Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Kabisa huyo ni anastahili kufunguliwa kesi kama child abuser

Tena hii itakuwa ndio njia rahisi ya kuachana nae, maana huyo mwanamke akitoka hapa atakuwa na hasira sana na yeye kitu kitakachopelekea kutoendelea na hiyo ndoa.
Yes, hii ndio njia nzuri na sahihi zaidi ya ku-deal na huyo mwanamke shetani.
Awe makini Sana huyo mume, siku moja atakuja kufanyiwa uovu wa namna hii hii au zaidi ya huo. Huyo Mwanamke ni adui mkubwa sana kwa usalama wa huyo mume na ndugu zake, akiendelea kuwa naye ipo siku moja maadui wa nje pia wataweza kumtumia huyo mwanamke ili amuangamize na kumuua huyo mume. Kulikuwa na kisa kimoja Cha ukatili wa namna hii kilichomhusu jamaa mmoja alikuwa anaitwa Oscar (Kama sijakosea Jina), nasikia alikuwa Mhasibu katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), naye alikuwa anaishi na mwanamke shetani wa namna hiyo hiyo. Mwisho wa siku nasikia huyo mwanamke wake alishirikiana na "wauaji" wa nje na kufanikiwa kumuua mume wake huyo, inasikitisha Sana kusikia kwamba yule jamaa aliuawa kikatili Sana, inasikitisha.
Naamini Watu wa HESLB wapo humu mtandaoni, wanaweza wakatupatia shuhuda nzuri zaidi kuhusu mkasa mzima wa kuuawa kikatili kwa huyo mfanyakazi mwenzao aitwaye Osca. Nafikiri watakuwa wanakumbuka vizuri tukio Hilo.

Kwa hiyo huyo bwana awe makini sana na huyo mke wake katili, siku zake naye zinahesabika.
 
wanakaa watoto wa miaka 3 iwe wa 8,?

kwa hyo unataka amuache hapo huyo dada yako mwenye roho ya shwetwain amuue? au kwa vile nimesema hao watoto wako wafukuzwe hapo ndo kimekuuma.

KIAZI WAHEEED
Kukaa wanaweza kukaa lakini haimaanishi kuwa ni sawa. Hii tabia ya ku outsource malezi ya watoto wetu ndio imechangia mno kubomoka kwa jamii zetu. Mtoto wa chini ya miaka 12 anatakiwa alelewe na wazazi wake na sio institution.

Sasa badala ya kupambana na huyo unayemuita shwetwain unamkimbiza malaika asie na kos! Ni ujumbe gani unaoutuma? Kwa sababu shwetain hamtaki mtoto pale nyumbani hauoni kuwa utakuwa umemzawadia kwa kumuondolea huyo malaika? Stupid as stupid does.

Amandla...
 
Fukuza hio takataka mm siwez kua na mwanamke ambae hapendi ndgu zangu.. ww kaz yako ni kusaidia watu Baki tu hadi lin pumbavyu
 
Fukuza oa mwingine mwenye roho ya upendo kwanza wakat unalioa hukulijua kua lina roho mbaya wanaume wngine bana umezingua sana
 
Eeeh! Naandika nafuta, naandika nafuta..... Natamani kungekuwa na Ku comment kwa voice note
 
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni jumamosi na jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani
Piga chini huyo mke wako, kama umeweza kusomesha ndugu zake bila kinyongo chochote iweje huyo mtoto mdogo awe kero kwake. I'm short huyo mkeo siyo liziki yako , uko mbeleni utapata shida sana. Nguvu zikianza kukuishia atakukimbia na yeye. Piga chini mara moja. Hao wanawake wapo design hiyo kwenye jamii akikuta na wewe ni kibwetele atakupanda kichwani.
 
Wala hutakiwi kumuogopa mkeo mueleze tu anachokifanya sio sawa angekuwa yeye hayupo duniani ingekuwaje kwa wanae?
Kweli kabisa, anajihesabia haki kana kwamba Dunia ni yakwake na ataishi milele mabaya hayawezi kutokea kwake ,binafsi nongewaomba radhi wanangu kwakiwachagulia mama shetani na kuwatafutoa mama mdogo fasta IMEISHA IYO
 
Pole sana mkuu

Ila huyo mke ana roho mbaya
 
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni jumamosi na jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani
Yaani baba wa familia hujui kinachoendelea nyumbani kwako?
Wewe ni MPAMBUVA SANA.

Sijui una uamzi gani lkn mimi kwa upande wangu kile kitendo cha huyo mwanamke kuniambia kuwa huyo mtoto ni mchonganishi ama la yeye aondoke wala nisengeli tafuta ushauri kwa yeyote,huyo angelikuwa alishaondoka mapema.

Siku ukimtoa huyo mtoto kwa kutii amri za huyo Delilah mateso sasa yata hamia kwako.
 
Yaani sisi baadhi ya wanawake ni maroho mbaya,eti katumwa kuwagombanisha mtoto mdogo namna hiyo tafuta la kumuweka huyo mtoto maana mke wako hamtaki afu kabla ya kumtafutia pa kukaa hvi
Kwani hapo nyumbani kwako mke ni wewe au yeye ni mke? Namaanisha kiongozi wa familia yako ni nani
Atafute pa kumuweka? Yeye ni mjomba na mjomba ni mama, ampeleke kwingine 😥Atatupa sababu Gani sisi ndugu zake? Akituelezea What happened automatic itatengeneza Chaos Sisi familia na mke wake.
Aonyeshe uanaume wake hapa. 🙂
 
Mwanaume unatakiwa kua na authority kwako, mi siwezi kukaa na mwanamke eti kitu kidogo anatishia aende kwao, ungemuacha aende huko na usimfate mpaka arudi mwenyewe, la sivyo ashajua udhaifu wako, Kila mkigombana atakua anatishia kwenda kwao

Kuhusu huyo mtoto, kama Kuna ndugu mwingine anaweza kukaa nae basi fanya mpango huo wewe ugharamikie Kila kitu kwa makubaliano kabisa, kuanzia mavazi,elimu,chakula,matibabu etc... Mtoto kukaa sehemu anaponyanyaswa huathirika physiological.... Mnamletea shida tu za badae huyo mtoto

Hilo lishemeji ulilitoa wapi?
Na akae akijua huyo mtoto akiondoka huyo shetani ataanza kumtesa huyu boya.
 
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni jumamosi na jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani

Kama sio chai wewe ndo umeolewa
 
mpaka unaandika huyo mke yupo tu? wanawake wana roho mbaya sana. wanaegamia kwao.wewe letq ndug zako siku 2 tu kanuna
 
Hilo ndio chaguo lako na ushazaa nae watoto wawili utakapomuacha fikiria mustakabali mzima wa watoto wako na wewe , Kama unaweza mtafutie shule nzuri ya boarding akakae awe anakuja nyumbani likizo tu. Na wewe uanze kuweka mipaka Kwa ndugu zake
Huo upuuzi sifanyi mimi.
Kama atachagua na kuwatesa watoto wangu basi sawa lkn siwezi kukaa meza moja eti ninazungumza na mwanamke wa namna hiyo.

Ni lazima ataondoka yeye na ndugu zangu wataendelea kula mema ya Nchi.
Huyo siyo mwanamke wa kuongea naye hata kwa kula chakula alichokipika,ni zaidi ya shetani.
 
Umeoa au umeolewa? Mpaka wmanamke anakutishia kuondoka wakati yeye ndo amekukosea ujue hapo umeshatekwa.

Mwanamke anajua huwezi kumfanya chochote hata akikusoea kiasi gani kwasababu unaogopa kumpoteza.

Binafsi ningemsafirisha mke usiku huo huo. Kurudi kwake ni baada ya bonge la kikao cha pamoja na wanaukoo wake wote na siyo wazazi wake tu.

Mtoto wa kaka yake pia angeondoka naye ila watoto wangu na mtoto wa dada yangu wangebaki. Ningeita ndugu upande wangu aje awahudumie watoto wangu kipindi hicho hata kwa gharama.

Huo mziki ningeucheza kwa mwaka mzima, akae kwao kwanza. Hakuna kupokea mawasiliano ya aina yoyote toka upande wake hata awe ni baba mkwe.

Hapo ndo ungemaliza huo ujinga. The moment mtu anahisi huwezi kuishi bila yeye, tambua umekosea mahali na unatakiwa kama mwanaume usimame katika nafasi yako.

Kimsingi mwaname hadodi, takwimu zinaonyesha kwamba duniani kuna wanawake wengi kuliko wanaume. Sasa ukiaply business principle ya demand and supply, utagundua kwamba mwanaume ana control soko na siyo kinyume chake.

Ya nini kukubali ujinga!?
Itakuwa wewe ni ndugu yangu.
 
Kuna asilimia kubwa hii story ni fake lakini ni uhalisia kwamba wanawake ndio viumbe wenye roho mbaya na katili hapa duniani. Hasa wao kwa wao. Na hii inazidi kama mwanamke mwenyewe ni wale washamba unsophisticated wenye hali ya chini. Afadhari kidogo wale classy.

Kama hii story ni ya kweli, basi wewe hufai kuwa mzazi. Mtoto wa dada yako ni kama wa kwako. Huyo shetani mliyekutana naye ukubwani ulitakiwa umvunje vilevile akili ikae sawa. Inshort huna mke hapo.

Alafu mtoto wa miaka 8 hapelekwi boarding school unless unapanga kumuua.
 
Kuhusu masuala ya mwanamke wa mtindo huo huwa sina muda wa kumumunya maneno.
Yawezekana usiku huohuo angelianza kuondoka yeye kabla hata sijampeleka mtoto hospital.
 
Mzee kifupi ulioa shetani, mtoto mpeleke boarding, anatishia kuachana mwambie yes unaweza kuachana nae kisa huyo mtoto, na kwa msisitizo mrudishe kwao, kusanya ushahidi kutoka kwa wapangaji wako, wachukulie maelezo na uwarekodi kwa sauti(sio video) nakiri hayo maelezo kichwani, kisha mpeleke kwao, wakikuuliza shida nini, waeleze A to Z, onesha hadi picha ya x ray za mtoto alipovunjika.. Waeleze wazazi wake kiunagaubaga, mbona we umelea watoto wa upande wa kwao bila tabu yoyote, hukatai mtoto kufunzwa lakini mkeo hafunzi ni anamtesa mtoto, na kwa hilo uko radhi kumpiga kibuti mazima.
 
Back
Top Bottom