I know kwa upande wangu pia naunga mkono waondolewe bungeniMkuu najua lazima Kuna walio shiriki ila tayari wote kwa sauti Moja wamewafukuza hao wabunge (Akiwemo mke wa Kigaila) kwenye chama; so kama Dr Tulia akiheshimu maamuzi ya Baraza kuu it won't matter anymore maana wameshafukuzwa
Lakini pia natamani sana kujua namna mchezo ulivyokuwa je zile fomu za uteuzi kutoka kwenye Chama,Tume ilizipataje
Maana uwepo wa hawa wake wa viongozi ndani ya hao wanaoitwa wasaliti wa Chama kwa upande wangu inanifikirisha
Kwa upande wangu naamini watu wa pande mbili na wenye nguvu wameshirikiana kuingiza wale wadada bungeni na hao ndio wanajua picha mwisho litakuaje
Ndio maana nasema ni ngumu saaana Halima kwenda na wenzie kuapa bila kupewa back up ya pande zote mbili ni ngumu saana hili suala
Ila kwasababu ya siasa kila mtu atakaa upande anaoamini ila naimani chama kinawajua wasaliti mbali na hao wabunge 19.