Akihojiwa na Katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM,Dk Mwaka amesema kwamba ndoa yake mpaka sasa haijavunjwa kwa sababu Sheikh wa mkoa hana mamlaka ya kuvunja ndoa bali Kadhi.
Mashauri ya ndoa hushughulikiwa na kadhi kuanzia ngazi ya kata,wilaya,mkoa na Taifa,hivyo anahoji huyo Sheikh katoa wapi mamlaka ya kuvunja ndoa?
Huku akiwa ameambatana na mkewe, Dk Mwaka alisema kwamba kama huyo Sheikh angekuwa smart angalau angelipeleka kwa Kadhi ndio baadae atangaze baada ya Mahakama ya Kadhi kutoa hukumu, lakini he was not that smart.
Aliendelea kuhoji, hilo baraza lililiovunja ndoa yangu ni lini liliwahi kunisulihisha Mimi na mke wangu?Ndoa huvunjwa baada ya mashauri kufanyika kwanza,wakishindwa shauri hupelekwa kwa Kadhi ambae nae baada ya kutusikiliza wote ndio hutoa hukumu.
Kwahio hili baraza halina mamlaka ya kuvunja ndoa yoyote,mwenye mamlaka ya kuvunja ndoa ni Mahakama ya Kadhi baada ya jitihada za kusuluhisha kushindikana,huko nako bado sijawahi kuitwa japo mke wangu alipeleka shauri.
Je, utaratibu ukoje wadau?