Wana mtoto mmojaKm hawakufunga ndoa rasmi, maana yake huyo sio Mke, vipi wana watoto? Mirathi inasemaje?
Subiri wajuzi wanakuja hapa.
Hivi ile mambo ya mkikaa miezi sita pamoja hiyo ni ndoa huwa sio rasmi?Km hawakufunga ndoa rasmi, maana yake huyo sio Mke, vipi wana watoto? Mirathi inasemaje?
Subiri wajuzi wanakuja hapa.
Hela zinatafutwa wapi?Kwahiyo walitaka asifanywe, si watafute zao..... hiyo nyumba ni yao?
Mimi ningekua kwenye familia ningeendelea kutafuta hela.
Documents zinasoma nani ni mmiliki wa hiyo nyumba hadi Sasa!?
Nani alikabidhiwa jukumu la kusimamia mirathi ya marehemu !?
Kama inawezekana pambaneni ili nyumba itambulike kama Mali ya mtoto na awepo msimamizi wa hiyo nyumba hadi mtoto akue maana ikitokea mke akaolewa na jamaa na mke akafariki master anapata nyumba na nyie mnachukua mtoto wenu(paiiiin)
Hadi Sasa suala la nyumba kuuzwa ili wajenge nyingine na mamtu ndio liko mezani kwamba mnajua au hamjui Hilo lazima linajadiliwa na mme atapewa kazi ya kutafuta mtejaAu anaweza (huyo mume), kufanya umafia wa kutapeli nyumba hiyo au kushinikiza iuzwe. Au kumuua huyu mama kimafia na akabaki na nyumba. Watoto wakabaki mikono mitupu.
Mario wengi hutajirika kwa kupitia wajane. 😊
Hadi Sasa suala la nyumba kuuzwa ili wajenge nyingine na mamtu ndio liko mezani kwamba mnajua au hamjui Hilo lazima linajadiliwa na mme atapewa kazi ya kutafuta mteja
Mimi nijuavyo, mtu akiishi na mke mume ndani ya nyumba moja kwa kipindi kisichopungua miaka miwili; huku wakitambulika na majirani pengine na hata serikali ya mtaa kuwa mnaishi pamoja hiyo tayari ni Ndoa kwa majibu wa sheria ya ndoa ya TZ.Mwanaume na mwanamke waliishi pamoja kwa takribani miaka mitatu kwa makubaliano ya “sogea tuishi” bila ndoa rasmi, na katika kipindi hicho wakapata mtoto.
Kwa bahati mbaya, mwanaume akafariki mwaka huu.
Familia ya marehemu ilikuwa inaweza kuichukua nyumba na kwa wakati ule mwanamke angekubali kuhama lakini familia haikutaka kuleta mambo mengi wala migogoro wakaamua kumuachia mwanamke nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu.
Sasa, familia imegundua jambo ambalo limeibua maswali mengi! 😳
Kuna mwanaume mwingine ambaye tayari anaishi kahamia hiyo nyumba, na taarifa zilizopo ni kwamba anajiandaa kumuoa huyo mwanamke!
Sasa swali linakuja hapa:
Je, familia ya marehemu ina haki ya kuhoji kuhusu huyo mwanaume mpya na matumizi ya hiyo nyumba, au walishafanya uamuzi sahihi kwa kumuachia mwanamke nyumba na hivyo hawapaswi kuingilia tena maisha yake?
Na je, kwa kuwa marehemu na mwanamke hawakuwa wamefunga ndoa rasmi, hali hii inapaswa kuangaliwa kwa namna gani?
Wewe ungekuwa kwenye nafasi ya familia ya marehemu, ungefanya nini? Tupe maoni yako! 👇🔥