Mke wangu anadai niifukuze familia ya kaka nyumbani

Fukuza yeye hana adabu ufukuze ndugu zako huko mkeo ovyo saaana mwambie mi sijapenda kbs

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani amfukuze mke wake yeye aishi na shemeji yake huo utakuwa ujinga. Kinachotakiwa kama wazazi wapo wampeleke huyo mwnamke huko akawasaidie yeye abaki na watoto wa kaka yake, lasivyo nyumba itakuwa inawaka moto
 
Unatakiwa umpeleke huyo mkeo wa wazazi wako au wake akaishihuko wewe baki na watotot. Halafu wanawake wengine tunashindwa kujiongeza yaani yeye anafurahia kukaa hapo kumfungulia shemeji yake geti huku mkewe na house girl wapo. Mimi kaka yangu alipata matatizo tukajadiliana mke wake aende kukaa na mama huku tukiishi na watoto wake mpaka mume wake matatizo yakaisha. Yaani miaka miwili upoupo tu unakazi ya kufanya majukumu sio yako lazima utachukiwa.
 
Nae ana kiherehere si aache kama vinamkera mkeo,mkeo ndio awe anakufungulia
 
Msikariri nguo zote za kulalia ni nyepesi kuna nguo za kulalia nzuri tu
 
Kwa maelezo haya inaonekana kabisa kuna kitu kinaendelea kati yako na shemeji yako,, naulaumu sana muziki wa singeli unaokula mashemeji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
4. Punguza mazoea yaliyopitiliza kwa shemeji yako, maana mnakoelekea utamla kabla kifungo cha jamaa hakijaisha au utaanza kumwonea wivu siku akipata lijamaa (kumbuka nae n binadamu mwenye hisia)

Huu ndo ukweli mtupu. Kama bado huumalizi mwaka huu kabla hujachungulia mali ya kakako.
Ushauri;
Mrudishe kwa wazazi wako au wake yeye, waeleze kuwa utamsaidia chochote utakachopata. Kuhusu kumpangia chumba si kweli, hapo ndio kabisa kishawishi kitazidi kwani miaka 2 hii shem hajauona mhogo wa jyang'ombe. Wadhani yeye hakumbukii kakako alivyo mpa??
Huruma yako itakuponza hata akija kakako akute umeiongeza familia. Wadhani kakako akija atakuheshimu sana kwa maneno atakayo yakuta hapo kwako?? Mrudishe kwao au kwenu umhudumie pale
 
Usikute huyo shemejio kwa mumewe wala hajawahi kuwa hivyo!
 
Hahaha... Shemeji anataka kulipa fadhila...
 
Na kwa nini awahi kukupakulia chakula? asubiri mume wake atoke jela ndiyo atoe hiyo huduma,na pia mkeo anakuwa wapi mpaka unachotewa chakula? kuna shida mahali pia ww unamchukuaje shemeji bila mkeo kwenda baa? maswali ni mengi.
 
😀😀😀 WAKAE KWA KUTULIA.
 
Mnachoshindwa kuelewa ni kuwa huyo mkeo amekosa amani na matendo ya shemej yako. Mbona hakukataa usimlete mwanzoni. Why anaplay role kama za mke? Anakupakulia chakula na kukufungulia geti? Hebu vaa viatu vyake? Lazima ahisi kuna ktu ingawa si kweli.

Huyo shem wako anapaswa kukaa kwa kutulia. Na hapasw kusema et hawez jishusha kisa mkeo mdg kwan hapo kwake? Wanajishusha mama zetu wakubwa huko majumban kwetu sembuse yeye. Hebu mpe amani mkeo. Mwambie shem ajiheshimu wewe sio mmewe. Una mtu wa kukufanyia hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…