Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

nyie ndo wale mabwege mmezaliwa ili mgongewe wake zenu , endelea hivyo hivyo kuwa mjinga, unagongewa alafu eti hatua kubwa ulichukua ni kununa? Bwege kweli wewe anza kuvaa chupi za mke wako umsubiri huyo jamaa anaekugongea wife wako aje awatembezee rungu wote maana mnaishi jinsia moja hapo ndani
 
Binafsi deep down my heart,
Siwez kumuacha MKE wangu eti kwa kosa la kuchepuka, hata nimkute kitandani maana nampenda Sana na bado namhitaji.
Ukzingatia pia mi mwnywn Ni mchepukaji haswa, nnapochepuka nafs sometimes inanisuta sana ila Basi TU[emoji29].

ila Sasa siwez ruhusu ajue Hilo
(Ni Siri yangu) maana ntatengeneza Uhuru wa manyani.

Ninachomwambia kila Mara,
Siku nikimbaini anachepuka Mimi na yeye bhasi, talaka inatolewa chap mfuko wa shati.

Na nimemuweka wazi Hilo kusudi Kama difensive mechanism maana mwanamke kuchepuka madhara yake kwenye ndoa Ni makubwa sana kuliko hata sisi wanaume tukichepuka.[emoji4]
Hiyo ni Kweli na ipo wazi wanaume tuna heshima sana ila mwanamke akianza kuchepuka utagundua tu,kuna mambo lazima yatabadilika.
 
Only If possible!! tofauti na hapo dahhh!!!!!!

Dada hiyo issue ni ngumu sana

Unapoamua kuowa basi amua kweli kua now sifanyi ujinga wowote
Na unapoolewa basi hakikisha umeyamaliza hayo yote

Ndio mwanzo wa matatizo na magonjwa

Ni upumbavu
 
Dada hiyo issue ni ngumu sana

Unapoamua kuowa basi amua kweli kua now sifanyi ujinga wowote
Na unapoolewa basi hakikisha umeyamaliza hayo yote

Ndio mwanzo wa matatizo na magonjwa

Ni upumbavu
Huwezi jua sababu zake za kutoka nje..tungesikiliza upambe wa pili babda so huwezi hukumu kwa kusikia upande mmoja mkuu!
 
Katika mafungamano ya maisha ya ndoa ni kuishi na mke kwa wema hata katika hali ya kuwa unamchukia. Na ikitokea unataka kumuacha pia iwe ni kwa wema.
 
Sasa Si Umfukuze. Unaonekana Boya sasa.
Mwanamke haonewi huruma. Utapigwa Tukio Uje Kulia Lia Humu
 
Ingawa mkuu nishakusoma wewe ni mtu wa Aina gani,kutokana na uandishi tu,Muno,hanajua,Mahana nk.

Wewe sio mjanja wa kutosha kujua janja za hawa marafiki wa yule joka.

Hata kufika hapa JF hongera maana sijui uliwezaje kua mjanja wa kufika huku kwa wajanja.

Unaonekana ni mwaminifu Sana kwa mkeo na ni Mtu wa Mungu,usie na janja janja,hongera kwa hili pia.

Ila Ulichofanya hakitoshi,acha augue,acha alazwe,acha ateseke hata mwaka,Kama umeamua usimuache,hakikisha anasota kweli kweli.

Mkuu dunia imebadilika inabidi nawewe ubadilike,yeye alivo fikiria kukusaliti hakukuonea huruma hata chembe,Hadi unamgundua anajitilisha huruma yeye,acha aendelee kupata adhabu.

Kisha hakikisha unamchapa mikwala huyo ex wake,ili utengeneze gepu kubwa Kati yao,vinginevyo atarudi kumshawishi tena.
 
Mkuu kuna VAR
Naizima tu, kosa la usaliti kwangu hakuna msamaha, skwezi vumilia, hapo ndio mchizi kagundua, bila ya kujua si mwali angeendelea kupakuliwa vizuri tu. Mpe kadi nyekundu akaigawe kwa uhuru.
 
Only If possible!! tofauti na hapo dahhh!!!!!!
Hakuna mazungumzo ya ziada hapo zaidi ya kuseparate tu. Labda kama kuna jambo ambalo mwanamke alikua anapitia jamaa hajaamua kulisema kwa sababu tuna hukumu kwa kusikiloza upande mmoja tu. Otherwise hakuna mazungumzo ya ziada yanaweza kuwepo
 
Tatizo kubwa lilianza pale nilipogundua anachepuka na ex wake. Baada ya kuligundua hilo sikutaka kuchukua hatua za shari sana papo kwa papo, bali nilichukua hatua ambazo mpaka leo anashindwa kuelewa afanyeje, sasa imefikia hatua muda wote ni analia tu, saikolojia hayupo sawa na kama anataka kuchanganyikiwa hivi.

Baada ya kugundua kwamba anachepuka nilichukua maamuzi yafuatayo

1. Siku hiyo hiyo niliyogundua sikutaka kumuuliza kama ni kweli au siyo kweli kwa sababu nilishajihakikishia kwa asilimia 100.

2. Sikula Chakula chake, nilifika naingia jikoni na kuandaa Chakula mwenyewe (hii imeendelea hadi leo)

3. Najitahidi sana niwahi kurudi nyumbani tofauti na siku za nyuma.

4. Tukilala kitandani mimi nageukia mzungu wa nne.

5. Tangia siku hiyo sijawahi kumuomba unyumba(japo anaweka mazingira ya jambo hili kila siku)

6. Akiniuliza namjibu kidogo halafu naendelea na utaratibu wangu.

7. Kila kitu najifanyia hadi nguo chafu zote za kwangu nakusanya na kufua mwenyewe nikipata nafasi(Ninapokuta amezifua narudia kufua)

8. Simtukani wala kumuongelesha vibaya bali nafanya mambo yangu ndani ya nyumba kivyangu.

9. Baada ya kuona hivyo, akasema anataka akaonane na Mama yake(ilikuwa Ijumaa usiku, nikampatia nauli muda huo huo na kumwambia asubuhi na mapema aende, ghafla akasema ameahirisha hadi sasa yupo)

10. Nimeacha kuchangia naye kitu chochote ndani ya nyumba isipokuwa sehemu ya kulala tu(kitandani na penyewe mzungu wa nne au nalala sebuleni wakati mwingine).

Sasa leo ni siku ya 6 tangia nimeanza kuishi hivyo na mke, mke wangu amenyongonyea ghafla, amekonda, amekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote.

Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah [emoji24][emoji24] nilimwonea huruma sana na nikaamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote, kiufupi anapitia wakati mgumu sana.

Wito kwa wanaume na wanawake hasa wanaoishi pamoja kama mke na mume kwa namna yoyote ile, kupigana siyo adhabu tosha ya kusuruhisha migogoro, mimi huyu mwanamke nimempa adhabu hiyo lakini naona imemnyoosha kweli kweli japo naona kabisa imemuharibu kisaikolojia kabisa.
Kusamehe ni swala zuri na la kiungwana na dini zinatufundisha hivyo. Ila ulitakiwa umpe za uso za kumtosha na ufanye kitu kwa huyo ex wake.
 
Kwa maelezo haya ni lazima uchapiwe tu. Na mimi nasema endelea kuchapiwa tu mpaka akili ikukae.
 
Kaka alisema
1.mwanamke akikupa sumu ukapona msamehe
2.mwanamke akikupiga risas akakujeruhi na ukapona msamehe
3.mwanamke akichepuka na kugongwa nje ..achana nae.mpe talaka aondoke au wewe ondoka..
(1 na 2 Ni falsafa)
 
Adhabu uliyotoa uliitoa huku unajuta ..Ni Kama ulikiwa hauko tayar au kazi ulizokuwa unafanya happy nyumbani(kufua,kujipikia nk)zilikushinda ukawa unasubir akuombe msamaha...na ulipoombwa ukaona umeshamuweza...ukasamehe..Hilo Ni kosa..uko soft Sana kwenye maamuzi..
 
Back
Top Bottom