50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,088
- 4,059
Hili la mume kumficha mke siri (za maendeleo) ni hatari sana. Nina kisa cha mtu wangu wa karibu Sana kupoteza mali nyingi kwa vile alijitenga kumshirikisha mke kwa vile hakuwa na kifua.Amwambie mke ajifunze kutunza siri,kama akishindwa kutunza basi aanze kufanya mambo yake kimya kimya....kama mke atakuwa na akili atajifunza
Sisi tuliobaki tukakubaliana kwa kauli moja kuwa mke akiwa mkorofi, hatunzi siri Dawa ni kumpandisha cheo awe Bi Mkubwa. Kisha aambiwe sifa za kumpandisha cheo. Baada ya hapo zoezi la kusaka Bi Mdogo mwenye kifua linaanza rasmi. Lengo ni kuhakikisha siri za maendeleo zinae wa kuzitunza. Ni somo ghafi hili tulipewa. Tunazingatia.
c.c malembeka18