Mke wa boss wako akikutaka kimapenzi, je utakuwa Mwaminifu? Jibu lako ndio Siri ya Anguko au Mafanikio yako

Mke wa boss wako akikutaka kimapenzi, je utakuwa Mwaminifu? Jibu lako ndio Siri ya Anguko au Mafanikio yako

Wenye biashara zao sasa hivi wapo busy kuzitumikia hata huu uzi hawajauona. Wengine wapo huko kwenye jukwaa la biashara.

😂😂😂

Mwambie pia Maxence Melo yupo humuhumu online kwenye Biashara yake ya mtandao.

Kuna Vijana wanafikiri kizamani Sana.
Hawajui wapo Watu kuwa online ndio biashara kwao.

Alafu huyo sio ajabu ana Shahada Fulani
 
Ahsante kwa ukumbusho wa kuendelea kutunza uaminifu wetu kwa wanaotuamini.

Ila kuna wakati matatizo au uhitaji hupelekea watu kuvunja uaminifu.

Mfano niliwahi kusimuliwa kuna jamaa Kurasini aliwahi kuiba baadhi ya vitu (deki, dvd players) kwa majirani zake mtaani ili apate nauli ya kwenda South na bahati nzuri alifanikiwa na huko alipoenda alipata mafanikio. Jamaa baada ya kurudi Tz kila familia ambayo aliipiga tukio wakati anaondoka alienda kuwafidia. Sasa mtu kama huyu tunamuweka kwenye kundi la waaminifu au wasio waaminifu?
 
Bado umesimama ukiwa umetekewa,
20141018_MAP004_0.jpg

tamaa na utashi wako vikipigana vikali nafsini Mwako. Je utamkubalia au utamkatalia MKE wa boss wako?
 
Kwa jinsi technology ilipofikia kwa sasa, unam record mazungumzo yote kisha unampelekea boss.

Kamwe usiruhusi ngono ikaharibu kibarua chako.
Kwa kweli hapa umeongea kitu.
Mimi lazima nimchome.

Siwezi fanya upuuzi kama huo, naamini Yusufu angekuwepo enzi zetu angemrekodi, asingefungwa na angekuwa mtu huru.

Uaminifu ni kitu ambacho hukupandisha kwenye daraja bora zaidi. Ukiwa mwaminifu Kwa binadamu au Kwa Mungu au Kwa Shetani , lazima watakupa zawadi, ndo hizi wengine wanapokea karama za rohoni wengine wanapandishwa kwenye daraja.
 
Back
Top Bottom