Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Hivi mtu unawezaje kuishi na mtu ana roho mbaya????
 
Upendo hausisitizwi, huyo mwanamke ana roho mbaya tu kwa ndugu wa mumewe . Hapo hakuna mazungumzo ya kurekebisha hiyo shida, options ni mke au mtoto aondolewe hapo nyumbani.
 
Inawezekana sana tu
Kwasababu tabia hazijifichi na hata kama ikijificha utaona tu mtu akiwa ana roho mbaya anakuwa hana upendo na utu na kwa hilo kosa kumfanyia mtoto ni kubwa sana .upendo haubagui hawa wa kwako au sio wako
Huyo mke ana matatizo ya akili makubwa sana kiufupi ameoa kichaa
 
Duh, pole sana mkuu! Akina mama sijui wakoje. Yaani wanataka tulee watoto wao wa ndugu zetu hawapendi hii haiko sawa wanatakiwa wajitafakari sana! Wa kwangu naye alitaka kuleta ujinga huo nikamtolea uvivu. Maana nilikuwa namwona nyumbani kwangu kunakuwa na mafuriko ya ndugu zake na hapo utamuona meno yote nje wakija wa upande wangu hayo meno huyaoni! Nikamkalisha kitako na kuweka msimamo! Nashukuru Mungu alinielewa! Sasa huyu wako mkuu mkumbushe watoto yatima hawateswi, maandiko matakatifu yanasema Mungu naye atalipiza kisasi kwa ajili yao kwa kuwaueni nyie ili watoto wenu nao wawe yatima.
 
Kumpeleka boarding ni kukwepa majukumu,mke anatakiwa arudishwe kwao pamoja na watoto wa ndugu zake. Akae kwao hata mwaka mzima mpaka akili zimrudi na ikiwezekana iwe ni talaka mazima. Mwanaume hatakiwi kui-entertain upuuzi,huyo mama hana tofauti na wale wanajeshi wabakaji.
 
Yaani mwanamke muuaji huyo bado uko nae. Na haitaishia hapo,hiyo kuna siku atakufanyia wewe mwenyewe kitu cha hatari. Na mke anaesemaga naona umenichoka bora nirudi kwetu. Huyo ni mzuri sana,hapo hapo ni kumwambia aende. Na usigeuke nyuma,wala kumfikiria.

Kama bado unaona ubaki nae huyo mwanamke ni bora huyo mtoto umpeleke boarding
 
Wanawake bwana hapo ukimzidi ujanja anaweza hata kukuwekea sumu.
 
kaka mkeo ana tatizo la akili, haya mambo sio ya miaka hii kabisa
 
Duh hii ndo shida ya kumpenda zaidi mwanqmke kuliko anavyokupenda yeye mkuu.Kwa sie wengine hilo haliwezi kutokea sababu mwanamke ndiye anayehaha kukupalilia ili tu usimteme hivyo ukileta ndugu atampambania kumuonyesha upendo sababu ataamini huyo ndo mtetezi wake.

BTW Mkuu japo hauna mke hapo hebu jiformat tena.Usihangaike umpeleke wapi mtoto huyo ni damu yako pure aishi kwako kwa sharti moja kubwa kwa mkeo kuwa achague kuishi kwa upendo na huyo mtoto au akaishi kwa upendo kwao na ndugu zake.


Kamwe usikubali ampe mtoto majuto sababu hakupenda kuishi bila mama na ukifanyacho kumlea kina malipo makubwa kwake,marehemu Dada yako,familia yako na kubwa kuliko vyote kwa Mwenyezi MUNGU.


SIMAMA IMARA BRO hili halikupaswa hata kuombea ushauri humu.
 
Ningekuwa mimi ningesema afanye haraka kujiandaa nimsindikize.
Kuna mambo ya kubembeleza.
Huyo atakuwa anakuchapa kwa fimbo hiyohiyo, maana anajua akisema nitaondoka unanywea.
 
Ipo siku kilio hicho atakilipia na yeye
 
Sijui kwanini wanawake wa hivyo wanapata wanaume wa aina yenu wapole...Mimi ningekuwa nimemvunja mguu kama alivomganyia mtoto wa dada,Tena marehemu. Aisee ningeua, kwanza kwa hulka yangu hata asingewaza kufanya hivo.

Mtoe hapo nyumbani uyo mwanamke ibilisi, mtoto miaka nane unampiga na tofali!!!? Nimejisikia vibaya sana
 
Aisee pole sana, huyo mkeo ni utafikiri hajaingia leba?. Cha kufanya mpeleke huyo mtoto shule ya boarding awe anarudi likizo tu, na then mwambie atoe ndugu zake ajue pa kuwapeleka pia, iwe pasu kwa pasu. Mke usimuache , utaacha wanapi?, Mana Kila binadamu ana mapungufu yake, unaweza kutana na bomu zaidi ya Hilo. Hila tu unatakiwa kuishi naye kwa akili mandhari umeshamjua tabia yake halisi, huyo hatoweza kukaa na ndugu yako yeyote yule.
 
Akirudi likizo si ndio atampa sumu kabisa.
Vitafunwa vimesababisha apasuliwe mguu, na tumeambiwa shule haendi ili awe mtumwa hapo nyumbani.
Bahati mbaya jamaa kaoa shetani maana hata yeye anatetemeshwa.

Nilishawahi kupiga kofi mke wangu miaka 27 iliyopita mpaka hivi leo analikumbuka.
 
Mnaoa wehu ndio tatizo halafu mnapenda hasa
Hata afanye nini utakalia kulia lia vijiweni ukirudi home kama sio wewe
Ngoja akupe sumu tu
Huyo mtoto ana dhambi gani wewe ushindwe kumlinda kama sio wehu na wewe pamoja na upofu wa mapenzi

Mpeleke polisi huyo kama huwezi ustawi wa jamii wapo
Yote ukigoma basi weka namba tuchangie boarding school fees zake
 
Ushauri huu asipoufanyia kazi basi atakuwa tayari mjomba wake afe kwa mateso anayopata kwa mke wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…