Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Fukuza hiyo mbuzi
 
Mi naona huyo mama ni wale watu wa fujo/kupigana yaani ni wale watu wauaji
Kama kimo cha tofali kwa mtoto je kwa mtu mzima mwenzio si ataweza kubebea kisu.
Miaka nane kama kakosea kosa gani ubebe tofali???
Aiseee mi nina wasichana wangu wawili wasaidiz juzi nilitoka safari nikawa nimelala my best food ni maarage nazi ubwabwa
Nimerudi tu niakingia ndani nikawaambia waeke maarage
Wakawasha tv…niko chumbani wakayaunguza kama kau kau afu wako wawili age kama wanalingana 19-18
Aisee niliongea jamani mpaka nilijiskia vibaya nikatamani ningeingia tu ndani na kuendelea na kingine
Baadae wakapika kingine wakaja wakawa wananisemesha kama hakijatokea kitu huku wanaangalia mwamposa
Unajua kwanini they are that comfortable kwa age hiyo
Sababu i cant go physical lakin pia siwaonei lakini pia najua ni watoto…..
Sometimes nawafurahia saa ingine wananiuzi maisha yanaendelea
Hawa ni hawa nilionao
Na ni wakubwa nawachukulia kama watoto basi
Kwanini huyo mama asimvhukulie tu huyo kama mtoto
Basi kama zamani wazazi walikua wanasema ukikua utajionea mwenyewe
 
Wewe utakuwa umemchoka shemeji mpk unatamani likizo ya kurudi 😹😹😹
Hapana sijamchoka lakini kurudishwa nyumbani haiwezi ikawa adhabu kwangu...itakuwa adhabu kwake.
Kwangu ni vacation😅😅😅. Hata nigombane nae vipi atahakikisha sirudi nyumbani yaani yupo radhi asiende kazini anichunge nisiondoke..
Iwe nimemkosea au amenikosea yeye ipo hivyo siku zote.
 
Huyo Mwanamke hata ww kukuua ni Dakika sifuri
 
Sawa Dada ila mfundishe kazi huyo mtoto kazi si mateso, hata kama una dada wa kazi amsadie hata kufuta vyombo, wakaao kwangu si kike si wa kiume ni kazi tu
 
😂😂😂 umefanya nikumbuke ya home kwangu.!!
Nna vijana wa dukani kuna siku niliwarekodi walichokuwa wanaongea sikutaka tena kuwafatilia nahisi ningekufa na presha.!!
Huku nyumbani ndio usiseme nna kijana wa kiume alimshawishi dada wa kazi akubali wanaume wanaomuita ili awachune wapate pesa.!! Nilipiga hiyo siku, halafu baadae huruma ikanijia nikaanza kumbembeleza.!!

Dada na kina kaka wa dukani nikianza kuongea mpk nachoka, kuna muda nasema au mnaniona mdogo ndiomana mnanidharau?? Au kwa vile sina mume hamnisikilizi?? Ila ndio hivyo nawapenda na jana wote tumeenda kutazama mpira wa Simba na Yanga. Tuko na furaha.!!

Sasa huyo mwenzetu ataweza kuishi na watu wengi ambao sio ndugu zake km sisi??
Mara nyingi hao wa hivyo wachoyo na waficha vyakula, hao km unaenda kusalimia utamuona kanuna.!!
 
Mke mwema hutoka kwa Mungu. Mimi mkewangu anaishi na watoto wa mdogo wangu na aawapenda mpaka sometimes nahisi Mimi Sina mapenzi nao kama yeye. Na siyo kwamba wazazi wao hawapo wapo ila walitengana. Ndo maisha lakini .hapo cha kukushauri Mzee huyo dogo mpeleke boarding school na akifunga likizo mpeleke kwa ndugu Yako mmoja unaemwamini . Atakua mkubwa tu siku hazigandi.
 
Anajua utaenda kusalimia mashem wa zamani kwani yeye mjinga? 🤣🤣🤣
Shem anakupenda na ana wivu analinda mzigo wake.! 😹
 
Be a man.
Chukua uamuzi wa kiume.
Sema na amua kuwa mtoto yeyote ambaye hamkuzaa wawili aondoke ndani ya masaa 24. Usibadili uamuzi.
Mchukue mtoto huyo wa dada mpeleke kwa ndugu utatuma pesa kidogo kila mwezi. Na huyo nguchiro wake aondoke haraka.
Hapo utaiponya ndoa yako na atakuheshimu kuwa wewe ni mwanaume unaweza kuamua jambo mda wowote .
Huyo mke wako ukimlea hivyo ipo siku atakuua hao watoto wenu wakikua.
Be a man
 
Anajua utaenda kusalimia mashem wa zamani kwani yeye mjinga? 🤣🤣🤣
Shem anakupenda na ana wivu analinda mzigo wake.! 😹
Wala sio sababu...mashem wa zamani watasalimiwa tu nikitaka😅😅
 
Mtoto ahame tuu hakuna namna, familia ni baba, mama na watoto, yeyote zaidi ya hapo ni ndugu tuu mpita njia, akiingia kuishi na familia lazima makubaliano ya dhati yawepo, mmoja akikataa huna haki ya kulazimisha, kumbukeni binadamu ni kama wanyama tuu, ndio maana simba akimkuta jike ana watoto kitu cha kwanza anaua wote anaanza upya, wenzetu wazungu hawana longolongo za wajomba au shangazi ni wao tuu na watoto wao, ila alichofanya ni ukatili lakini nature ndivyo ilivyo hampendi anamuona Kama mvamizi tuu, na haya mambo ni very common kwenye familia nyingi ila hatuongei tuu, kwa issue hii huyo aende kwa bibi au babu ndipo atapata mapenzi ya kweli na umsaidie huko kifedha, Kama hawezi boarding inamhusu ila hapo hakai
 
😂😂😂😂😂 jaman wanachuo wakae hostel
 
Kati ya wewe na mkeo nani mwenye hela zaidi? Wewe ndo unamtesa mtoto kwa kushindwa kutumia madaraka yako kama kichwa cha familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…