Mke wa Marehemu kaka aliachiwa nyumba na familia lakini mwanaume mwengine kahamia

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Mwanaume na mwanamke waliishi pamoja kwa takribani miaka mitatu kwa makubaliano ya “sogea tuishi” bila ndoa rasmi, na katika kipindi hicho wakapata mtoto.

Kwa bahati mbaya, mwanaume akafariki mwaka huu.

Familia ya marehemu ilikuwa inaweza kuichukua nyumba na kwa wakati ule mwanamke angekubali kuhama lakini familia haikutaka kuleta mambo mengi wala migogoro wakaamua kumuachia mwanamke nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu.

Sasa, familia imegundua jambo ambalo limeibua maswali mengi! 😳

Kuna mwanaume mwingine ambaye tayari anaishi kahamia hiyo nyumba, na taarifa zilizopo ni kwamba anajiandaa kumuoa huyo mwanamke!

Sasa swali linakuja hapa:

Je, familia ya marehemu ina haki ya kuhoji kuhusu huyo mwanaume mpya na matumizi ya hiyo nyumba, au walishafanya uamuzi sahihi kwa kumuachia mwanamke nyumba na hivyo hawapaswi kuingilia tena maisha yake?

Na je, kwa kuwa marehemu na mwanamke hawakuwa wamefunga ndoa rasmi, hali hii inapaswa kuangaliwa kwa namna gani?

Wewe ungekuwa kwenye nafasi ya familia ya marehemu, ungefanya nini? Tupe maoni yako! 👇🔥
 
Ndugu waache umbea, walipokubali kuichia na maisha mengine yakaendelea walitakiwa kubaki na msimamo huo huo.

Kuhusu kuishi hapo hayo ni maamuzi ya mwanamke kwa sababu ndiye mmiliki halali wa nyumba kwa sasaa...
 
Mkizidi kufatilia sana,
• mtoto siyo wa ndugu yako,

•mwanamke alihusika kwenye kifo cha ndugu yako ili aolewe na huyo mwanaume

• huyo jamaa ndiye baba mtoto,
Nae alikuwa kwenye mchongo wa kumuua ndugu yako.
 
Documents zinasoma nani ni mmiliki wa hiyo nyumba hadi Sasa!?
Nani alikabidhiwa jukumu la kusimamia mirathi ya marehemu !?
Kama inawezekana pambaneni ili nyumba itambulike kama Mali ya mtoto na awepo msimamizi wa hiyo nyumba hadi mtoto akue maana ikitokea mke akaolewa na jamaa na mke akafariki master anapata nyumba na nyie mnachukua mtoto wenu(paiiiin)
 
Haja zake za kimwili azitatue kupitia hiyo nyumba? La msingi nyumba iwe ni urithi wa damu yenu basi, hakikisheni hilo.
 
Documents zinasoma nani ni mmiliki wa hiyo nyumba hadi Sasa!?
Nani alikabidhiwa jukumu la kusimamia mirathi ya marehemu !?
Kama inawezekana pambaneni ili nyumba itambulike kama Mali ya mtoto na awepo msimamizi wa hiyo nyumba hadi mtoto akue maana ikitokea mke akaolewa na jamaa na mke akafariki master anapata nyumba na nyie mnachukua mtoto wenu(paiiiin)

Au anaweza (huyo mume), kufanya umafia wa kutapeli nyumba hiyo au kushinikiza iuzwe. Au kumuua huyu mama kimafia na akabaki na nyumba. Watoto wakabaki mikono mitupu.
Mario wengi hutajirika kwa kupitia wajane. 😊
 
Hadi Sasa suala la nyumba kuuzwa ili wajenge nyingine na mamtu ndio liko mezani kwamba mnajua au hamjui Hilo lazima linajadiliwa na mme atapewa kazi ya kutafuta mteja
 
Mario ndio wanapata mali kwa namna hiyo mjini. Hapo ikiuzwa 100M mario atamwambia 60M wafanye biashara. Biashara itakuwa ya Mario. 😊

Mjini shule.
Cha mlevi huliwa na mgema.
 
Mwanaume na mwanamke waliishi pamoja kwa takribani miaka mitatu kwa makubaliano ya “sogea tuishi” bila ndoa rasmi, na katika kipindi hicho wakapata mtoto.

Kwa bahati mbaya, mwanaume akafariki mwaka huu.

Familia ya marehemu ilikuwa inaweza kuichukua nyumba na kwa wakati ule mwanamke angekubali kuhama lakini familia haikutaka kuleta mambo mengi wala migogoro wakaamua kumuachia mwanamke nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu.

Sasa, familia imegundua jambo ambalo limeibua maswali mengi! 😳

Kuna mwanaume mwingine ambaye tayari anaishi kahamia hiyo nyumba, na taarifa zilizopo ni kwamba anajiandaa kumuoa huyo mwanamke!

Sasa swali linakuja hapa:

Je, familia ya marehemu ina haki ya kuhoji kuhusu huyo mwanaume mpya na matumizi ya hiyo nyumba, au walishafanya uamuzi sahihi kwa kumuachia mwanamke nyumba na hivyo hawapaswi kuingilia tena maisha yake?

Na je, kwa kuwa marehemu na mwanamke hawakuwa wamefunga ndoa rasmi, hali hii inapaswa kuangaliwa kwa namna gani?

Wewe ungekuwa kwenye nafasi ya familia ya marehemu, ungefanya nini? Tupe maoni yako! 👇🔥
Mimi nijuavyo, mtu akiishi na mke mume ndani ya nyumba moja kwa kipindi kisichopungua miaka miwili; huku wakitambulika na majirani pengine na hata serikali ya mtaa kuwa mnaishi pamoja hiyo tayari ni Ndoa kwa majibu wa sheria ya ndoa ya TZ.

Kwa maana hiyo, nyumba ambayo watu wameishi pamoja kwa hicho kipindi kisichopungua miaka miwili, hugeuka umiliki na kujulikana kuwa ni ya kwao (50/50) na pale mmoja anapotangulia mbele za haki, aliyebakia huwa na hisa ya 100% . Ninacho taka kusema, wenye haki kwenye hiyo miradhi ni Mke na mtoto....

Nijuavyo ni kama mama atapata mweza na kuamua kuolewa, nyumba hubaki chini ya umilikaji wa mtoto chini ya uangalizi wa mama wa mtoto; hadi mtoto atapokua..
 
Ndgu mkiwa na akili timamu lazima mjue kua huyo mwanamke lazima akazwe tu.

Shida ni ndgu kuoneana aibu kuibua hiyo hoja, kama vile hamkazani huko makwenu.
 
Back
Top Bottom