je mke wake alikuwa nyumbani au alikuwa katoka? na kama alikuwa nyumbani je alikuwa na mpango wa kwenda popote? najua lazima mke na mume lazima wapeane ratiba.nauliza maswali haya kutoka na hivyo viatu na hand bag kukutwa karibu na geti je mama wa nyumba alikuwa anarudi nyumbani au alikuwa anatoka na kama kulikuwa na safari labda mume wake alimwambia katika maongezi yake.tukijua hapo sasa tunaweza kujaribu ku-connect dots kutoka hapo alipokuwepo mwanzo au alipokuwa anataka kwenda je watu waliomtegemea kuja baada kuona kimya wali-react vipi ?


kitu kingine kuna simu ya ndani? kama hipo mume wake alivyomkosa kwenye simu ya mkononi alijaribu simu ya ndani ? je mfanya kazi wa ndani alikuwa na cell phone? kama alikuwa nayo mume wake alijaribu kumpigia hili kujua kama kila kitu salama au kama mama wa nyumba yupo? nimeuliza hivi kutokana na watu wengi wana cell phone siku hizi kama hakuwa nayo hili swlai sio muhimu.
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao~AMEN. Huyu mfanyakazi si ajabu kashirikiana na Majambazi na kuna vitu ambavyo si ajabu vimeibiwa katika nyumba hiyo.
 
what if huyo mfanyakazi wa ndani naye ameuawa na kuburuzwa sehemu nyingine, au ametekwa n.k
 
what if huyo mfanyakazi wa ndani naye ameuawa na kuburuzwa sehemu nyingine, au ametekwa n.k

That is possible too Mkuu, wakati polisi wakiendelea kumtafuta mfanyakazi wa ndani majambazi ndiyo wanazidi kutokomea na kuharibu ushahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…