Mke wangu akiwa nami 'full kununa' ila tukiwa na rafiki zangu anatabasamu na kucheka sana

Hawa viumbe hawapendani wenyewe kwa wenyewe. Pia wanakuwa na urafiki feki
 
Alikutaka wewe uwe mume kwa sababu zake na zimeexpire, haoni nuru tena ya uvunaji tena au amekinai kwa sababu si rafiki yako wa kweli na wa kudumu maisha yenu, unless iwe ni seasonal mnapokuwa na ugomvi ndani otherwise huyo kashaona alibugi hana cha kupoteza
 
Good inahitaji kujua hutokea hali na nyakati zote au ni muhimu
 
Hataki kuonyesha wageni ananunaga.... so shukuru tuu Mungu hata kwa hilo.
 
Kuna shida mahala, mkabili atakwambia kila kitu
 
Hakika kabisa, hapa umenena maneno ya hekima na busara.
 
Mke mzuri sana huyu, yaani anajuwa namna ya kuji-tune ili akuridhishe wewe na ujinga wako. Hivi ungejisikiaje wanakuja marafiki zako halafu mkeo anawachunia? Nakuambia nenda kwa mkeo sasa hivi ukamuombe msamaha haraka sana la sivyo nakuja kumchukua awe wangu.
 
Wife anaficha siri ya ndani.
 
Ni hivi kawaida mkiwa mmepishana maneno hata kugombana mkiwa wenyewe hamuwezi kuonyesha mbele ya wageni au watu wa nje inabidi muwe kawaida ila wakiondoka mjadala unaendelea ni kwa manufaa ya mahusiano yenu ili mjadala huohuo usijirudie tena mbeleni.Usitegemee uvuruge halafu ipite kirahisi tu au isahaulike bila kusuluhishwa.

Kitu kingine inawezekana humchekeshi,hutaniani nae upo serious sana...(you are not fun to be around).Au hamna maongezi ambayo yanampa amusement yaani your boring.
Jaribu kuloosen up na kuwa huru na mkeo,mtekenye,mtanie,flirt with her ndio raha ya huba.

Hali hii imeanza lini?Au ipo siku zote kwenye mahusiano yenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…