Mke wa Dkt. Mwaka asema yuko tayari kumuachia Dkt. Mwaka kila kitu mradi apate amani

Mke wa Dkt. Mwaka asema yuko tayari kumuachia Dkt. Mwaka kila kitu mradi apate amani

Bi Queen apiga magoti na kusema anachohitaji zaidi yeye kwa sasa ni Amani, na kwamba yuko tayari kumuachia Mwaka kila kitu ili abaki na amani na kulea watoto wake.

Amesema kuwa anatamani mwisho wao uwe na amani, na kama kuna chochote Dkt. Mwaka anakihitaji basi amwambia ni njia zipi apite lakini vitendo vya kupelekana polisi kutengenezeana kesi na kudhalilishana kwenye mitandao si kitendo kizuri, mitandao isitumike vibaya kudhalilishana.

Akiongeza kuwa kauli ya Dkt. Mwaka alivyosema kuwa 'bado anampenda lakini hayuko tayari kuishi na yeye' imetosha kabisa kuonesha kuna sababu nyingi za kufanya wao wasibaki pamoja.

Amuomba Rais Samia, viongozi wa serikali na viongozi wa dini wamsaidie ili apate haki yake awe huru na kupata amani.
Hii yote ni ujinga wa dini za kuletewa tu....hapa penzi limekwisha huyo Mwaka anamuwekea ngumu mwanamke ili iweje? Nashauri Mwaka akamatwe nakucharaza bakora si chini ya 1000 kwa kukataa kumuacha mtoto wa watu.
 
Sasa amejiingiza kwenye mtego wa Dr. Mwaka bila kutarajia.

Nadhani hakuwa anajua kwamba sio kama Dr. Mwaka haitaji waachane, ila ni mwamba hataki waachane kisha wagawane mali

Hii angeijua mapema angezichanga karata zake vizuri.

Hakuna aisee kuna nyumba SA imeandikwa kwa jina la mke tu ndio mmiliki!
Hapo ndio vurugu la mambo yote!
 
Wanawake wa mujini.
Hawa huwa wako tayari hata kuua kisa mali.
Tunawaita wadada wa mujini, yupo tayari kukana kila kinachomuhusu apate mali tuu shenzi.
Kama yule mwenzao kaua mtoto apate mali kapata Kawa kama kadata sasa[emoji16][emoji16][emoji16]ubwa kabisa hawa
Nani mkuu...Muna?
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? Kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Sasa mtu si hampendi tena na labda amepata mpenzi mpya
 
Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Ndio hivyo wapo wengi wa dizaini hio karne hii especially wa kutoka huko Chemba
 
Kwani kuna shida gani mtu akitaka kuachana na ndoa? Hata akiolewa kesho yake tatizo likwapi kama taratibu zimefanyika?
Kwanini mumlazimishe mtu ambae hataki, kwanini yaani
Tatizo sio kutaka tatizo ni kulazimisha lazima waachane means kuna mwamba anampresurize pembeni aachwe amuoe yeye, wanawake kutoka Chemba hatari sana
 
Kosa kubwa WALIOFANYA Waislam ni kukubali kufuata mahakama za Kizungu ambazo ni za kirumi na warumi.

Ndio za kiislama hua ni ndoa imara sana katika misingi ya dini ya kiislama inayosimamiwa na mahakama ya Kadhi.

Kukosekana Kwa mahakama ya Kadhi yanye mamlaka kamili kikatiba ni janga kubwa Kwa ndoa za kiislama kama zilivyo ndoa za kikristo.

Wanawake wengi wa Kikristo( makristo wa uongo ) wanaua waume zao wakishirikiana na watoto wao ambao wengi wamewazaa Kwa kutoka nje ya Ndoa. Wanawake wengi wa kikristo wanaona ufahari kuzaa nje ya Ndoa wengine wamezaa mpaka na watumishi wa makanisa lakini wanajificha kwenye mwavuli wa ndoa ya mke mmoja na kiapo Cha kutenganishwa na kifo huku wakibeba kauli mbiu ya KITANDA HAKIZAI HARAM.

Kwa Waislam ni dhambi kubwa kumdanganya mtoto baba . Yaani Mwanamke wa Kiislam haruhusiwe kumsingizia mtu mtoto. Yani mtoto wa X ni marufuku na ni dhambi kusema kuwa baba yake ni Y. Kama amezaliwa nje ya Ndoa anatajwa Kwa Jina la mama yake.
Haya ni mafundisho mazuri ambayo Waislam hawaifundishi jamii ikauelewa uislam matokeo yake jamii imetekwa na uzungu na upagani wao na mambo ya hovyo hovyo yameingia kwenye ndoa na Wahanga Sasa ni jamii nzima.
Mahakama ya kadhi bila utawala wa kiislam uliona wapi wdwe?
 
Mtu akishataka talaka mpe, uislam unataka mwanamke akipewa talaka akae eda kabla ya kuolewa Tena..eda inaanzia miezi mitatu
Akimuacha tu achukui round kuna mwamba anamuweka ndani hakuna kisingizio sijui watoto kufanya nini, kuna mmoja alishawahi anakupenda Chama kuliko watoto sasa watoto ni nini wakati ameshapata mshedede mwingine wa kumsugua
 
Tatizo sio kutaka tatizo ni kulazimisha lazima waachane means kuna mwamba anampresurize pembeni aachwe amuoe yeye, wanawake kutoka Chemba hatari sana
Sawa, kama ni hivyo ndo usimle talaka? Ndo unampa vizuri ili aende zake maana ukiendelea kukaa nae kilazima ni kujitafutia majanga. Let her go
 
Sawa, kama ni hivyo ndo usimle talaka? Ndo unampa vizuri ili aende zake maana ukiendelea kukaa nae kilazima ni kujitafutia majanga. Let her go
Wanawake wa Chemba pasua kichwa
 
Kwani kuna shida gani mtu akitaka kuachana na ndoa? Hata akiolewa kesho yake tatizo likwapi kama taratibu zimefanyika?
Kwanini mumlazimishe mtu ambae hataki, kwanini yaani
Huyo mwanamke kama aliolewa bila kujua maana ya ndoa, hilo ni kosa lake, sio la Dr. Mwaka.

Taratibu unazosema kufanyika moja wapo ndio mpaka Dr. Mwaka atoe talaka, sio nje ya hapo.

Ndoa sio kama shati unalovaa, ukilichoka unaenda dukani kununua jingine, ndoa ni kuvumiliana.

Kama akiachwa aondoke hapo aende sehemu nyingine, kisha aseme tena amechoka after few days, huo utakuwa ni uhuni, na dini inayojielewa haiwezi kukubali hilo.

Mwanamke atulie kwa mume wake, kama amechoka akili amuombe mume wake ampeleke Dubai akatulize kichwa, akirudi aingie jikoni kumpikia mume, full stop.
 
Ha haa sa mbona kama mnamlazimisha? Ndo hataki tena sasa🤣🤣🤣🤣🤣
Mwaka atoe talaka
 
Unatakiwa utambue fika; ndoa hailazimishwi! Ndoa ni makubaliano ya pande mbili. Kama ikitokea upande mmoja hauridhishwi, talaka haikwepeki.

Huwezi kumlazimisha huyo mwanamke kuendelea kumpenda mtu ambaye kwa wakati huu, hayupo moyoni mwake. Kama alivyosema; ni vizuri akasaidiwa ili aachane na huyo mume wake kwa amani, na hivyo kuendelea na maisha yake ya amani.
Mnachochea uhuni tu, huwezi kusema umemchoka mumeo kama unavyoichoka nguo unayovaa, na huko anakotaka kwenda tena aje kusema amechoka baada ya muda fulani, huu mnaotetea hapa ni uzinzi tu, akae na mumewe atazoea maisha yataenda vizuri.
 
Nani mkuu...Muna?
Naam... Kawa kama kadata now.
Kuna muda anatamani heri mtoto wake angekuwepo.
Anajitahidi kuonyesha kwamba anafurahia maisha ila kiukweli anapitia kipindi kigumu sana yule dada cha 90% huzuni na majuto na 2% robo ya furaha
 
Back
Top Bottom