Mke wangu anadai niifukuze familia ya kaka nyumbani

Mke wangu anadai niifukuze familia ya kaka nyumbani

Kuna tatizo sehemu,tena kubwa,tatizo ambalo ww unazidi kulikuza na mkeo anazidi kukusaidia kulikuza..

tuanze na wewe,kwa nini wewe mke wa nduguyo anavaa nguo ya kulalia na anakaa sebuleni mbele yako bila ku hukua hatua ya kuzuia hali hyo?
Kwanini anakuandalia chakula na hulalamiki kila siku na umeridhika?kwa nn unaenda kuka nae bar bila mkeo?

Tuje kwa mkeo,je kwa nn amekasirika wkati hafanyi jukumu lake kwako?kwa nn mnafundishwa na hyo mgeni lakin wote ww na mkeo mmeshindwa kujifunza?unashindwaje kufundishana ndani chumban hali halisi ilivyo na mkeo ajifunze?kwa nn kila siku aridhike ww mumewe uandaliwe chakula na mke wa nduguyo na yy yupo ndani?kuchelewa kwako kurudi nyumbani hakuhalalishi kutokulala kwao mapema,je mkeo hana namba yako ya simu umpigie au akupigie mfungulie geti?upo serious kwel na ndoa yako bro?

Shemeji je anaona nafany heshima lakin ameshindwa kugundua hapo sio kwake na yte anayokusaidia hayastahili kwa sasa?ameshindwa kujua ww ni mume wa mtu na yupo kwa watu?anashindwaje kumwelewesha mkeo cha kufanya kam mkeo kajisahu?
Au bro unataka kumega kisela sema tu unashindwa kuanika hapa jukwaani?au ushamega?

Kuna tofauti kubwa kati ya mjinga n mpumbavu,mjinga anajua ila anajua vibaya,ila mpumbavu hajui kabsa na hajui kua hajui.. Utachagua kupi kunakufaa hapo...na kipi bora kwa faida yako na familia yko. Ita wote usimame kiume tabia hii huipendi na isirudiwe. Mkeo kamkanye chumbani kwamba afanye kam shemeji yako anavyofanya. Tchao
IMAAAGINE!
 
Shemeji yako so mkeo, imenishangaza anamtaka mkeo ajishushe na kukupa masharti ya kumpangia nyumba. Hajui kama mnawafanyia hisani na hamlazimiki kuwasaidia? Mkataze asikuhudumie, alikuta ukihudumiwa na mfanyakazi, na uliikubali hiyo hali, sasa yeye asiingilie maisha yenu zaidi ya kupokea msaada. Asikuite mume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwambie shemeji mwisho saa mbili awe ameshalala.asikufungulie geti.na mkeo mwambie hapo shemeji haondoki kama vipi aondoke aone nani atachekwa na dunia .fala sana asikutafutie dhambi bure.familia ya ndugu yako iteseke kisa mtu mmoja akwende huko
 
mwanaume unakosaje say na watu walioko chini ya paa lako!?how comes unaona kabisa hapa kuna linalotafutwa zaidi ya ushemeji na unakaa unachekelea unaanza kulinganisha unayofanyiwa na mke,KAMA SIO UFALA NI NINI?
mwanamke unashindwaje kujaza nafasi yako kwa mumeo?mume anarudi umelala,anapakua chakula umekaa,unashindanaje na mtu over ur husband?the whole idea ya kumuuliza mgeni huyu unamwita mumeo ni mumeo?huo ushindani unatpoka wapi?KAMA SIO UPUMBAVU NI NINI?
shemeji anajiwekaje wekaje kuandaliwa kuliwa?hata kama mkewe hafungui mlango?
hata kama mkewe hampakulii chakula?
kimbele mbele gani kinamkuta?KAMA SIO UMALAYA NI NINI?

SO WAMEKUTANA WOTE WAJINGA TUPU!
MMOJA ANACHEKELEA UPUUZI
MWINGINE ANAHOFIA KIVULI CHAKE
MWINGINE ANAKUSUDIA KUVUNJA NDOA YA WATU!
kuna nini hapo ?
Nimekusoma

Sent from my TV
 
Wewe unamtafuna au unaelekea kumtafuna huyo so called shemeji.......

1. Kukupokea mzigo na kukupkulia chakula si jukumu lake..... KIHEREHERE CHA NINI KAMA HAMTAFUNANI????

2. Anaanzaje kutoa amri ya kumzuia HG wakato yeye ni
mgeni? MNAKULANA NYIE

3. Guts za kukupokea na kusubiriana akiwa na night dress anatoa wapi kama HAMLANI AU MNAELEKEA KULANA???

4. Unaanzia wapi kumtoa mke wa kaka yako out bila mkeo? MNAKULANA AU MNAELEKEA KULANA...

5. Guts za kutaka mama mwenye nyumba ajishushe ametoa wapi....MNAKULANA AU MNAELEKEA KULANA

6. Unapakuliwa chakula na shemeji na anakusubiria umekaa tu unakenua mijino? MNAKULANA AU MNAELEKEA KULANA

7. Anakusubiria usiku wewe mumewe??? MNAKULANA


8. Anakyita mumewe??? MNAKULANA

Kiufupi kama sio chai hii basi :-

1. mshalalana au mshatongozana au mnaelekea ndio maana shemeji yako anahisi ana haki juu yako

2. Kama bado hajalalana (chance ni ndogo sana hapa kuwa hamjadukuana nyie) Huna msimamo kama mwanaume...mume na baba wa familia. Mwanaume mwenye uanaume wake lazima aweke mipaka..... yaani shemejio asingethubutu kufanya afanyayo.... keshakuona rahisi mno ndio maana

YAANI MKEO ANAPASWA AWAITE WOTE WAWILI MKAE KIKAO AWAPE DO N DONTS TENA AWE WAZI KWA HUYO SHEMEJIO KUWA IKISHINDIKANA AENDE AKAISHI UKWENI (na kilichomfanya asiende kwa wakweze ni nini? Watoto endelea kisomesha mama mtu akasubirie ukweni huko aone kama anaweza vaa night dress amsubirie baba mkwe wake mfyuuuuu)

Yaani na mashart ya wewe kumpangia anakupa??? Tchaaa
 
Huyo dada anachofanya ni kama kumshukuru shemeji yake kwa mema anayomfanyia yeye na watoto wake!!! Ebu tuache kuwa na negative perceptions.....unafikiri kuishi nyumba ya watu ni kitu rahisi eeenh????

Jamani...hata kama kuishi nyumba za watu mtihani...ndio ukeshe usiku kusubiria kufungua mageti ili hali kuna mke na dada wa kazi juu....Mbona kazi za kuamsha amsha ni nyingi tu za kuonyesha uwepo wako....usafi ndani na nje, kama kuna eneo tifua bustani ali mradi heka heka tu....
 
Huyo mkeo umwitie wazazi wote wa pande mbili wa kwako na wakwake wambie hali halisi watoto wa ndugu yako ndio wanao huyo mkeo unaweza kumuacha na akaondoka kwenda kuzaa kwengine lakini hao watoto watakwita tu baba mdogo or baba mkubwa na huyo SHEMEJI yako awe na ukarimu wa kweli sio wa pande mbili kukuvalia night dress si majanga hayo chupi ndani anavaa au kweupe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpeleke shemeji yako kwa wakwe zake, mpeleke kwenu akamsubiri huko mmewe. Kusema ukweli hata mimi nisingekubali. Hasa mwanamke kama huyo mwenye kimbelembele, unafikiri yeye hana matamanio, kuna siku mtavunja amri ya sita msipoangalia.
 
Hii Kauli ya shemej yako imeniogopesha sana aisee, Kama una uwezo wa kumpangia huyo shemej yako chumba Kimoja tu na wewe uendlee kubaki na watoto naamin itapunguza misuguano.
Huko atakuwa amempa freedom na yeye anatunza mali ya kaka mkuu.
 
Haya mambo yamevuruga ndoa nyingi sana,tena linapokuja swala la mke kutofautiana na ndg zako hapo bila misimamo na hekima kote unaweza kuharibu si ndg si mke,kwa mjibu wa maelezo yako mke ana haki ya kukuhisi vibaya maana wenzetu jicho la 3 limewapita kushoto,lkn jaribu kumwambia shemeji yako apunguze care kidogo amwachie mwenye majukumu hayo atimize maana hapo tatzo ninaloliona ni wivu zaid japo kwenye kuwaingiza watoto kwenye mambo yenu ndpo roho mbaya inaanza kuonekana,jaribu kufanya haya.Kisha utupe mrejesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguo za kulalia anavaa anakaa sebulen ili iweje..nawe unasifia tu nakuona mwanzo mwsho...
Unamtoaje outing[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32]
Kwakifupi ushageuza kibao...we na shemejio mnatafuta mchawi...
Yn mume wangu arudi ukimbilie kumsave food chaaaah...
 
Halafu unavyosema asijw chukuliwa na 'jitu' kaka yako aliyefungwa ni jitu pia.
 
Jamani...hata kama kuishi nyumba za watu mtihani...ndio ukeshe usiku kusubiria kufungua mageti ili hali kuna mke na dada wa kazi juu....Mbona kazi za kuamsha amsha ni nyingi tu za kuonyesha uwepo wako....usafi ndani na nje, kama kuna eneo tifua bustani ali mradi heka heka tu....
Hana lolote

Wanakulana hao
 
Maana naona tayar shemej mtu anataka kujifanya na yeye mama mwenye nyumba kumfundisha maza house majukumu yake
Wanawake hatuwezi kukaa nyumba moja lazima tutaanza mashindano ambayo mshindi hatakaa apatikane ilitakiwa hapo mmoja ajifanye mjinga.
 
Bro I'm not in your situation na sijui ningefanyaje ila from an observers point of view angalia nafsini mwako nia Ilikuwa ni ipi kumleta hapo na je bado ipo, think about your brother and if it were reverse ungependa iweje, kumbuka your brother is your brother for life. Wewe mwenye unajijua kama your intentions are still pure, usijaribu Kabisa kushawishika na mwanamke wa kaka yako. Kwa upande wa shemeji yako kukufungulia na kupakua msosi ni jukumu la mke kama halifanyi asilalamike badala ya kujishtukia na kuanza kufanya yeye analalamika. In short be the man of the house remember it all rests on you, usijibizane mkeo sema tamko au better kaa Kimya na sema this sentence ' I cannot abandon my brother's family. ' full stop

Sent from My BlackBerry Passport
 
Back
Top Bottom