Mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyokopa

😁😁 labda alitaka akuongezee mkuu
 
Bro naona inatoa maelezo meeengi mengini hata yasiokuwa na mantiki kwenye hii kesi

Kwanza kabla hujaanza kuwatetea hao wadaiwa sugu na kuwaona wakopeshaji ni wahuni na waonevu umewahi kuona jinsi wanavyosumbuliwa na hao wakopaji kwenye marejesho??

Yaani mtu mkataba wake umeisha unakuta Bado anadaiwa marejesho zaidi ya matano na anafahamu kabisa mkataba ukiisha kama hajamaliza deni basi vitu alivyoweka dhamana ni Mali ya kampuni, lakini yeye anakuwa hayuko tayari kuzitoa vitu hivyo... Badala yake anaanza kuishi kwa kujificha, hata simu zenu hapokei.

Na mbaya zaidi Kila mkienda kwake mnaambiwa hayupo hata kama yumo ndani watoto wake au ndugu zake wanasema hayupo... Mnaweza mkatumia hata miezi miwili Kila mkienda mnamkosa na sio kwa sababu hayupo Bali anajificha.

Yaani mtu amekopa pesa kwa makubaliano maalumu kwamba akishindwa kulipa, basi Kuna collateral ya kufidia deni lake, lakini hataki kutoa hivyo vitu bali anaishi kwa kujificha akitegemea kwamba ipo siku mtakata tamaa ya kutafuta.

Siku maafisa mikopo wakichoka ndio wanafikia hatua hii.

Sasa ukiona mpaka wadai wamefikia hatua ya kutumia nguvu ujue Wana sababu ya kutumia nguvu na sio uanze kutoa lawama tu huku ukiwakingia kufua hao wadaiwa sugu wanaokiuka makubaliano ya kwenye mkataba.

Naona umekomaa tu regulators.. regulators sijui unataka wawe wanasamehe madeni kwa ajili ya kuwaogopa hao regulators... Watu wenye mawazo kama yako ndio huwa mnalea kasumba za kipuuzi za watanzania kwa sababu wanajua watatetewa.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Basi Sasa kama ni hivyo binadamu wote yatupaswa tujifunze kuheshimu makubaliano tunayowekeana hususani kwenye haya masula ya madai... Sio tunakubaliana vizuri leo halafu siku ya deni ikifika unaanza kuniletea maelezo marefu..
Hebu tuambie vizuri, na wewe ni mwana oya? Naona unajitahidi kweli kufanya wanukie

Huyu mubaba marehemu alikuwa mdeni wa oya?
 
Mkuu nina imani unajua utaratibu upo vipi ,hayo mambo ya kusumbuana ni kawaida ndio challenge ya kazi kama huwezi kuvimilia na una take it personal wakati wewe ni muajiriwa tu hapo kazi imekushinda ukatafute kazi nyingine
Police wapo, mahakama zipo huna haja ya kutumia nguvu kwenye dunia ya sasa, unaenda kuchukua court order tu na polisi watakusaidia kukupa ulinzi wa kuchukua hivyo vitu haina hata haja ya kubishana wala kusukumana
 
Mkuu nafikiri unawajua wabongo walivyo, majitu mengi hapa Yana comment kwa mihemko tu kwa kuangalia matokeo ya tukio zimaz na Wala hata hawajisumbui kuangalia kwanini wamefikia huko mpaka kwenye mauaji..

Watu hawajiulizi mbona hatuoni wateja wengine wakilalamika kuhusu kuonewa na Hawa jamaa, mbona Kuna wateja wengine wanakopa kwao miaka na miaka na hawajawahi kuonewa hivi?

Yaani watu wamejikita Zaidi kwenye matokeo badala ya kuangalia chanzo Cha tatizo?

Ona kama huyu eti anawashangaa kwanini jamaa huwa wanawafuata wadaiwa wao saa nane usiku na Wala hasumbuki kujiuliza kwanini hao wateja wafuatwe saa nane usiku?

Wabongo ni watu ambao huwa muda wote wanajihisi kuonewa tu hata kama sababu ziko wazi za kuonewa kwao.
 
Wana practice ya kutumia nguvu ,ndio imekuwa tabia yao kwenye kudai sasa namna hii tunayaweka maisha ya wananchi wetu kwenye hatari , wawe suspended wakati matukio au malalmiko haya yanachunguzwa maana watatuulia ndugu zetu
Kama kutumia nguvu pale inapobidi endapo kama mtuhumiwa ni mkaidi na mkorofi ni kosa kisheria, basi hata jeshi letu la polisi alistahili kuwepo yaani lifutwe...

Kaka sijui unaongea nini.. mtu mnapenda kumdai halafu kwa jeuri kabisa anawaambia hela yenu nitawalipa humu ndani sitoi kitu chochote, na hapo mkataba umeshaisha na hata muda wa ziada mliomuongezea umeshaisha,.. hapo mtaacha kutumia nguvu ilihali yeye mwenyewe emakaa kishari shari, hivi wewe jamaa kwanza umewahi kumkopesha mtu hata laki uke experience ule usumbufu wanaopitia maafisa mikopo?
 
Vipi taratibu za kisheria huwa zinazuia mdai kubeba vitu vilivyowekwa dhamana? Maana inawezekana mzozo umetokea kwenye kubeba hivyo vitu na marehemu akatetea mali zao mwishowe ikatokea murder.
generally hadi mahakama itoe kibali ,ila kuna baadhi ya mikataba inaruhusu kuchukua mali moja kwa moja
Kwa hiyo endapa kama huyo mtu(mdaiwa sugu) amegoma kutoa vitu alivyoweka dhamana maafisa mikopo wachukue hatua gani??
 
Polisi ndio kazi yao kulinda amani na kutulinda dhidi ya wahalifu ndio maana tunawapa bunduki na mabomu kwa ajili hiyo
Bank kazi yake kukopesha hela na kuna mikataba ambayo inatoa remedy mtu akishindwa kulipa, remedy zipo nyingi, ila hakuna sehemu yoyote bank inatakiwa kutumia nguvu ndio maana hata bank imewakana leo kwa kutoa tamko kwamba halijawatuma kutumia nguvu, kutumia nguvu ni jinai
 
Kwa hiyo endapa kama huyo mtu(mdaiwa sugu) amegoma kutoa vitu alivyoweka dhamana maafisa mikopo wachukue hatua gani??
Kuomba ulinzi kupitia polisi watakusaidia kutoa mbona polisi wanatoa hadi watu kwenye nyumba unakuwa na eviction order yako tu mengine unawaachia wao au dalali wa mahakama full stop, afisa wa bank na kutumia nguvu wapi na wapi
 
Kesi kama hizi ndio lisu anapaswa kuonesha uwanasheria wake.

Na sio zile za kulikomoa Taifa.

Hapo ikishaisa kesi ya jinai.

Huyo mama afungue kesi ya madai t
Dhidi ya hao wafanyakazi na kampuni ya Oya.

Awadai fidia kwa mamilioni kama si mabilioni.
Lisu umemshusha kwenye kesi za wanandoa? Hizo ni kesi za bush lawyers . Mtu kama lissu yupo above kwa sasa
 
Na kama huyo mwana ndoa mmoja aliyechukua mikopo alidanganya kuwa Hana mume, mme wake ameshafariki hapo kosa la nani? Na maafisa mikopo wachukue hatua gani? au ndio wahesabu maumivu?
 
Mkuu
Hata kama unafaidika lazima ukweli usemwe.
1. Hii mikopo ina riba kubwa hivyo ni chanzo cha umasikini kwa wakopaji na wizi kwa wakopeshaji na wanaonea wale wa hali ya chini.
2. Unapokopesha unatakiwa ufanye tathimini ya uwezo wa mtu kulipa na si tamaa ya kuchukua vilivyo vyake.

Huu uhuni ni lazima ukomeshwe. The sector is not well regulated.
 
Kuomba ulinzi kupitia polisi watakusaidia kutoa mbona polisi wanatoa hadi watu kwenye nyumba unakuwa na eviction order yako tu mengine unawaachia wao au dalali wa mahakama full stop, afisa wa bank na kutumia nguvu wapi na wapi
Kwamba Mimi nakudai 75,000/= halafu eti nikawachukue polisi ndio waje wasimamie zoezi la kuchukua vitu, polisi ambao nao kuwatoa kituoni pale itabidi niwape hata 50,000/= pia kumbuka hapo nimetumia usafiri ambao pia ni gharama..

Yaani nitumie gharama kurejesha pesa yangu kisa tu Kuna mpuuzi mmoja ameamua kujitoa ufahamu na kuniletea ubishi ilihali Kila kitu Kiko wazi kwenye mkataba??

Aisee sitakuwa na huo muda.. tutamalizana na wewe humo humo ndani, kama unaita mwizi ita, kama unashika panga shika tuuwane vizuri...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…