Mke wangu ananipiga vijembe WhatsApp

Nakushauri kabla ya kuchanganya lugha hebu kwanza tazama mwandiko wa mleta mada. Huyu si wa kuandikia kimalkia
 
Wewe umeuma maneno inawezekana amekufuma na michepuko au umezaa nje ya ndoa.
Unalo hilo babu!
 
Sasa si umuache utafute mwengine. Hayo ndio matatizo ya kufunga pingu za maisha.
 
KITENDO TU CHA MWANAMKE KUANZA KUKAA KWAO TAYARI NI TATIZO KUBWA KWENYE NDOA BORA HATA MNUNIANE KULIKO KUWA ANAONDOKA KWAO MKIGOMBANA.


Wengine wanaona wakibaki kununiana ndani itazidi kumuumiza moyo yule alokosewa yaani mke kila anapomuona huyo mumewe alofanya makosa ya makusudi anajisikia vibaya.

Sasa kuepukana na maisha ya kujaa uchungu moyoni bora kuondoka maana asiye machoni na moyoni huondoka.

Kuna watu wana maudhi ya makusudi kwenye ndoa jamani ?!
 
mblock watsup kwa muda then kaa kimya..

akichoka kukaa kwao atakutafta

usijichoshe,
kama mamake na babke walishatengana basi huyo nae atakusumbua tu

Hili ni kweli kabisa wazee washatengana na story ya wazee wake ilikua kama hii yangu haina tofauti
 
JF imenifanya nione ndoa ni upuuzi mtupu. Kila siku ni malalamiko ya mahusiano tena ndoa kabisa.
Poleni wanandoa.
 
Aibu sana usipoheshimiwa na mke ni kazi bure, heshima, adabu, utii na unyenyekevu ndio nguzo ya mke.
 
Unapokuwa kwenye kumi na nane hakikisha unampa dozi ya uhakika, hiyo ndio tiba
 
Umechanganya hbr kiasi hata nimeshindwa kuelewa ulitaka kutujulisha nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…