Mke wa ndoa anaposema maneno haya anamanisha nini ?

Mke wa ndoa anaposema maneno haya anamanisha nini ?

Hapa yuko sahihi kabisa. Mm mume wangu huwa akichukua hata mia yangu ujue huo ni mkopo, atarudisha tu.

Hapa jiandaye, soon atakuwekea sumu kwenye msosi. Kilicho moyoni mwake ni wewe kurest in peace.
Duh! Inamaana hata kutunza watoto pia ni hela za mwanaume wewe zako hazihusu? Hv familia ni mume au ushirikiano wa mume na mke?
 
Shida ni kwamba wanataka watoe hela pasu pasu na mkewe afu bado anyenyekewe (mikazii yoote)
Wanashindwa kuelewa mwanamke Hamna Kitu kinachomuuma Kama hela afu ukute huyo kaka hahudumii mahitaji ya bidada ajinunulie mwenyew ,hapo lazima ataona mume mbinafsi

Aisee wakitaka warambwe mpaka unyayo,kupendwa mpaka ncha y'all unywele wahudumie familia yao bila kupiga jicho hela ya mwanamke..... Huyo dada atakupenda mpaka uhisi anaigiza


Kwa wanaosema kaanza jeuri sababu ya kuchepuka sio Kweli .... Mara nyingi mdada akiolewa kuchepuka Labda anatafuta amani ya moyo, attention, care.!!! Na si vinginevyo
I am a woman!
Ila ninachoshangaa wanawake siku hz mmekuwaje? Yaani unafanya kazi na mmeo anafanya kazi mna watoto (familia) lkn mke hutaki kutoa hela yako kusaidia familia. Mume ndo afanye kila kitu, kodi ya nyumba, chakula, ada za watoto, umeme maji vyote afanye mwanaume, wewe mwanamke hela yako kazi yake nini? Chakushangaza zaidi utataka nguo ununuliwe, viatu, chupi, nywele usiponunuliwa unadai hakuudumii, jamani hii ni haki? Wewe zako unapeleka wapi?

Wanawake acheni ubinafsi, huo ni ubinafs wa hali ya juu. Familia ni ya wote baba na mama. Kutunza watoto ni jukumu la wote baba na mama labda tu mama uwe huna kazi wala kitu choxhote cha kukuingizia kipato hapo sawa mwanaume ana haki ya kufanya yote.

Maisha ni kusaidiana sio kukomoana jmn
 
Mkuu mpandishe cheo umfanye mke mkubwa maana naona hajuwi simba huyo anamchezea sharubu sijuwi anafikiri eti ww ni paka....
Ukiona upande wa kichwa umebuma jaribu ipande wa swala
 
Sijui nisemaje lakini kukunyima mshahara wake ni haki yake ....pesa za mwanamke ni za kwake yeye mwenyew ..kama ataamua kukusaidia majukumu sawa vinginevyo hutakiwi kuzipangia matumizi zile ni zake....kakwambia kweli kasomeshwa na wazazi wake ili awafae baadae hakusomeshwa sababu nyingine ....kingineee kupeleka maji bafuni sio kazi yake labda aamue kukupelekea kwa mapenzi yake tu .....kufua pia labda aamue kukufulia kwa mapenzi tu vinginevyo tafuta dobi ...samahani kama utakwazika lakini habari ndiyo hiyo

Somesha wanao usimtegemee yeye wewe ndie kichwa na kiongozi wa familia
Aisee! Alafu wewe unategemea kupata mwanaume uwe mke kwa akili hz? Utapata tabu sana dada
 
Ni ujinga kufikiri wewe mwanamke umesomeshwa ili ukahudumie wazazi wako! Je mwanaume siyo binadamu? Kama wewe umesomeshwa na wazazi wako uwahudumie na mwanaume amesomeshwa na wazazi wake ahudumie wazazi wake! Kwa mantiki hiyo nani atahudumia familia yao? Michepuko?

Nikueleze mzazi lazima asomeshe watoto alowazaa kwa raha zake ( mwanamke wazazi wake na mwanaume wake pia). Hivyo wewe na mwanaume wako ni jukumu lenu kuhudumia watoto wenu ambao kwa raha zenu mmewaleta duniani! Jukumu lenu si kuhudumia wazazi ila watoto wenu! Ni mwanamke mpuuzi kama zenc anayeona kazi yake kuhudumia wazazi baadala ya watoto wake aliochekecha kiuno kuwazaa


😂😂😂kiufupi mie nasomesha m1..ingawa hatujataka wajue😊.kila mtu nawake.😊
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].. nyie km vitoto vya form 6[emoji87][emoji85]... mie sipendi kelele... in anymeans mie aipend kbs makelele ila.siku nikiamuaga kusema anawekaga mkono.km.mic hvz narap weee namaliza..ila kubwabwaja siwez..ila huwa nataman mie ningekuwa na nguvu za kupigana..kila week ningekuwa namfumua sana sana
Acha ubabe[emoji23][emoji23]
 
Punguzeni kujilinganisha na wanawake
Mtaishi kwa Amani

Unakuta mwanamke anaongea mwanaume nae anachambana na mkewe

Kila pesa ya mwanamke unaitamani na kuipangia matumizi halafu unajiita mume
Hapo naona ni ndoa ya wake wawili
Umenikumbusha binti mmoja alikuwa ananisimulia anavyosumbuliwa na kaka yake aliyemaliza chuo hana hela awe anamtumia. Jamaa anadai sister yake atakuwa na hela tu maana anahongwa!

Yaani unajiuliza mtu mzima, graduate, anatamani hela za kuhongwa za mdogo wake wa kike!!! Sijui jamaa naye anatamani ahongwe!!!
 
Unadhani msemo wa ukioa mchagga lazima ujenge kwao ulitoka wapi?
Sijui maana mm mume wangu hajajenga kwetu sisi tunajenga kwa ajili yetu na wanetu kwetu wanajenga kaka zangu sasa sijui kama eti mashemeji ndo wanajenga nyumban tena
 
Umenikumbusha binti mmoja alikuwa ananisimulia anavyosumbuliwa na kaka yake aliyemaliza chuo hana hela awe anamtumia. Jamaa anadai sister yake atakuwa na hela tu maana anahongwa!

Yaani unajiuliza mtu mzima, graduate, anatamani hela za kuhongwa za mdogo wake wa kike!!! Sijui jamaa naye anatamani ahongwe!!!
Yaan huu n upuuzi wa kiwango cha hali ya juu..eti unategemea Dada yako akupe hela maana anahongwa! Mwanaume wa hivi mwisho ataolewa kabisa mfyuuuuu
 
Back
Top Bottom