John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Yes, hii ndio njia nzuri na sahihi zaidi ya ku-deal na huyo mwanamke shetani.Kabisa huyo ni anastahili kufunguliwa kesi kama child abuser
Tena hii itakuwa ndio njia rahisi ya kuachana nae, maana huyo mwanamke akitoka hapa atakuwa na hasira sana na yeye kitu kitakachopelekea kutoendelea na hiyo ndoa.
Awe makini Sana huyo mume, siku moja atakuja kufanyiwa uovu wa namna hii hii au zaidi ya huo. Huyo Mwanamke ni adui mkubwa sana kwa usalama wa huyo mume na ndugu zake, akiendelea kuwa naye ipo siku moja maadui wa nje pia wataweza kumtumia huyo mwanamke ili amuangamize na kumuua huyo mume. Kulikuwa na kisa kimoja Cha ukatili wa namna hii kilichomhusu jamaa mmoja alikuwa anaitwa Oscar (Kama sijakosea Jina), nasikia alikuwa Mhasibu katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), naye alikuwa anaishi na mwanamke shetani wa namna hiyo hiyo. Mwisho wa siku nasikia huyo mwanamke wake alishirikiana na "wauaji" wa nje na kufanikiwa kumuua mume wake huyo, inasikitisha Sana kusikia kwamba yule jamaa aliuawa kikatili Sana, inasikitisha.
Naamini Watu wa HESLB wapo humu mtandaoni, wanaweza wakatupatia shuhuda nzuri zaidi kuhusu mkasa mzima wa kuuawa kikatili kwa huyo mfanyakazi mwenzao aitwaye Osca. Nafikiri watakuwa wanakumbuka vizuri tukio Hilo.
Kwa hiyo huyo bwana awe makini sana na huyo mke wake katili, siku zake naye zinahesabika.