Mke wangu alibakwa na baba yake mdogo aliyekuwa anamlea akiwa na miaka 13, leo ukweni akataka arudie tena!

Mke wangu alibakwa na baba yake mdogo aliyekuwa anamlea akiwa na miaka 13, leo ukweni akataka arudie tena!

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
Mke wangu alifiwa na wazazi wake wote wawili kwa ukimwi mkali ule wa zamani, hivyo akalelewa na baba yake mdogo tangu akiwa na miaka 8, darasa la pili.

Wife alipofika darasa la saba alibakwa na baba yake mdogo huyo aliyekuwa anamlea na kumtishia kuwa akisema atamuua.

Uzuri wife akawa amefaulu na kuchaguliwa shule ya bweni. Mkoa aliochaguliwa kulikuwa na shangazi yake ambaye ni aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi, hivyo likizo zote zilimalizokia kwa shangazi hadi anamaliza kidato cha nne.

Kipindi cha kusubiri majibu shangazi akawa anamsisitiza kwamba aende kusalimia kwa baba mdogo, ndipo wife akamweleza yote aliyofanyiwa na baba mdogo. Shañazi akaelewa.

Majibu yakatoka wife akachaguliwa kujiunga na shule ya bweni mkoa mwingine ambapo hakuwa na ndugu. Alisoma kwenye mazingira magumu sana.

Kwa kufupisha habari, huyu baba mdogo amefiwa na mkewe na tumezika leo. Jinsi huyo baba mdogo alivyo mchawi, akawa amemwita wife chumbani kwake mida ya saa nne. Wife alipoenda akawa anamlazimisha amlale, kwenye purukushani wife akapiga kelele.

Kwa kweli baba mdogo katia aibu sana.

Kesho tunarudi zetu Dar
 
Back
Top Bottom