Mke wangu anadai niifukuze familia ya kaka nyumbani

Mke wangu anadai niifukuze familia ya kaka nyumbani

Shemeji mtu anakaa sebuleni na night dress? Unamtoaga out (peke yenu) kunywa bia? Mkeo ana haki ya kulalamila na usipoangalia utampindua bro wako.

Tafuta hela huyo shemeji akapange kwingine kama una nia ya dhati kabisa kunusuru ndoa yako.
 
Uctuzingue hapa eleza kila kitu kama ilivyo la sivyo natoboa yote maana nakufahamu vizuri 1.nani aliyemwambia housigel asiwe anafungua mlango 2.mara ngapi mkeo kakukuta kwa shemejio ukatoa kisingizio kuwa ulienda kumuangalia mtoto anakoroma vibaya 3.......4.......5.....6....7.....8....9....10

Sent using Jamii Forums mobile app

Bila shaka wewe ndiye mkewe wa @navin-govind kwa kuwa mmekuja kulianika wanajamvi tuwashauri si vibaya tukachangia mawazo yetu:

1. Mume na shemeji yako mnapotea kama hamjapotea tayari.
2. Mtu mzima halelewi, ana kila kiungo, akili anayo, muda anao kwa nini alelewe?
3. Hiyo pesa mnayotumia kumlea muongezeeni kma ipo nyingine mpeni mtaji aanze kujishughulisha ailishe familia yake mwenyewe.
4. Gharama za shule za watoto, wasaidieni hadi mwisho.
5. Msisite kumsaidia kila atakapokwama huyo shemeji mtu na familia yake.
6. Mawifi mmalize uhasama, kaeni muongee myamalize.
7. Mawasiliano yote ya maendeleo ya familia yafanyike baina ya mawifi.


OVA. Jamaa unamla shemeji yako sisi sio watoto wadogo, na lazima hiyo dhambi ikutafune bwege wewe.




Mtanikuta zimbabwe.
 
Huyo dada anachofanya ni kama kumshukuru shemeji yake kwa mema anayomfanyia yeye na watoto wake!!! Ebu tuache kuwa na negative perceptions.....unafikiri kuishi nyumba ya watu ni kitu rahisi eeenh????
Swadaqta mkuu sijui nisemeje
Hii coment umeitoa
Kiusahihi sasa tena kwa fikra
Pana sanaaa hakuna jambo gumu kama kuka kwa mtu asee
Tena anailea familia yako asee sema watu fikra hasi ndo znmejaa
Hongera dada
 
Huyo dada anachofanya ni kama kumshukuru shemeji yake kwa mema anayomfanyia yeye na watoto wake!!! Ebu tuache kuwa na negative perceptions.....unafikiri kuishi nyumba ya watu ni kitu rahisi eeenh????
Jamaa kasema hata zaman mke wake alikuwa hampi hizo huduma
Zaidi ya dada wa kazi tu
Sasa watu sijui hawaoni huo msitari!
Watu wamekazana tu anaingilia majukum sio yake akat jamaa
Amekiri dada wa kaz ndo alikuwa
Akilfanyia hayo
Ya kumfungulia geti
 
Mkeo ana matatizo ila na wewe nae unamtoaje out shemeji unamwacha mke?
Kuna watu coment zenu short
Ila za kifikra sanaa
Huwa nakuelewa dada lake
Hapo kote kuna shida.
 
Kuna tatizo sehemu,tena kubwa,tatizo ambalo ww unazidi kulikuza na mkeo anazidi kukusaidia kulikuza..

tuanze na wewe,kwa nini wewe mke wa nduguyo anavaa nguo ya kulalia na anakaa sebuleni mbele yako bila ku hukua hatua ya kuzuia hali hyo?
Kwanini anakuandalia chakula na hulalamiki kila siku na umeridhika?kwa nn unaenda kuka nae bar bila mkeo?

Tuje kwa mkeo,je kwa nn amekasirika wkati hafanyi jukumu lake kwako?kwa nn mnafundishwa na hyo mgeni lakin wote ww na mkeo mmeshindwa kujifunza?unashindwaje kufundishana ndani chumban hali halisi ilivyo na mkeo ajifunze?kwa nn kila siku aridhike ww mumewe uandaliwe chakula na mke wa nduguyo na yy yupo ndani?kuchelewa kwako kurudi nyumbani hakuhalalishi kutokulala kwao mapema,je mkeo hana namba yako ya simu umpigie au akupigie mfungulie geti?upo serious kwel na ndoa yako bro?

Shemeji je anaona nafany heshima lakin ameshindwa kugundua hapo sio kwake na yte anayokusaidia hayastahili kwa sasa?ameshindwa kujua ww ni mume wa mtu na yupo kwa watu?anashindwaje kumwelewesha mkeo cha kufanya kam mkeo kajisahu?
Au bro unataka kumega kisela sema tu unashindwa kuanika hapa jukwaani?au ushamega?

Kuna tofauti kubwa kati ya mjinga n mpumbavu,mjinga anajua ila anajua vibaya,ila mpumbavu hajui kabsa na hajui kua hajui.. Utachagua kupi kunakufaa hapo...na kipi bora kwa faida yako na familia yko. Ita wote usimame kiume tabia hii huipendi na isirudiwe. Mkeo kamkanye chumbani kwamba afanye kam shemeji yako anavyofanya. Tchao
Swadaqta
 
Jaribuni kukaa watatu, wewe mkeo na shemeji, mkubaliane mkeo afanye majukumu yake, shemeji kama anasaidia kazi kuwe na mpaka, mambo yote yanayokuhusu wewe mkeo ndio anapaswa Fanya. Ikifika kwenye majukumu ya watoto hapo sasa shemeji ndio aweke juhudi, lakini chakula chako, nguo zako na takataka zote zinazohusu wewe mwanaume... Wanawake wengi wanasahau majukumu yaho has a Hawa wake zetu, wakipata majaribu kama hayo wanaishia kusema " kuna kitu kuna kitu" kwa mazingira hayo wewe endelea kumsahidia shemeji, dunia inazunguka hii uwezi jua nani atakuwa msahada kwako badae...

Sent using Jamii Forums mobile app
Swadaqta
 
mwambie shemeji mwisho saa mbili awe ameshalala.asikufungulie geti.na mkeo mwambie hapo shemeji haondoki kama vipi aondoke aone nani atachekwa na dunia .fala sana asikutafutie dhambi bure.familia ya ndugu yako iteseke kisa mtu mmoja akwende huko
Sawa
 
Yani uko mbioni kumla shemeji. Kwasababu kwanza yeye atakua anakutaka, maana huenda kabla ya mme wake kufungwa alikua hamfanyi haya yote kwa mmewe
Pili kuna uzaifu fulani umeonyesha mbele yake kuhusu mkeo sasa anataka achukue hiyo advantage umtafune.
Hawa wote ambao wanasema huyu dada anaroho mbaya aithani alishaona mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mleta mada anashangaza sana ati hataki familia ya kaka ake isambaratike wakati ya kwake iko kwa hati hati ya kusambaratika. Huyo Shemeji ni sawa na kukaribisha pepo na inawezekana ana pepo LA jela angalia usije ishia jela na wewe. Usimlaumu mkeo ati ana roho mbaya, mkeo hana roho mbaya na yeye anatetea familia yake. Mtafutieni cha kufanya huyo Shemeji kama hawezi akakae na wazazi wako akafanye hizo heshima huko wewe baki na watoto
 
Nguo za kulalia anavaa anakaa sebulen ili iweje..nawe unasifia tu nakuona mwanzo mwsho...
Unamtoaje outing[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32]
Kwakifupi ushageuza kibao...we na shemejio mnatafuta mchawi...
Yn mume wangu arudi ukimbilie kumsave food chaaaah...
Hahaha hahaha utamfanyaje
Na ndo kashamtengea[emoji23]
 
Bro I'm not in your situation na sijui ningefanyaje ila from an observers point of view angalia nafsini mwako nia Ilikuwa ni ipi kumleta hapo na je bado ipo, think about your brother and if it were reverse ungependa iweje, kumbuka your brother is your brother for life. Wewe mwenye unajijua kama your intentions are still pure, usijaribu Kabisa kushawishika na mwanamke wa kaka yako. Kwa upande wa shemeji yako kukufungulia na kupakua msosi ni jukumu la mke kama halifanyi asilalamike badala ya kujishtukia na kuanza kufanya yeye analalamika. In short be the man of the house remember it all rests on you, usijibizane mkeo sema tamko au better kaa Kimya na sema this sentence ' I cannot abandon my brother's family. ' full stop

Sent from My BlackBerry Passport
Swadakta
 
Wote watatu mna makosa:-
1.kosa la mkeo ni kushindwa kutambua na kutimiza majukumu yake kama mama mwenye nyumba maana inaonekana hata kabla ya shemeji kuhamia hapo, house girl ndio alikuwa akitimiza majukumu mengi ya mkeo.

2.kuruhusu urafiki wa karibu mno kati yako na shemeji hata kupelekea kutoka out ukimwacha mkeo nyumbani, hii si sawa na ndiomana imepelekea shemeji yako kutozingatia umuhimu wa yeye kuwa na mipaka kwako na kumtii mkeo maana anachukulia masihara.

3.Japo kukufungulia mlango usiku, kuandaa chakula na hata kukupokea mizigo sio jambo la ajabu sana lkn kufanyika mara kwa mara na shemeji yako inaleta maswali kwasababu wahusika wapo ambao ni mkeo na h/g.
Shemeji ni mgeni hapo hivyo hana mamlaka yoyote kwa mkeo hivyo asivimbe kichwa na kuanza dharau.

Mtafutie mtaji afanye hata biashara ambayo itamfanya asishinde nyumbani na kupunguza mapishano.
Inaonekana mkeo hajawahi kukupa huduma unazozipata kwa shemeji, mweleze mkeo au tafuta rafiki yake wa karibu amweleze kuwa ndoa hainaga mazoea.kama anashindwa tu kumpokea mumewe au kumuandalia chakula basi ni yeye ndio anayekaribisha matatizo.
Fact
 
Wadau nawasalimu,

Kuna mgogoro wa kifamilia unafukuta nyumbani kwangu,

Ni kwamba kuna kaka yangu ambae alipata matatizo na yupo jela sasa takribani mwaka wa pili akitumikia kifungo cha miaka saba.

Huku nje familia yake ilishindwa kumudu kodi ya nyumba baada ya kodi aliyolipa jamaa kuisha, mkewe alikuja kuniona kwa ajili ya hilo, nami nikaliwasilisha kwa wazee ambapo walishauri niichukue hiyo familia tukae pamoja kwangu kwa kujibanabana hivyo hivyo.

Kwa kuwa kumlipia kodi kwa kweli kwa majukumu niliyonayo nisingeweza, maana ada za shule za watoto wake ni mimi pia ndio nalipa kwa sasa, tuliwatoa shule za gharama na kuwaleta za kawaida.

Wakahamia kwangu yeye na watoto wake, tunaamini kuwa miaka mitano iliyobaki katika kifungo si mingi sana, tukimwacha mwanamke aende njia yake si ajabu jamaa akatoka huku familia imepotea au kuchukuliwa na jitu lingine ukizingatia mwanamke hakua na kazi, ni house wife na wote tunajua jinsi hawa wenzetu walivyo dhaifu, nadhani wengi mmeshasikia simulizi nyingi za watu waliofungwa waliwakuta wake zao wako wapi pindi walipotoka huko.

Nyumbani amani imetoweka sasa, kati ya mke wangu na huyo shemeji yangu, huyu shemeji kiukweli ni mchapa kazi na mwenye heshima ya hali ya juu, nikirudi kutoka kazini huja mlangoni kunifungulia geti, baada ya hapo huja kwenye gari hunipa shikamoo huku amepiga magoti na kupokea kwa unyenyekevu mzigo wowote ninaokua nao.

Nikitoka kwenda bar nikirudi saa tano saa sita usiku huja kunifungulia geti anamzuia housegirl asiamke anakuja yeye, kisha hunipakulia chakula na kunikaribisha, ananisubiria anatoa vyombo na kuni wish good night.

Sasa hii treatment ambayo huyu shemeji ananipa imemkasirisha sana mke wangu ambae kwa kweli nimeshasahau mara ya mwisho ni lini alinikirimu hivi, mm uhudumiwa na hg na wengi wao huwa viburi sio kama anavyofanya shemeji,
Sasa umezuka ugomvi mkubwa ndani kati ya mke wangu na shemeji.

Usiku silali naambiwa nichague nimfukuze shemeji au yeye aondoke eti kama nimeona shemeji ni bora, mke wangu sasa haendi kulala mapema anakaa sitting room na shemeji hadi saa sita hadi nifike ili aone kama kuna kitu kinafanyika, ameshatangazia wanaukoo kuwa mimi na shemeji kuna kitu kinaendelea jambo ambalo sio la kweli.

Pia shemeji anapenda kuniita kwa jina la "" mume"" juzi mke wangu alimsikia akiniita hivyo na kumuuliza mume wako na nani ukazuka ugomvi mkubwa sana, wakati mwingine naporudi usiku mwingi shemeji anakua yupo ukumbini na mavazi ya kulalia akitazama series, mke wangu nae anatoka kuja kunisubiria hapo hapo akidhani kuna kitu labda tutafanya hapo na shemeji, hawazungumzishani kitu hadi mimi napofika, yule shemeji anawahi mezani kunipakulia chakula.

Juzi juzi tulikua tunakunywa bia mimi na shemeji yangu mahala fulani, huwa namtoa out mara moja moja ili walau apoteze mawazo ya matatizo yaliyowapata, nikatumia Muda huo kuongea ili ajishushe kuepusha ugomvi usiokua wa lazima pale home lakini akanijibu kuwa wife ndio anapaswa kujishusha kwa kuwa ni mdogo kwake.

La hasha nikampangie kwake yeye na wanawe niwe namhudumia huko, nikamjibu sina uwezo huo wa kuhudumia familia mbili, ukizingatia kuwa ndugu ni kama wamenitelekezea mm huu mzigo kila mtu anajifanya yupo busy na wengine wakilia ugumu wa maisha.

Wadau mnanishauri nini kuhusu tatizo hili, maana hali sasa ni tete, mke wangu amenipa ultimatum kwamba nimuondoe shemeji or else aondoke yeye, mimi tatizo langu kubwa ni wale watoto, hatima yao, inafikia hatua sasa mke wangu anawazuia watoto wetu wasicheze pamoja na wale wa kaka kutokana na ugomvi na mama yao.

Msaada wa haraka unahitajika



Sent using Jamii Forums mobile app

Mkeo kesha baini "mkakati OVU" wa shemejio ambao wewe wala hujashtukia na huonyeshi kushtuka hata tone pamoja na flirting zote hizo.

HUYO SHEMEJI ANATAKA KULALA NA WEWE.

Msikilize MKEO Kwakua Mkeo yupo sahihi kwa asilimia 100%.

Wanawake wanajuana katika mbinu za kutongoza na wanajuana kutambuana hisia zao kirahisi sana.
Mke wa kaka yako hapaswi kukaa hapo KWAKO muda wote huo. NI KUJILETEA MATATIZO.

Mtafutie Mradi na nyumba ya kupanga aondoke hapo home yeye na watoto wake, akakae kwake.

Mambo ya kuletewa Maji ya kuoga. Ni kama unalialia kua ungetaka uwe unapelekewa Maji. Kwanini unakuja usiku kila siku.?
Mambo mengine uangalie mwenyewe kama yako na tija ama la?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi wanasema mke wako ana roho mbaya. .
Ila samahani tu, mi mwenyewe siwezi kuishi na familia ya shemeji yangu kwa miaka 7. .

Kwa nini hasingeenda kuishi kwenu ambapo ni ukweni kwake?
Afu mwanamke ajishugulishe kutafuta chakula, wewe utafute hela za ada za watoto wake na mahitaji
 
Duuuh pole sana. Ila mke wako ana visa, na hajui thamani yako kwake.
Shemej naye apunguze speed, ili muone kama zle uduma anazokupa kama mkeo ataweza kukupa ili wivu uishe.
 
Back
Top Bottom