Mke wa Dkt. Mwaka asema yuko tayari kumuachia Dkt. Mwaka kila kitu mradi apate amani

Mke wa Dkt. Mwaka asema yuko tayari kumuachia Dkt. Mwaka kila kitu mradi apate amani

Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? Kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Kwani ndoa ni utumwa?

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Amesema kuwa anatamani mwisho wao uwe na amani, na kama kuna chochote Dkt. Mwaka anakihitaji basi amwambia ni njia zipi apite lakini vitendo vya kupelekana polisi kutengenezeana kesi na kudhalilishana kwenye mitandao si kitendo kizuri, mitandao isitumike vibaya kudhalilishana.

Akiongeza kuwa kauli ya Dkt. Mwaka alivyosema kuwa 'bado anampenda lakini hayuko tayari kuishi na yeye' imetosha kabisa kuonesha kuna sababu nyingi za kufanya wao wasibaki pamoja.
Poleni akina Mama lakini msiwe kama yule dc aliyekwenda kuolewa Pangani
 
Talaka ni haki ya kila mmoja aliyepo ndani ya ndoa ikifikia hatua hiyo! Mamlaka ya Muumba yanaruhusu na hata mamlaka ya nchi yanaruhusu.

Kama kweli huyu dada anachokisema kinatoka moyoni na hana hatia juu ya hili, basi huyo Mwaka ajitafakari.

Hili jambo limeibua madhaifu mazito kwenye taasisi “nyeti” 2 ambazo kwa kiasi kikubwa ni mihimili muhimu katika ujenzi wa familia, jamii na taifa kwa ujumla!!

Ndoa na Uislam.

Tunaendelea kujifunza at the expense ya watoto! Mungu tuongoze.
Wananchi wamegawanyika

Kuna wanaotaka ndoa isivunjike.

Kuna wanokubali matokeo ndoa ivunjike.

Acha tuone
 
Kataa ndoa ewe kijna wa kizaz hiki ndoa ina utapeli ndani yake
 
Uislam ulipowafikia waarabu waliupinga,wakimpiga Vita mtume,walidai upo tofauti na utamaduni wao... uislam siyo uarabu ewe punguani
Nimekuelewa vizuri sana

Tatizo la Waislam hawautangazi uzuri wa dini ya Kiislam .
Waislam wengi wanatumiwa na Watawala madhalimu Kwa manufaa yao.

Mfano Mahakama ya Kadhi unapigwa vita mpaka na watawala Waislam wakati wanajua ni takwa la kiimani na kidini.

Jambo jengine ni Biashara na mabenki Dini ya kiislam imeelekeza vizuri sana kuhusu Mikopo na Riba lakini Muislam akiupata Urais au uwaziri wa Fedha Hana muda Tena wa kueleza uzuri wa Mikopo isiyo na Riba na banki zinazofuata mfumo wa Kiislam. Muislama wangeweka pembeni unafiki na kusimamia ukweli uliopo kwenye vitabu vya dini hata mabeberu yange badilika na kuwa na hofu ya Mwanyezi Mungu.

Wengi wanachanganya kati ya uislam na Mila za Kiarabu .

Kushindwa kupambanua Mila za watu na maagizi ya Mwanyezi Mungu ndiko kumewafanya wakristo kukengeuka na Sasa wengi wanamuabudu Shetani wakiona uzungu ndio Ukristo.
 
Kwenye mazingira kama haya sio kila mwanaume anayekataa kutoa talaka ni kwamba anampenda sana mkewe, bali anaweza kuwa anatumia hiyo njia kumuadhibu huyo mke baada kuchezewa rafu mbaya sana.
Kuna rafu nyingine mume akichezewa na mkewe na anaona akimpa talaka ndio kama kamtunuku zawadi ya alichokuwa akikitafuta hivyo kuamua kumuadhibu kwa kutompa talaka huku akiwa ameshamchukia vibaya., ni kama kumweka kifungoni kwa kosa alilotenda .
Kwa lugha ya mfano ni kama kumkamata mwizi nyumbani kwako kaiba kitu halafu ukamfungulia mlango mwenyewe atoroke..
 
dini ya wisilamu inatambua kuwa kila kitu kina mwisho hata haya maisha tunayo ishi yana mwisho

hivio basi ndio katika wisilamu sio jela wala adhabu kama mwanamke anaone awezi endelea kuishi na huyo mume wake kutokana na sababu mbali

akaona akiendelea kuishi nae atomtii mume huyo hivio akaisi kupata dhambi sher,iya inampa ruhusa mwanake huyu kujivua yana kurudishia mumewe mahari yake hili hawe huru kama hana anaweza kupewa na kaka zake baba yake mama hata watoto wake

huo ndio ubora wa mwanamke kuolewa kwa kiasi kidogo hili akiona hana mume anamzingua anarudishia chake anasepa atakako

lakini kama mke huyo anafanyia hila hili aachike bila sababu mwanamke huyo akifa hawezi iona pepo ya allah makazi yake yatakuwa motoni milele

ifaamike talaka iko kwa dini wauwisilamu tu sio vinginevio sababu dini nyingine hazina mfumo huo
Bro hujui kuandika?
 
Kosa kubwa WALIOFANYA Waislam ni kukubali kufuata mahakama za Kizungu ambazo ni za kirumi na warumi.

Ndio za kiislama hua ni ndoa imara sana katika misingi ya dini ya kiislama inayosimamiwa na mahakama ya Kadhi.

Kukosekana Kwa mahakama ya Kadhi yanye mamlaka kamili kikatiba ni janga kubwa Kwa ndoa za kiislama kama zilivyo ndoa za kikristo.

Wanawake wengi wa Kikristo( makristo wa uongo ) wanaua waume zao wakishirikiana na watoto wao ambao wengi wamewazaa Kwa kutoka nje ya Ndoa. Wanawake wengi wa kikristo wanaona ufahari kuzaa nje ya Ndoa wengine wamezaa mpaka na watumishi wa makanisa lakini wanajificha kwenye mwavuli wa ndoa ya mke mmoja na kiapo Cha kutenganishwa na kifo huku wakibeba kauli mbiu ya KITANDA HAKIZAI HARAM.

Kwa Waislam ni dhambi kubwa kumdanganya mtoto baba . Yaani Mwanamke wa Kiislam haruhusiwe kumsingizia mtu mtoto. Yani mtoto wa X ni marufuku na ni dhambi kusema kuwa baba yake ni Y. Kama amezaliwa nje ya Ndoa anatajwa Kwa Jina la mama yake.
Haya ni mafundisho mazuri ambayo Waislam hawaifundishi jamii ikauelewa uislam matokeo yake jamii imetekwa na uzungu na upagani wao na mambo ya hovyo hovyo yameingia kwenye ndoa na Wahanga Sasa ni jamii nzima.
 
Kumbuka hio ni ndoa ya kiislamu so talaka inaruhusiwa na kuolewa tena inaruhusiwa pia

Kwani kuna tatizo akiolewa tena?

Mkichokana msisubirie mpaka muuane.

Mwanamke keshamchoka mwaka so mwaka atoe talaka bibie awe huru
Talaka inaruhusiwa ndio lkn sio kizembe hivyo, someni Quran vizuri muelewe.
 
Aache kutafuta huruma ya rais, akae kwa kutulia. Kwani aki step aside bila talaka hatoipata hiyo amani? Mwanamke mpumbavu huibomoa ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? Kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Unajua mwanamke ni kiumbe wa kumtazama mara mbili mbili sana. Nilikuwa sielewi kwann sheria za kislam zinasema hata mahakamani ushahidi wa mwanamke m'moja hautoshi kumtetea bali ushahidi wa wanawake wawili sijui watatu ndio unalingana na ushahidi wa mwanaume m'moja.

Huyu dada ndie ameanza kuleta haya mambo mitandaoni saa hii analalamika kuwa Dkt. Mwaka ndio anamshambulia mitandaoni sasa nani aliyeyaleta huku kama si yeye?

Hapo anasema yeye anataka amani tu hataki mali wala nini, huu ni uongo tena wa uzito mkubwa sana. Kilichomleta katika hayo mahusiano ni mali how come atoke kapa, hiyo haitawezekana, hiyo ni mbinu mkakati. Ukiona mwaka anakomaa kutokutoa talaka basi kuna shida upande wa mwanamke.

Wanaume mwanamke akizingua ni dakika moja tu kumuandikia talaka asepe. Ila ukiona mwanaume anagoma kutoa talaka it means kuna jambo linaendelea na huyu dada anajaribu kukwepa hilo jambo.

Shida ya wanawake ni kutaka huruma za jamii na kuonewa huruma ila nyuma ya pazia huku ukija kufahamu mchango wake katika majanga anayosababisha ndipo utaelewa ni kwann kunatokea utofautiano.

Kwann ana ng'ang'ania watoto?!

Anakwenda kuanza maisha wapi na kwa mtaji upi?! Dkt Mwaka asipokuwa makini huyu mwanamke atamharibia jina na reputation yake aliyoijenga kwa gharama. Hii ndio shida ya mwanamke kwenye maisha ya mwanaume. Anakuja kuharibia sio kukujenga au kukupa mchango wa kuboreka hapana.

Tuwe makini sana. Diamond Platinum hadi leo hajaoa mnaona anavyotoboa maisha tokea akiwa bwana mdogo. Na kuhakikishia diamond Platinum akisema tu aweke mwanamke ndani au wanawake ndani, atafilisika miaka si mingi na atarudi kuwa zero na huyo mwanamke au wanawake watamuacha kama takataka. Kinachomsaida Diamond ni mama yake yupo pale na dada zake wameweka ulinzi mkali sana wa mali kwahiyo hakuna mdangaji anafanikiwa akija pale, wanaambulia mimba tu kwisha habari. Tena mimba zenyewe wanategeshea ili walazimishe maisha.

Wanawake wa sasa ishi nao kwa formula tofauti sana achana na story zinazowapamba kuwa ni viumbe wenye huruma, sijui akipenda anapenda kweli, sijui ukitaka baraka sijui kuwa na mwanamke wako, huu ni mtego tena mtego mbaya sana.

Thamini pesa zako na mifumo yako ya kupata pesa ndio uipe attention na upendo hiyo ndio itakulinda hadi uzeeni miaka 90 au 100 huko watu kama akina diamond unawaona wanaheshimu pesa zao tazama anavyokwenda fresh,anawala kama nini na anaishi vizuri tu,mama yake yule pale anafaidi matunda ya mwanae. Tazama Zari anajinadi anapesa ila ona anavyolalamika diamond hampi pesa,sasa jiulize pesa za nini na mtu amepaki gari za bei anasema anafanya biashara na anapesa, ndio uone mwanamke ana interest zake katika mahusiano sio wewe mwanaume.

Ukiwa na pesa utapata mtu wa kukuhudumia vizuri tu, wapo watu atakubali kuja kukuhudumia kwa malipo ya kawaida kabisa. Sasa jidanganye na hizi mbaga za hawa wasema chochote wakati tunaona wanaume wenzetu ambavyo hawatoboi hata miaka 50 salama wanakuwa wameshachakaa lawama kibao na kutengwa juu. Hakuna mwanamke atakupenda wewe ile ya mapenzi ya kweli kabisa, hao wanawake alikuwapo ila sio miaka hii kwa malezi haya ya kidangaji na kuthamini mali na pesa, mwanamke mbele ya mali anachagua mali wewe ni kitu gani tena hauna thamani yoyote kwake.

Kama vipi apite hivi.
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? Kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Ndio amani yenyewe hiyo...we unataka umpe amani ?! Amani ninkitu kinatoka ndani yake!
 
Wanaendelea kijicholesha tu bure, media ya bongo ndo inavyo penda bora akae kimya tu yataisha tu, kama kweli hana mapenzi na huo bwana.
Kabisa na kuwa dhalilisha wana familia na watoto sijui wana rithishwa nini hapo, Mungu atusaidie sna na kutujaalia hekima na busara ktk haya maisha yetu. Marehemu Baba yangu aliwahi niambia ukiwa na hasira jizuie kusema utaweza sema neno likakugharimu ktk maisha yako. RIP Baba.
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? Kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Ushauri kama huu ndio unawaponzaga wanawake wengi, eti arudi wayamalize unataka mpaka aje kuuliwa ndio mjue kwamba kulikuwa hakuna amani katk ndoa yake?

Mwanamke akishakuchoka achana naye la sivyo unajitagutia matatizo tuu.
 
Wanawake wa mujini.
Hawa huwa wako tayari hata kuua kisa mali.
Tunawaita wadada wa mujini, yupo tayari kukana kila kinachomuhusu apate mali tuu shenzi.
Kama yule mwenzao kaua mtoto apate mali kapata Kawa kama kadata sasa😁😁😁ubwa kabisa hawa
 
Back
Top Bottom