Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Kila wakati huwa nasema hawa wasanii wawe wanaangalia na kujifunza kutoka kwa wenzao,hawa wasanii nyota ni kama hawajui kuna kesho, hawa wasanii wakiwa kwenye good time hawajui kesho na hawajuia kama kuna watu wana shida na kuwa kuna siku nao watakuwa hawana kitu.

Mimi nikiugua au ndugu yangu akiuugua siji mitandaoni kuomba msaada,ni mzigo wangu. Ukienda pale Muhimbili kuna mwembe unaitwa Mwembe mawazo huwa wanakaa watu mbalimbali kila mtu anahangaika na mgonjwa wake,utasikia huyu anapiga simu uza shamba,au muambie baba mdogo achangie , na wala hutawasikia kusema tuweke namba zetu mtandaoni tuwaombe watu.

Pamoja na umasikini wao, mzigo wangu ni wa kwangu, kila mtu abebe furushi lake! hawa wasanii hakuna wanaowasaidia wakiwa kilingeni wao ni starehe na watu wao.
Ukweli unauma. Umesema kweli kabisa kabisa. Tutamwombea sawa. Ila kama usemavyo hii issue ya kwao na walitakiwa watumie mali zao watu wao ndugu zao.
Pale mwembe mawazo ukisikia jinsi raia wanavyohangaika ndugu zao wapone waweza toa machozi kabisa.
Wasanii kumbukeni bima za afya. Wakumbuke kuwekeza. Wakumbuke nasi tuna majukumu yetu. Wakumbuke pia wasije kwa raia wakati wa shida huku tukiwa vituoni wao wakipita na magari ya kifahari yenye ac na kutuona kinyesi…
 
Aisee nimelia. Mwembetogwa? Ngoja niende nikajionee kama ni kweli usemayo.
 
Ruge aliwekeza nini na nini outside cmg?
Alikuwa shareholder mkubwa CMG, alikuwa anamiliki Prime Time Promotion, Alikuwa mmiliki wa Escape One and Two, mmiliki wa THT alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Tatumzuka. Alikuwa mratibu wa matamasha makubwa karibu yote nchini kupitia Primetime Promotion. Alikuwa na miradi endelevu akipitia CMG kama Summer Jam nk

Kwa taarifa yako kampuni ya Prime Time Promotion wana vifaa vya sound kubwa ya kuburudisha watu zaidi ya elfu kumi kwa wakati mmoja ambavyo zipo seti tatu. Ndio zilizokuwa zinakodishwa kampeni za CCM za Urais na kwenye matamasha makubwa
 
Mwenyezimungu amfanyie WEPESI apone na kujumuikana nasi.Maradhi ni mtihani kwa binadamu na hivyo familia iendelee kuwa na subra na kumfariji mgonjwa . Mimi nipo mbali yangu DUA KWAKE .🤲🤲
 
Daa we jamaa Jose amewahi kukudharau vipi? Acha roho mbaya.
Uwezi jua, wasanii wakubwa ukitaka kuwajua ukiwa underground unataka msaada utoke, ndo utajua kachumbali mboga au Nini, afadhali wasanii wa kizaz kipya wanamoyo sio manguri wa zamani.
 
Back
Top Bottom