Jasusi.. that is the story we have been told; but in a situation like this there is a story behind the story. Ngoja nioneshe matundu machache kwenye stori ilivyo sasa.
a. The Story:
Kwa hiyo.. timeline yetu ni kuwa lolote lililotokea lilitokea siku ya Jumamosi kati ya mchana na jioni. Halikutokea usiku. Kama lilikuwa ni tukio la ujambazi na matumizi ya nguvu kiasi hicho hao majambazi watakuwa ni watu wa karibu sana kiasi cha kutokusababisha shuku toka kwa majirani mchana kweupe; na hiyo ina maana wapo mashahidi walioona kilichotokea, gari, watu n.k
Balozi alilala salama usiku ule bila kutoa taarifa polisi, kwa ndugu, jamaa na marafiki huku akiwa hana mawasiliano na mke wake na hajasema kama alijaribu kuwasiliana na msaidizi huyo wa nyumbani. (this is important to keep in mind)
b. The Story:
Sasa tunajua kuwa Balozi alilala salama usiku wote ule na hakufanya juhudi ya kupiga simu nyumbani siku ya pili wala kutoa taarifa kwa mtu mwingine yeyote. Muda huo unatoa nafasi ya mtu yeyote kutoweka na kuchelewesha uchunguzi.
Lakini pia tunaona jambo jingine muhimu kwa upelelezi. Malango ya nyumba ya Balozi yalikuwa yamefungwa kwa ndani. Sasa hapa hatuna budi kujiuliza huyo msaidizi wa nyumbani alitokaje na vitu vya kuiba halafu akafunga mlango kwa ndani kiasi kwamba mtu aliye nje anashindwa kuufungua?
La pili ni kuwa Balozi hana ufunguo wa mlango wa nyumba yake akiwa nje?
c. The Story:
Hapa kuna tatizo kidogo. Kwenye upelelezi tunaweza kusema ni kutokubaliana kwa eneo la tukio (inconsinstence of crime area). Viatu vya mhanga na mabegi yake yamekutwa karibu na geti. Vilifikaje hapo? Je mhanga aliuawa nje, aliwafukuza wahusika, hapa ni clue nzuri.. kulikuwa na damu karibu na geti?
d. The story:
So far.. tunachosikia hapa ni kwamba ndani ya nyumba na eneo zima hakukuwa na ushahidi wa foul play! Ina maana huyo mama hakuuawa ndani ya nyumba au nje ya nyumba kwani kama kungekuwa na damu au aina yoyote ya ushahidi kuwa amedhurika wangeita polisi mara moja. Kama walikuta ushahidi wa kitendo kibaya walipoingia ndani (hasa baada ya kukuta viatu vyake nje na mabegi) walitakiwa kutoa taarifa polisi mara moja, itakuwaje kama wabaya walikuwa bado wako ndani wanasubiri? especially baada ya kujua kuwa geti lilifungwa kwa ndani?