Habarini?
Ni leo ya asubuhi kabisa akaniambia kuna kitu anataka kuniambia,nikamwambia "sema mke"
"Unajua tangu tujuane huu mwaka wa tatu hujawahi kuniridhisha?" Hili swali limenistua mpaka nikaanza kumuonea huruma mtoto wetu mwenye miezi minne tu.
Swali hili nimeliona ni zito mno kwangu kwasababu sidhani kama nitakuja kuwa na uwezo zaidi ya ninaouonesha tangu tulipojuana na mpaka sasa hivi.
Kutokana na swali hilo pia moja kwa moja nikaona huyu simfai na wala hanifai tena yaani hakuna anaemfaa mwenzake kwenye suala la kuridhishana kitandani na kumbe ni mimi tu ndyo nilikuwa najiridhisha.
Akili yangu inaniambia kwamba niachane nae tu lakini akili nyingine inaniuliza huyu mtoto ataishije bila baba?
Yaani kiufupi nmeanza kupitia wakati mgumu sana kwenye hii ndoa.
Naombeni ushauri wenu lakini usahuri ulenge hasa kwa maslahi ya mtoto tu!.
Ahsanteni
Kama kweli limetokea, basi kuna tatizo kubwa.
Chukulia jambo hili kiume zaidi kwa sababu unavyotutaka kukushauri juu ya watoto pekee bila kuunganisha jambo lote, tutakudanganya, haitawezekana, ushauri hautaunganika.
kukushauri ni lazima tuguseguse maeneo yote bro, ukatae ukubali.
Tuanze na historia yake kwanza, kisha tuje kwenye mahusiano yenu.
Yeye ni mzaliwa wa ngapi kwa wazazi wake.
Je alilelewa na wazazi wake wote katika ndoa?
Je kabla ya kumuoa wewe, aliwahi kuishi kinyumba na mwanaume mwingine?
Je ndoa yenu ina muda gani,
Kabla ya kufunga ndoa mlianza mahusiano ya kimapenzi kabla?
Je historia ya mahusiano yenu ulitumia nguvu kubwa, hasa nguvu ya pesa kumpata?
Je kabla ya kutamkiwa hayo, kuliwahi kutokea ugomvi ambao ulitokana na wewe kugundulika kuwa una mchepuko?
Je una mchepuko ambaye unadhani mkeo hajui?
Nitapenda maswali yangu ya dodoso uyajibu ili niweze kushauri sawa sawa.
Lakini kabla haujanijibu ninakupa angalizo:
Kuhusu kulea watoto, hakuhusiani na mapenzi na ndoa, kila jambo linajitegemea.
Chukulia mfano, je angelikufa ghafla hao watoto ungeliwaleaje?
Hilo la kwanza, la pili ni kwamba mapenzi hutoka rohoni na si kutokana na ngono pekee.
Hivyo kutokumridhisha kimapenzi, kunamaanisha muunganiko wa mambo mengi kiujumla wake, kunabeba mustakabali karibia wote wa maisha yenu ya ndoa.
Usije ukamnywea 'mkongo' ukidhani haumlali kiufasaha kama wengi naona wanakushauri humu, utakuwa umejidanganya pakubwa.
Nijibu hayo maswali nipate 'catch word' ya kuunganishia.