Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Ww ndo umenena mkuu, achana na yanayobwabwaja et oooh bima haicavi figo, kumbe hayajui kitu.

Ona sasa kumbe NHIF wana bima kubwa ya almost 1.9M inayohudumia magonjwa kama hayo na hatujui. Na yy kumbuka alikuwa mbunge, so atakuwa anafahamu. Ila sema ss binadamu tunajisahau sana.

Yakitukuta ndo hivyo tena, kulaumiana
Niliuguza mgomjwa wa figo 2018-2021 mkuu, nilijua mengi kuhusu huu ugonjwa. Nilitembea sana Muhimbili na Mloganzila hivyo najua kiasi chake.
 
Wasanii wakubwa wengi wakiwa kwenye pick maringo na nyodo, wakiumwa au kufulia wanakuwa wema na kutaka huruma za mungu.
 
Duh kwa kweli Mungu mwenyewe tu amsimamie na amponye tuchange kwa tulichojaaliwa hakuna aijuaye kesho maana hata jana alikuwa mzima kama sie.
 
Kitu usichokijua ni bora ukae kimya mkuu,hivi yeye anapotoa msaada kwa wengine wewe utawezaje kujua au ulitaka awe anatangaza kila anaposaidia!,tenda wema nenda zako.

Tetesi ni kuwa ana shida ya figo,hiyo kitu inaitwa dialysis isikie tu kwenye bomba wala usiombe ukapata mgonjwa kwenye familia akahitajika kufanyiwa hiyo kitu,kama tajiri Luge ilifikia mahali kuombewa michango,Prof J ni nani,weka akiba ya maneno mkuu,kesho yako huijui...
Naona unatoa mipovu kama fisi, hata nikiwa ni mimi au ndugu yangu sitaomba msaada wa kutembeza bakuli, hayo sijui ya figo au nini sio yeye wa kwanza kuugua ,urafiki wako peleka huko kwani wangapi wana tatizo la figo na umewachangia?
 
Acha roho mbaya mkuu binafsi jamaa alipiga hela ila majanga yalikuwa mengi! Imagine uvunjiwe nyumba ghafla unafikiri kujenga same house ni bei gani?

Naskia pia mbowe alikusanya hela toka kwao ku fund kampeni za lissu mwaka 2020. Sasa hebu imagine una 150M na unevunjiwa nyumba. Ujenge nyumba mpya labda 60M hivi na makorokocho ya ndani 75M kuna hela tena humo?

Hapo bado kuna mke na mtoto wa kum support haya kingine akakosa ubunge term iliofata. Nilipoona mkewe kaanza tu kuwa MC nilihisi tayari kuna tatizo kwenye ile familia.

Kwa stage ya maisha aliyofikia hakuwa mtu wa kuunga show au kutafta kazi ya utangazaji. Let the nigga fight for his life jamani tum support sababu mitihani ni sehemu ya maisha hakuna mtihani mgumu kama kuumwa. Mungu amjalie afya aweze kuendelea ku support familia yake tuache kiburi cha uzima na mabezo.

Ipo siku na sisi tutapitia kuumwa tu wala sio swala la kumbeza mtu na kumkejeli. We would all need help in some way.

Hata uwe na million 100 jiulize dialysis kila week ni laki 3 unafikiri ni hela kiasi gani utatumia ukilala kwa week 20 tu? Bado gharama za kitanda kwa VIP daily kulala unaweza pigwa laki au zaidi. Matibabu sio rahisi tuache kiburi cha uzima jamani!

Bima tulizonazo nyingi ni za janja janja inakutibia magojwa ya malaria tu na UTI magonjwa mazito inakuacha upambane na hali yako nyie acheni tu!
Wangapi wanaugua figo na wanatembeza bakuli kwenye vyombo vya habari,wangapi wana wagonjwa mahututi wanatembeza bakuli,kuwa superstar hakufanyi wewe upendelewe zaidi ya wengine, nenda Muhimbili ndio utaona kila mtu anabeba msalaba wake kimya kimya, tunapokuwa na pesa tujue pia kuna kesho,nilichoandika sio roho mbaya bali ni kutuasa sisi sote, nadhani sote tunamkumbuka mzee Majuto pamoja na mikataba yote na hela nae ikawa hivi hivi, najiuliza ni kwanini bakuli liwe kwa watu maarufu tu tena wenye pesa na isiwe bakuli kwa malofa wenzetu ambao wapo hoi bin taabani mahosipitalini? mbona hatujifunzi?
 
"Wakati tunaanza kuuguza hatukutarajia kama itakuwa serious, tulijua ni kitu cha muda mfupi."

Nimewaelewa sana hapa.

Inauma. Ila msife moyo.

Wakati ni mgumu lakini mtashinda.

Na hamtaamini mmeshindaje.

Mungu ni wa ajabu sana.
Mimi nauguza baba yangu, wakati anaanza kuumwa tulijua tu ni kwa muda tu atakaa sawa, wanachokisema nawaelewa sana, hali hii isikie tu kwa wengine, get well soon Prof.. Mungu akufanyie wepesi upone haraka
 
Jamaa Tutamchangia Na Kumuombea Ila Ukweli Mchungu. Kuchomoka Ni Ngumu sanaa. Tunakupenda Legend. Hata Ruge Ilianza Hivi. Muhimbili wakikulaza Zaidi ya Wiki ni Ngumu kutoka.

Figo unavyozidi kukaa hospital ndio zinazidi kuwa Mbaya
 
Naona unatoa mipovu kama fisi, hata nikiwa ni mimi au ndugu yangu sitaomba msaada wa kutembeza bakuli, hayo sijui ya figo au nini sio yeye wa kwanza kuugua ,urafiki wako peleka huko kwani wangapi wana tatizo la figo na umewachangia?
Mwenzio ni public figure,sasa wewe utembeze bakuli nani anakujua ? punguza wivu mkuu...
 
Tema mate chini ndugu yangu. Bado hujayajua maisha haswa haya ya kibongo. Ruge na uwekezaji wote aliokuwa nao lakini tulimchangia hapa jukwaani.
Kuuguza ni mtihani sana na watanzania wengi hatuna akiba za kihivyo. Tunapata hela tunajenga, tunasomesha, tunasaidia ndugu huku tunaendelea kutafuta. Ukiugua say baba ambaye ndio mtafutaji mkuu inakuwa shida sana na mambo yote yanaharibika

Tumchangie Jay kwa chochote tulichonacho hata kama 2000 itasaidia maana watu 5000 wakitoa hiyo inakuwa 10,000,000
Ruge aliwekeza nini na nini outside cmg?
 
Mkuu Unajua maana ya Privacy ? Kutaka mambo ya ndani kukaa ndani sio utamaduni wa kizungu hata huku tunao;

Faragha ni muhimu hata ukitoa pesa sio kwamba ndio una Haki ya kujua au kupewa daily feedback (utapata information panapobidi)
Ukisema unataka faragha maana yake uachwe kivyako, hutaki kufuatiliwa una hali gani, umeambukizwa na nani, uko wapi, unatibiwa na nani, unaletewa chakula na nani.

Lakini sisi Waafrika hatuko hivyo wakati wa shida!

Huyo mkewe au mwana familia aliyetoa tamko kwa umma alituletea mikogo ya kizungu, sasa mikogo imemtokea puani. Ajifunze na abadilike, kuiga kila cha mzungu utapasuka msamba.

Unataka privacy halafu unataka tushikamane na wewe, tushike lipi ?
 
Back
Top Bottom