Mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyokopa

Mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyokopa

Jambo hili la mikopo ya kifedhuli liliwahi kujadiliwa bungeni na kauli ikamtoka waziri Mwigulu kuwa hawa jamaa ni wahuni na hawana vibali vua kufanya hivyo.

Nani anawapa leseni ya kuendesha kampuni hizo?

Mwisho wa siku, hakuna kampuni inayotoa mikopo ilikunufaisha wakopaji. Wao nawataka wakunyonye usishe ufe uzikwe.
 
Ila hawa jamaa lakini, walishidwa hata kumpiga miguu mpaka washambulie shingo kweli? Hapa kesi ya kuua kwa kusudia inawakwepa kweli?
Hiyo ni bahati mbaya inayotokana na umaskini. Wote hao marehemu aliyegomea deni la elfu sitini, mke wa marehemu aliyekopa na hao wafanyakazi. Wafanyakazi wanalipwa kidogo, wanapewa malengo ya makusanyo makubwa, wana hali ngumu bila kulazimisha kulipwa hawapati kamisheni na wanapunguzwa kazi kuonekana hawasaidii kampuni.

Huo ni umaskini wa kijamii unagusa kila mtu.
 
Leseni ya kutoa mkopo ..then unaua amejiharibia brand
Hawatengenezi brand hawa hamna kilichoharibika. Wanaokopa wana njaa hawatafuti brand wanatafuta hela tu.
Mtaani umaskini ni mkubwa sana hayo mambo ya kizungu ta boycott sijui susa bidhaa hayapo bongo, mtu ana shida ya hela anataka akope wewe umwambie hii kampuni iliua mtu, wakati shida zinataka kumuua.
 
Ukigongwa na gari la CocaCola utataka kampuni ifungwe sababu haikupewa kibali cha kugonga watu?

Hayo makosa ya wafanyakazi sio maelekezo ya kampuni. Yeye alileta ugomvi wakamzidi bahati mbaya na sheria ichukue mkondo wake. Kampuni haiwezi fungwa kwa makosa binafsi ya wafanyakazi wake.
Scenario yako ni tofauti na kilichotokea
Hawa oya kazi yao ni kutoa mikopo
Mtu akashindwa kulipa,
Kuna njia za kudai ambazo sheria zimeweka kama kuchukua security au la kumpeleka mahakamani
Huwezi kurecover hela kwa kutumia nguvu,
Ni sawa coca cola kutuwekea maji machafu kisa kuna uhaba wa maji ,ni nje ya utekelezaji wa leseni yao
 
Ukigongwa na gari la CocaCola utataka kampuni ifungwe sababu haikupewa kibali cha kugonga watu?

Hayo makosa ya wafanyakazi sio maelekezo ya kampuni. Yeye alileta ugomvi wakamzidi bahati mbaya na sheria ichukue mkondo wake. Kampuni haiwezi fungwa kwa makosa binafsi ya wafanyakazi wake.
Hawa kukopesha na kudai ndio core business ya leseni yao ukitekeleza tofauti core business ya leseni yako inatakiwa regulator wa leseni yako akufutie leseni maana umeshindwa kufuata sheria ya utekelezaji wa leseni yako
Coca cola kututengenezea vinywaji vyenye ubora ndio core business ya leseni yao ,wakishindwa kututengenezea soda zenye usalama kiafya hapo itabidi leseni yao ifungwe, unakumbuka case ya madabida na arv feki ?
Sasa hawa oya wameshindwa kutekeleza regulations za leseni yao malalmiko makubwa kwenye recovery ya mikopo yao watu kupigana, kutoana kwenye mitandao hadi kuuana ,hapo its obviously kashindwa kufuata masharti ya leseni
 
Juma Said Mfaume, mkazi wa Mbagala Mlandizi, Pwani, amefariki dunia baada ya kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa Kampuni ya OYA Microcredit. Tukio hilo lilitokea alfajiri ya Jumanne, tarehe 8 Oktoba 2024, wakati wafanyakazi hao walipofika nyumbani kwake kudai marejesho ya mkopo wa Tsh 60,000 ambao mke wa Juma, Khadija, alikuwa ameshindwa kulipa kikamilifu.

Baada ya mabishano, wafanyakazi hao walitaka kuingia ndani ili kuchukua mali kama fidia ya mkopo. Juma alikataa, hali iliyosababisha ugomvi ambapo mmoja wa wafanyakazi hao alimshambulia Juma kwa kigongo shingoni. Baada ya kuanguka, walimbeba na kumpeleka hospitali, ambako alipoteza maisha.

Khadija, mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyochukua mkopa huo
Soma:

=> Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji
Huyu dada anajikanyaga na kujikana kabisa kwenye maelezo yake
 
Nina mashaka kama mume alikuwa anaujua huu mkopo,maana akipelekewa swali upande huo anashikwa na mtetemo mkali wa sauti,kuna uwezekano mawasiliano yake na mumewe kuhusu kukopa hayakuwa mazuri...
 
Back
Top Bottom