Juma Said Mfaume, mkazi wa Mbagala Mlandizi, Pwani, amefariki dunia baada ya kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa Kampuni ya OYA Microcredit. Tukio hilo lilitokea alfajiri ya Jumanne, tarehe 8 Oktoba 2024, wakati wafanyakazi hao walipofika nyumbani kwake kudai marejesho ya mkopo wa Tsh 60,000 ambao mke wa Juma, Khadija, alikuwa ameshindwa kulipa kikamilifu.
Baada ya mabishano, wafanyakazi hao walitaka kuingia ndani ili kuchukua mali kama fidia ya mkopo. Juma alikataa, hali iliyosababisha ugomvi ambapo mmoja wa wafanyakazi hao alimshambulia Juma kwa kigongo shingoni. Baada ya kuanguka, walimbeba na kumpeleka hospitali, ambako alipoteza maisha.
Khadija, mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyochukua mkopa huo
Soma:
=>
Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji