Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

ndo maana sometimes naona kumuomba mwanamke (mke) wako msamaha ni upuuzi tuu.....kwanza hilo ndo itakuwa fimbo ya kukuchapia.....fanya hivi.....mwambie hamia kanisani wiki 2......halafu uje ntakuwa na majibu.....
 
Huyo mama anaoneka hayupo sawa atakuwa ametoa hayo masharti kwa akili za kuambiwa/kufundishwa sio zake
 
Hata kama amenilisha LIMBWATA la damu ya binadamu kamwe siwezi kutekeleza huu upuuzi wa namna hii, katu kabisa siwezi.
 
Kupga magot na kuitana mama mm siungi mkono ila kwa msamaha jamaa aende tu
unaelewa maana ya kujichoresha? hiko unachotaka jamaa afanye ni kujichoresha. kila muumini atakaemuona barabarani atakua anajua uovu aliotenda. sio kitu kizuri. yaishe tu chinichini
 
Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.

Msamaha wa kweli na unaotoka moyoni kamwe hauna masharti. Mwenye kutaka kusamehe, husamehe na husahau. Kama una macho ya kusoma na akili ya kuelewa nilichoandika, utaelewa ninazungumzia nini.
 
Naskia ucchungu wanaume tunazidi kupungua...

Mke wako amepata wapi ujasiri wa kukwambia upuuzi huo aiseee !!!

Hata Mungu hapendi ujinga kama huo kasema tuungame dhambi zetu kimya kimya sio kudhalilishana[emoji16][emoji16][emoji16]..

Au ndugu yetu umekwama jogoo hapandi mtungi
Na bado anakuja kulalamika kishamba hivi.

Wanaume tupo wachache sana.
 
Hahaa ukaombe msamaha mbele ya kanisa, kwani umelikosea kanisa? Au anataka ufanye show kama ya WCB

Ila kuja kuomba ushauri hivi itakuwa inamaanisha upo 50/50[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Acha kuwaza huo upupu hata kwa asilimia moja[emoji1]
 
Usikubali kutekeleza upuuzi wake huu, usikubali kabisa.
Ukifanya hivyo utakuwa umejidhalilisha vibaya sana, sawasawa NA kusema unaenda kuvua nguo zako zote ulizovaa mwilini NA kubaki uchi wa mnyama mbele ya madhabahu ya kanisa. Aibu itakuwa kubwa sana kwako wewe, KWA mke wako, watoto wenu na familia zenu wote KWA ujumla. Watoto wenu watakuwa mmewaathiri kisaikolojia ktk maisha yao yote kutokana na aibu zenu nyinyi wazazi,
Mwambie mkeo atathmini kwanza juu ya athari za kufanya hivyo anavyotaka.
 
Wakuu nawasalimu,
Niko katika hali hii kwa sasa.
Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.
Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.
1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.
2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.
3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.
Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?
Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?
Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.
Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.
Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.
Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
Muulize hivi siku hizi una akili timamu?
 
Ndio kosa alilomfanyia? Mimi nilijua labda alichepuka[emoji3][emoji3][emoji3] kama alisema mbele ya kanisa ni vizuri kauli akaifutie huko huko
Duh hata kama kuchepuka ndio akapige magoti mbele kabisa kanisani!?? Mke ana masharti magumu mno aisee! !
 
Kwanza msamaha wa kweli hauna masharti ndani yako, msamaha ni kitu kinachotoka moyoni kama kupenda au kuchukia hakuna masharti ndani yake

Pili: Huyo mke wako ni aina ya wanawake wajinga ambao ujinga wao umeutengeneza wewe mwenyewe kwa kumuendekeza mpk akupe masharti ya kukudhalilisha. Kuwa mwanaume na simamia misingi ya kiume husiyumbishwe wala kuchezewa na mwanamke. Hata kama umefanya kosa kubwa kama kuzaa na mwanamke mwingine lazima mwanaume uwe na sauti ya mwisho umeomba msamaha ndio mwisho akihamua kusamehe sawa asiposamehe sawa sio unambembeleza bembeleza kila siku utadhani akiondoka unakufa bwana. Pumbaaaf

Nakazia hapa

Cc Kingsmann
 
Wewe utakuwa mume sarawili,marioo. Mnaachiwa magari myaendeshe wakati wake zenu wakiwa kazini. Ameshakuona huwezi chochote bila yeye. Pigana mwanaume
 
Back
Top Bottom