Ndugu yangu, uaihangaike kuumiza kichwa.....
Hili janga halijakukuta pekee yako ni wanaume wengi wanapitia hii hali.
Nitakupa sababu zinazoweza kuwa chanzo cha hiyo hali.....
1. Ulimbukeni wa mabadiliko ya maisha: kuna aina ya watu ambao huwa katika akili zao hawakuwa kutarajia kufika hatua fulani ya kimafanikio.
Sasa kwa bahati mbaya hii sampuli ikatokea akapata hayo mafanikio ambayo hakuyatarajia mfano, kupandishwa cheo, kupata kazi ya ndoto zake, kuongezwa mshahara, au kutusua dili ya pesa nyingi hapo ndipo akili yake hupoteza nguvu yake ya busara na hekima na hujikuta anaropoka na kufanya mambo ambayo si mwenendo wake wa kawaida. Watu wa namna hii huwa hawadumu katika kile kinachowapa kiburi katika maisha maana huwa wanaongozwa na sifa na jeuri hivyo we mpe muda tu atakutana na adabu ya MUNGU na atarudi kwako ameufyata. Haya ni matokeo ya kuwa na damu na akili ya kimasikini.
2. Mwanamke wako anaweza kuwa ana act hivyo kutokana na influence ya marafiki, ndugu au mzazi wake mojawapo sana sana mama. Hawa watu huwa wanakawaida ya kutobalance story kwa maana ya kwamba inapotokea ninyi wawili mkatofautiana wao hawatafanya jitihada ya kusuluhisha kwa kuwasikiliza nyote kila mtu upande wa story maana muwamba ngoma huvutia upande wake. Matokeo yake hapo ni kutoa ushauri ambao unalenga zaidi kukomoa na sio kusolve tatizo kwa wenza. Usikute ameshauriwa kuwa wewe mjibu unavyotaka asikupangie namna ya kuishi.
3. Huyo mwanamke anaweza kuwa kaanzisha mahusiano kwa usiri baada ya kuona kuna baadhi ya vitu hapati hapo kwako. Wanawake wa siku hizi wana akili mbovu sana nyakati za changamoto. Anaweza aone kuna changamoto fulani, lets say ya kipato katika familia badala ya kusimama na mume wake kumpa moyo na sapoti yeye anawaza kutoka kivyake ili maisha yaende. Sasa unaweza kuta kunashida ameinusa kaona isiwe nongwa, atafute mtu wa pembeni ambaye mwisho wa siku anaishia kumfanya awe na dharau hivyo.
4. Tabia mbaya ya mwanamke wako inaweza kuwa sababu. Kuna aina ya wanawake huwa anaweza kupretend kwa muda mrefu na inafika kipindi anakuwa hawezi jificha tena ufake wake ana amua kufunguka. Huyu mwanamke wako anaonyesha alikuwa na kiburi tokea muda sana ila tu alikificha na sasa ndio muda anaamua kionyesha maana anahisi hana cha kupoteza.
5. Pengine sababu ya ukorofi wa huyu mwanamke ni matokeo ya uvumilivu wa muda mrefu wa mwenendo wako, yaani kama ulikuwa unamfanyia matukio ya usaliti na ameshakufumania mara kadhaa.....sasa amefikia muda ameona kama vipi vipi. Katika hili ukweli unao wewe mkuu sio mimi.