Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Kakomaa na neno KISAIKOLOJIA, KISAIKOLOJIA, KISAIKOLOJIA, Mbona hiyo saikolojia hakuiona wala kuitumia kabla hajasalitiwa!
Anyway hawa ni wale wasiofurukuta kwa wanawake zao!
Dear ex endelea kukamua muke ya huyu jama ili kumsaidia kazi maana hawez kazi ila anaweza saikolojia.
Nawasiwasi kama wana mtoto jamaa analea watoto wa watu
 
Hakuna mazungumzo ya ziada hapo zaidi ya kuseparate tu. Labda kama kuna jambo ambalo mwanamke alikua anapitia jamaa hajaamua kulisema kwa sababu tuna hukumu kwa kusikiloza upande mmoja tu. Otherwise hakuna mazungumzo ya ziada yanaweza kuwepo
Exactly!!
 
Tatizo kubwa lilianza pale nilipogundua anachepuka na ex wake. Baada ya kuligundua hilo sikutaka kuchukua hatua za shari sana papo kwa papo, bali nilichukua hatua ambazo mpaka leo anashindwa kuelewa afanyeje, sasa imefikia hatua muda wote ni analia tu, saikolojia hayupo sawa na kama anataka kuchanganyikiwa hivi.

Baada ya kugundua kwamba anachepuka nilichukua maamuzi yafuatayo

1. Siku hiyo hiyo niliyogundua sikutaka kumuuliza kama ni kweli au siyo kweli kwa sababu nilishajihakikishia kwa asilimia 100.

2. Sikula Chakula chake, nilifika naingia jikoni na kuandaa Chakula mwenyewe (hii imeendelea hadi leo)

3. Najitahidi sana niwahi kurudi nyumbani tofauti na siku za nyuma.

4. Tukilala kitandani mimi nageukia mzungu wa nne.

5. Tangia siku hiyo sijawahi kumuomba unyumba(japo anaweka mazingira ya jambo hili kila siku)

6. Akiniuliza namjibu kidogo halafu naendelea na utaratibu wangu.

7. Kila kitu najifanyia hadi nguo chafu zote za kwangu nakusanya na kufua mwenyewe nikipata nafasi(Ninapokuta amezifua narudia kufua)

8. Simtukani wala kumuongelesha vibaya bali nafanya mambo yangu ndani ya nyumba kivyangu.

9. Baada ya kuona hivyo, akasema anataka akaonane na Mama yake(ilikuwa Ijumaa usiku, nikampatia nauli muda huo huo na kumwambia asubuhi na mapema aende, ghafla akasema ameahirisha hadi sasa yupo)

10. Nimeacha kuchangia naye kitu chochote ndani ya nyumba isipokuwa sehemu ya kulala tu(kitandani na penyewe mzungu wa nne au nalala sebuleni wakati mwingine).

Sasa leo ni siku ya 6 tangia nimeanza kuishi hivyo na mke, mke wangu amenyongonyea ghafla, amekonda, amekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote.

Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah [emoji24][emoji24] nilimwonea huruma sana na nikaamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote, kiufupi anapitia wakati mgumu sana.

Wito kwa wanaume na wanawake hasa wanaoishi pamoja kama mke na mume kwa namna yoyote ile, kupigana siyo adhabu tosha ya kusuruhisha migogoro, mimi huyu mwanamke nimempa adhabu hiyo lakini naona imemnyoosha kweli kweli japo naona kabisa imemuharibu kisaikolojia kabisa.
Wewe ni mgeni na hao watu hujui ZE COMMEDY Zao
 
Utachapiwa tena, mark my words. Na safari hii kitapigwa hadi kilainike, na ataomba talaka akakae peke yake ili aendelee kufaidi kwa nafasi. Utarudi hapa kuomba ushauri. Sababu za kuchapiwa tena:
  1. Hujajua kwa nini amechepuka. Huwezi kutatua tatizo usilojua chanzo chake
  2. Umekurupuka kutoa dawa ya ugonjwa usiojua
  3. Uanaume wako haujadhihiri kwa vitendo ulivyomfanyia mkeo ukiviita eti "adhabu". Kununa, kususa na kuzira ni tabia za kike. Kwa vitendo hivyo umemthibitishia mkeo kwamba kaolewa na mwanamke mwenzake, kwa hiyo baadaye atajihisi kwamba alifanya sahihi kutafuta mwanaume kwa njia ya mchepuko
  4. Umemthibitishia mkeo kwamba huyo X wake ni mwanaume halisi na wewe ni "suruali" tu, mnunaji!
  5. Kama kuchepuka kwake ni sawa na kumwagia mbigiri kitandani, wewe umeharibu kabisa kwa kumwaga upupu, hapatalalika tena. Ataendelea kutafuta faraja kwa michepuko.
 
sawa mkuu ila na wewe ukipewa show piga show la maana hadi asimfikirie yule x wake tena, mwanamke ni mgumu sana kutoka kwenye ndoa kama uchumi wako upo sawa basi show ya uhakika ni kitu muhimu sana.
 
Mke wa ndoa kawaida huchepuka na waliowahi mlala kabla yako.Sio watu wapya.SIo mwanzo Wala mwisho tayari wana agano hao watu.

MNGEKUWA NA AKILI,MNGECHA KUOA KWA GHARAMA NYINGI YA FEDHA NA MUDA.
 
Mwanamke akishaanza kuchepuka huyo ni sawa na nyoka ndani ya nyumba. Kuendelea kuishi na mtu wa hivyo utakufa kabla ya siku zako.
 
Ingawa mkuu nishakusoma wewe ni mtu wa Aina gani,kutokana na uandishi tu,Muno,hanajua,Mahana nk.

Wewe sio mjanja wa kutosha kujua janja za hawa marafiki wa yule joka.

Hata kufika hapa JF hongera maana sijui uliwezaje kua mjanja wa kufika huku kwa wajanja.

Unaonekana ni mwaminifu Sana kwa mkeo na ni Mtu wa Mungu,usie na janja janja,hongera kwa hili pia.

Ila Ulichofanya hakitoshi,acha augue,acha alazwe,acha ateseke hata mwaka,Kama umeamua usimuache,hakikisha anasota kweli kweli.

Mkuu dunia imebadilika inabidi nawewe ubadilike,yeye alivo fikiria kukusaliti hakukuonea huruma hata chembe,Hadi unamgundua anajitilisha huruma yeye,acha aendelee kupata adhabu.

Kisha hakikisha unamchapa mikwala huyo ex wake,ili utengeneze gepu kubwa Kati yao,vinginevyo atarudi kumshawishi tena.
Sahii kabisa,
Yule mhuni anaemla mkewe inaonekana kana kwamba anamuogopa, na jamaa kule ashajua keshajulikana afu jamaa anasita kumfata.

Ni udhaifu mkubwa sana
 
Yote umefanya sahihi kabisa, kosa kubwa hapo ni HURUMA!

Hata kama ungemsamehe, haikutakiwa kuwa rahisi kiasi hicho. Imekuwa rahisi kama vile ni issue ndogo tu, kumbe mtu kapeleka kipapa kwa jirani/ex.
 
nyie ndo wale mabwege mmezaliwa ili mgongewe wake zenu , endelea hivyo hivyo kuwa mjinga, unagongewa alafu eti hatua kubwa ulichukua ni kununa? Bwege kweli wewe anza kuvaa chupi za mke wako umsubiri huyo jamaa anaekugongea wife wako aje awatembezee rungu wote maana mnaishi jinsia moja hapo ndani
Comment ya kipumbavu Sana hii. Sijapendezewa. Sigongewi lkn majibu haya ni kum_#@35-e

Vipi sigongewi.

Najua kukaba mbaya.

Ila Tusijiamnishe. Kuna jamaa mkewe ni mzuri anaitwa a...... Mkubwa anafanya utata mkewe anasimulia. Tujue tukkaza wakipata mwanya wa natusema.
Sasa basi kigongewwa si kosa letu
 
Kununa hajujawahi kua suluhisho la kudumu kwenye migogoro Kama hiyo.

Ulichokifanya Ni kana kwamba uyo mwanamke ni unaiba tu (Mchepuko au hawala yako).
Hujaonesha Yale makucha na mAmlaka ya kiume kuonesha umekasirishwa na alichokifanya.

Na kwasababu umemsamehe kirahisi Sana, nna imani atachepuka Tena maana keshakusoma una moyo mwepesi Sana wa kusamehe haraka.

Ulitakiwa uoneshe advertise Moja matata Sana kama unamwacha Moja kwa moja.
(Hata Kama huna.mpango wa kumuacha)

Pia uyo ex wake nae umchimbe mkwara mzito Sana kwamba umejua na akiendelea dawa yake inachemka. Ajutie kabisa Ujinga aliufanya. Yaan ikiwezekana uyo kijana ndio amkimbie mkeo.

Unapojificha eti unanuna na hufunguki kwa pande zote mbili kilichokukasirisha. Eti unajifulia nguo n.k
Huo unakua Ni ufala.

Wote wanakuona Ni mwanaume mwenye wivu sana na kisirani tu. Na ulivosamehe kirahis wameshakuchora Ni mwanaume kisirani na laini asiye na msimamo kabisa.

BE A MAN and be a HUSBAND[emoji120]
Simamia ndoa yako, ilinde familia yako
Kwa hiyo unamshauri mwana akakiwashe au sio [emoji1]
 
Back
Top Bottom