Ni walewale waliofanya shambulio la atomiki huko Japan na kusababisha madhara makubwa.
Ni walewale Walioichafua Libya, wakasababisha raia wa taifa hilo kuwa masikini.
Ndio haohao walioitembelea familia ya ndugu yetu Azory Gwanda ambaye hajulikani alipo. Mungu amsaidie arudi salama Inshaallah.
Kitendo cha balozi huyo kufanya ziara kwa familia ya ndugu yetu mpendwa kimetusikitisha sana.
Bila shaka, balozi huyo anatumia machungu ya ndugu yetu kisiasa. Tunajiuliza huruma hiyo ametoa wapi?
Ingelikua ana ubinaadamu angeishauri serikali yake iache kufanya mauaji ya watoto wadogo huko Yemen.
Angeishauri Marekani iache kutengeneza makundi ya kigaidi, maradhi ya ebola na udumavu. Kwakweli angekua na huruma, angejiuzulu.
Tunamshauri balozi huyo akatembelee ndugu wa waandishi wa Marekani ambao waume zao wamepotezwa na Trump.
Waache kumtumia ndugu yetu kama silaha ya kutupiga nayo wenyewe. Mataifa mengi walianza hivihivi wakaishia kufanya uvamizi wa kijeshi.