Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uctuzingue hapa eleza kila kitu kama ilivyo la sivyo natoboa yote maana nakufahamu vizuri 1.nani aliyemwambia housigel asiwe anafungua mlango 2.mara ngapi mkeo kakukuta kwa shemejio ukatoa kisingizio kuwa ulienda kumuangalia mtoto anakoroma vibaya 3.......4.......5.....6....7.....8....9....10
Sent using Jamii Forums mobile app
Ashamtafuna anajikosha to coz mwez uliopita wife alitonywa na wambea shemeji ametoa mimba na hela ilitumwa kwa daktar kutumia cmu ya mume ... Cjui kwa nn anaomba ushauri huku anaficha haya
Sent using Jamii Forums mobile app
Damu nzito kuliko maji, hao watoto ni wa ukoo wenu, usiwatupe. Kuwa kama mwanamme, toa tamko kama hawezi kukaaa na shemeji yako aondoke aende anakotaka, huenda ana jamaa nje ndio kiburi. Na ww kwa nini usimtimizie huyo shemeji mahitaji yake ya kimwili? Yaani mpaka uoneshwe nn ndio ujue anahitaji? (duuu wanaume wa dar bana). Tafuna bana!Wadau nawasalimu,
Kuna mgogoro wa kifamilia unafukuta nyumbani kwangu,
Ni kwamba kuna kaka yangu ambae alipata matatizo na yupo jela sasa takribani mwaka wa pili akitumikia kifungo cha miaka saba.
Huku nje familia yake ilishindwa kumudu kodi ya nyumba baada ya kodi aliyolipa jamaa kuisha, mkewe alikuja kuniona kwa ajili ya hilo, nami nikaliwasilisha kwa wazee ambapo walishauri niichukue hiyo familia tukae pamoja kwangu kwa kujibanabana hivyo hivyo.
Kwa kuwa kumlipia kodi kwa kweli kwa majukumu niliyonayo nisingeweza, maana ada za shule za watoto wake ni mimi pia ndio nalipa kwa sasa, tuliwatoa shule za gharama na kuwaleta za kawaida.
Wakahamia kwangu yeye na watoto wake, tunaamini kuwa miaka mitano iliyobaki katika kifungo si mingi sana, tukimwacha mwanamke aende njia yake si ajabu jamaa akatoka huku familia imepotea au kuchukuliwa na jitu lingine ukizingatia mwanamke hakua na kazi, ni house wife na wote tunajua jinsi hawa wenzetu walivyo dhaifu, nadhani wengi mmeshasikia simulizi nyingi za watu waliofungwa waliwakuta wake zao wako wapi pindi walipotoka huko.
Nyumbani amani imetoweka sasa, kati ya mke wangu na huyo shemeji yangu, huyu shemeji kiukweli ni mchapa kazi na mwenye heshima ya hali ya juu, nikirudi kutoka kazini huja mlangoni kunifungulia geti, baada ya hapo huja kwenye gari hunipa shikamoo huku amepiga magoti na kupokea kwa unyenyekevu mzigo wowote ninaokua nao.
Nikitoka kwenda bar nikirudi saa tano saa sita usiku huja kunifungulia geti anamzuia housegirl asiamke anakuja yeye, kisha hunipakulia chakula na kunikaribisha, ananisubiria anatoa vyombo na kuni wish good night.
Sasa hii treatment ambayo huyu shemeji ananipa imemkasirisha sana mke wangu ambae kwa kweli nimeshasahau mara ya mwisho ni lini alinikirimu hivi, mm uhudumiwa na hg na wengi wao huwa viburi sio kama anavyofanya shemeji,
Sasa umezuka ugomvi mkubwa ndani kati ya mke wangu na shemeji.
Usiku silali naambiwa nichague nimfukuze shemeji au yeye aondoke eti kama nimeona shemeji ni bora, mke wangu sasa haendi kulala mapema anakaa sitting room na shemeji hadi saa sita hadi nifike ili aone kama kuna kitu kinafanyika, ameshatangazia wanaukoo kuwa mimi na shemeji kuna kitu kinaendelea jambo ambalo sio la kweli.
Pia shemeji anapenda kuniita kwa jina la "" mume"" juzi mke wangu alimsikia akiniita hivyo na kumuuliza mume wako na nani ukazuka ugomvi mkubwa sana, wakati mwingine naporudi usiku mwingi shemeji anakua yupo ukumbini na mavazi ya kulalia akitazama series, mke wangu nae anatoka kuja kunisubiria hapo hapo akidhani kuna kitu labda tutafanya hapo na shemeji, hawazungumzishani kitu hadi mimi napofika, yule shemeji anawahi mezani kunipakulia chakula.
Juzi juzi tulikua tunakunywa bia mimi na shemeji yangu mahala fulani, huwa namtoa out mara moja moja ili walau apoteze mawazo ya matatizo yaliyowapata, nikatumia Muda huo kuongea ili ajishushe kuepusha ugomvi usiokua wa lazima pale home lakini akanijibu kuwa wife ndio anapaswa kujishusha kwa kuwa ni mdogo kwake.
La hasha nikampangie kwake yeye na wanawe niwe namhudumia huko, nikamjibu sina uwezo huo wa kuhudumia familia mbili, ukizingatia kuwa ndugu ni kama wamenitelekezea mm huu mzigo kila mtu anajifanya yupo busy na wengine wakilia ugumu wa maisha.
Wadau mnanishauri nini kuhusu tatizo hili, maana hali sasa ni tete, mke wangu amenipa ultimatum kwamba nimuondoe shemeji or else aondoke yeye, mimi tatizo langu kubwa ni wale watoto, hatima yao, inafikia hatua sasa mke wangu anawazuia watoto wetu wasicheze pamoja na wale wa kaka kutokana na ugomvi na mama yao.
Msaada wa haraka unahitajika
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo dada anachofanya ni kama kumshukuru shemeji yake kwa mema anayomfanyia yeye na watoto wake!!! Ebu tuache kuwa na negative perceptions.....unafikiri kuishi nyumba ya watu ni kitu rahisi eeenh????Yani uko mbioni kumla shemeji. Kwasababu kwanza yeye atakua anakutaka, maana huenda kabla ya mme wake kufungwa alikua hamfanyi haya yote kwa mmewe
Pili kuna uzaifu fulani umeonyesha mbele yake kuhusu mkeo sasa anataka achukue hiyo advantage umtafune.
Hawa wote ambao wanasema huyu dada anaroho mbaya aithani alishaona mbele.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila mwambieni ukweli shemejie nae kazidisha,unajua unapofika kwa watu unatakiwa Ku behave kwa mujibu wa maisha aliyoyakuta sasa na yeye huyo bi Dada kazidi kujitia tia kwa shemejie,kujikalisha sebuline na night dress kwa shemeji yake si picha nzuri,ipo siku jamaa yenu hapa ataja sema shetani alimpitia,yeye kama baba anatakiwa kiyakemea yote mbaya ili hao wanawake waishi kwa amani humo ndani sasa akiwa lege lege tutarajie ipo siku atateleza tu maana speed ya shemeji si ya kitoto wallah,kumpakulia chakula mume wa mtu inauma jamani wee! Mimi kwa kweli sitaki kabisa hiyo kitu bora mwanaume apakue mwenyewe maana kwenye kuinama kuvuta hotpot waweza pitisha vijimaziwa vyako kwa bahati mbaya kwenye mkono wa mume wa mwenzio mambo yakawa hovyo hovyo!Damu nzito kuliko maji, hao watoto ni wa ukoo wenu, usiwatupe. Kuwa kama mwanamme, toa tamko kama hawezi kukaaa na shemeji yako aondoke aende anakotaka, huenda ana jamaa nje ndio kiburi. Na ww kwa nini usimtimizie huyo shemeji mahitaji yake ya kimwili? Yaani mpaka uoneshwe nn ndio ujue anahitaji? (duuu wanaume wa dar bana). Tafuna bana!
Hii ndo maana ,,katika uchaguzi wa kuoa nilazima uangalie sifa za nje kwanza .....binafsi napenda mwanamke kwanza apende watu sana ndugu jamaa namarafiki kisha apende kula
Uko sahihi na inaonekana kitumbua anapewa sio kwa kupetiwa hukoInawezekana kabisa nia yako ni njema kumsaidia kaka kwa kutunza familia yake, ila huo uhadithiaji wako tu nina mashaka kama kaka yako atamkuta huyo mke kuwa ni wake bado...khaa...
Huyo shemeji yako anataka kuvunja ndoa yako !! Yeye hapo ni mgeni amekaribishwa tu, kwa kweli huyo shemeji yako anakutaka ila anashindwa kukuambia sasa anakwambia kwa vitendo, ataivunja ndoa yako kua mwangalifu.1.Hongera sana kwa kumfadhili kaka yako aliyepo matatizoni, huo ni uanaume.
2.Wanawake wakikaa pamoja ni desturi yao kutoaminiana.
3. Mpangishie shemeji yako mpe na mtaji ili azalishe pato lake.
Safi bila shaka ukipenda kula lazima unajua kupika , nawewe sio mchoyo !!!.....Napenda kula mimi jamaniii