Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Narudia Tena,
Hapo Hamna adhabu yoyote ya maana uliyomuadhibu, Kwa Mwanamke Ni Kawaida Sana kujishusha anapokosea.

Ila kumsamehe HARAKA Tena kizembe namna iyo umekosea Sana, ulipaswa uombe USHAUR tukushauri adhabu nzur ya kisaikolojia, I'll sio hiyo yako.
Mpaka sasa, shauri zote zimejielekeza kufanya maamuzi kwa pupa na fujo zaidi ambazo mara nyingi hitimisho lake waga ni kihama.
 
Unge mkaushia miezi hata mi 3
Tena akiwaamemrudisha kwa wazazi wake, kule kwao atachambwa balaa na wazazi wake na ndugu zake kwa kuiletea aibu familia Yao ukweni.

Wanawake Ni Watu wanaoheshimu na kuogopa Sana walikotokea, itamuuma Sana

Siku ukija kumrudisha atakua keshanyooka vya kutosha, kutokurudia UPUMBAVU ule.
 
Tatizo kubwa lilianza pale nilipogundua anachepuka na ex wake. Baada ya kuligundua hilo sikutaka kuchukua hatua za shari sana papo kwa papo, bali nilichukua hatua ambazo mpaka leo anashindwa kuelewa afanyeje, sasa imefikia hatua muda wote ni analia tu, saikolojia hayupo sawa na kama anataka kuchanganyikiwa hivi.

Baada ya kugundua kwamba anachepuka nilichukua maamuzi yafuatayo

1. Siku hiyo hiyo niliyogundua sikutaka kumuuliza kama ni kweli au siyo kweli kwa sababu nilishajihakikishia kwa asilimia 100.

2. Sikula Chakula chake, nilifika naingia jikoni na kuandaa Chakula mwenyewe (hii imeendelea hadi leo)

3. Najitahidi sana niwahi kurudi nyumbani tofauti na siku za nyuma.

4. Tukilala kitandani mimi nageukia mzungu wa nne.

5. Tangia siku hiyo sijawahi kumuomba unyumba(japo anaweka mazingira ya jambo hili kila siku)

6. Akiniuliza namjibu kidogo halafu naendelea na utaratibu wangu.

7. Kila kitu najifanyia hadi nguo chafu zote za kwangu nakusanya na kufua mwenyewe nikipata nafasi(Ninapokuta amezifua narudia kufua)

8. Simtukani wala kumuongelesha vibaya bali nafanya mambo yangu ndani ya nyumba kivyangu.

9. Baada ya kuona hivyo, akasema anataka akaonane na Mama yake(ilikuwa Ijumaa usiku, nikampatia nauli muda huo huo na kumwambia asubuhi na mapema aende, ghafla akasema ameahirisha hadi sasa yupo)

10. Nimeacha kuchangia naye kitu chochote ndani ya nyumba isipokuwa sehemu ya kulala tu(kitandani na penyewe mzungu wa nne au nalala sebuleni wakati mwingine).

Sasa leo ni siku ya 6 tangia nimeanza kuishi hivyo na mke, mke wangu amenyongonyea ghafla, amekonda, amekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote.

Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah [emoji24][emoji24] nilimwonea huruma sana na nikaamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote, kiufupi anapitia wakati mgumu sana.

Wito kwa wanaume na wanawake hasa wanaoishi pamoja kama mke na mume kwa namna yoyote ile, kupigana siyo adhabu tosha ya kusuruhisha migogoro, mimi huyu mwanamke nimempa adhabu hiyo lakini naona imemnyoosha kweli kweli japo naona kabisa imemuharibu kisaikolojia kabisa.
Big up bro kwa huu ujasiri
 
Adhabu kisaikolojia Ni kkubwa,
ila haiwez kumfanya kujutia alichokufanya asirudie Tena kukifanya.

Lazima mkeo umtengenezee hofu ya matokeo ya kukucheat, sio ajue akikucheat ukikasirika utaishia kufua nguo na kuosha vyombo.

Huo Ni udhaifu sana na kuonesha kwake hupindui, na anajua umemsamehe Kwasababu unampenda Sana na huna mbadala.

Kwanza kile l kitendo Cha kuwahi mapema ana imani anajua huna pa kwenda, Ndo maana umerud nyumban mapema sababu ya wivu wako.
Hofu niliyomtengenezea kwa adhabu hii ni kubwa muno na pengine anajutia sana hajawahi kupewa mateso ya saiklojia ya namna hii.

Jioni hii amepelekwa hospitali hali yake imekuwa mbaya sana na pressure imekutwa iko juu sana.
 
ni wewe huyu unaandika yote haya au???

kwamba wewe huchepuki, au mkeo hachepuki na mchungaji??

au kwa vile hujamkamata???
Binafsi deep down my heart,
Siwez kumuacha MKE wangu eti kwa kosa la kuchepuka, hata nimkute kitandani maana nampenda Sana na bado namhitaji.
Ukzingatia pia mi mwnywn Ni mchepukaji haswa, nnapochepuka nafs sometimes inanisuta sana ila Basi TU[emoji29].

ila Sasa siwez ruhusu ajue Hilo
(Ni Siri yangu) maana ntatengeneza Uhuru wa manyani.

Ninachomwambia kila Mara,
Siku nikimbaini anachepuka Mimi na yeye bhasi, talaka inatolewa chap mfuko wa shati.

Na nimemuweka wazi Hilo kusudi Kama difensive mechanism maana mwanamke kuchepuka madhara yake kwenye ndoa Ni makubwa sana kuliko hata sisi wanaume tukichepuka.[emoji4]
 
Unajua kuna watu hapa wananiona kama nilichofanya badoo, ila adhabu hii niliyompa imepelekea jioni hii imebidi apelekwe hospitali, pressure iko juu sana na akitoka salama Mama yake anamchukua kwanza, kwhy unaweza kuona hili Jambo nilivyomakini nalo muno.
Amekuigizia na wewe umeingia kingi,

Kwanza kitendo Cha binti yao kuchepuka na ukawaficha wazazi wake unatengeneza bomu baya Sana.

Usichokijua,
Wanawake huwasikiliza na huwaogopa Sana wazazi wa kuliko hata wewe.

Wazaz wake na ndugu zake Wana nafas Kubwa Sana ya kumsema akabadilika kuliko hata wewe mme wake.

Hamna kitu wanawake wanaogopa Kama kuchafua jina la ukoo wao au familia Yao.

Malalamiko na makasiriko ya wazazi wake huwauma na kuwachoma Sana kuliko hata hicho kisirani Chako uko nyumbani kwako
 
Mpaka sasa, shauri zote zimejielekeza kufanya maamuzi kwa pupa na fujo zaidi ambazo mara nyingi hitimisho lake waga ni kihama.
Sio kweli,
Sio kila kosa Ni la kumuacha MKE,
Binafsi huwa najisemea kua siwez kumuacha MKE wangu kwa kosa la kuchepuka (japo siombei itokee, na sitak ajue Siri hii)

Ila hata nikimkuta kitandani sitompa talaka,
Kwa maana mbali na Hilo la kuchepuka, anayo mazur yake mengi Sana yanayolifunika Hilo baya la kuchepuka.
Ambalo kwa Mimi nimeshamkosea sana uko mafichoni.

Ila ujue siwez msamehe kirahisi hivyo,
Ntamnyoosha ipasavyo mpk ajutie UPUMBAVU ule.
 
Ndugu yangu,ukisikiliza ushauri wa wengi humu.utachanganyikiwa.kwanza nikuulize kama mna watoto.kama una watoto,hao ni kiunganishi kikubwa sana kati yenu.huenda nawe pia ktk maisha yako sidhani kama hujawahi kuchepuka.kuna watu wamezaa ndani ya ndoa na bado wakasemehewa na wenzi wao.adhabu hiyo uliyompa,sidhani kama atathubutu kurudia.mungu alisema samehe 7 mara 70 utapata thawabu.
 
Nakuelewa sana unajua kuna vitu vinapotokea ndani ya ndoa vinahitaji uvumilivu na uhamuzi wa busara kwanza kuliko nguvu. Waswahili wanasema unaweza kuruka mkojo ukakanyaga mavi.
Sahihi lakini hilo kosa adhabu yake ni straight RED CARD. Hakuna adhabu nyingine hapo. Makosa mawili kwenye ndoa hayahitaji vikao vya suluhu. Mke kuchapuka au kufanya mambo ya ushirikina. Malizana naye huyo mwanamke bro.
 
Unajua kuna watu hapa wananiona kama nilichofanya badoo, ila adhabu hii niliyompa imepelekea jioni hii imebidi apelekwe hospitali, pressure iko juu sana na akitoka salama Mama yake anamchukua kwanza, kwhy unaweza kuona hili Jambo nilivyomakini nalo muno.
Pia siyo jambo rahisi yaan we jamaa jasiri saana mimi nilimjeruhi vibaya nimeponea chupu chupu kua mahabusu saa hizi so naelewa ulichokifanya na nina heshimu kwasabab mimi najuta kwakua nimeharibu reputation yangu
 
Hofu niliyomtengenezea kwa adhabu hii ni kubwa muno na pengine anajutia sana hajawahi kupewa mateso ya saiklojia ya namna hii.

Jioni hii amepelekwa hospitali hali yake imekuwa mbaya sana na pressure imekutwa iko juu sana.
Unaweza pima Hofu? Hofu inapimwa kwa kipimo gani? Inaonekana wewe ni mrugaruha sana, eti hofu,
 
Hofu niliyomtengenezea kwa adhabu hii ni kubwa muno na pengine anajutia sana hajawahi kupewa mateso ya saiklojia ya namna hii.

Jioni hii amepelekwa hospitali hali yake imekuwa mbaya sana na pressure imekutwa iko juu sana.
Hizo zpte ni zuga tu, mwanamke anaweza hata zuga anakaribia kukata kamba, hizo zuga
 
Back
Top Bottom