Nimepata muda wa kupitia komenti, baadhi ya watu wanakomenti kwa hasira muno na matusi juu, kitu ambacho wengi wetu tunasahau ni kwamba
Wake tunaowaoa wanakuwa siyo Bikra, kwa maana hiyo wanakuwa wameshalalwa na watu wengine kama sisi wanaume tunavyokuwa tumeshalala na wanawake wengine.
Ni kweli kosa la kuchepuka halifai kupewa msamaha hata maneno matakatifu yametamka wazi, lakini ukimwacha ukamuoa mke mwingine, huyo mwingine utamkuta Bikra?, Vile vile upo uwezekano wa kumuoa mwingine mwenye tabia chafu zaidi na mambo yakaharibika zaidi.
Wanaume wenzangu nawaelewa mnaposema nimekosea kumsamehe, hii ni kwa sababu mara nyingi tunavutaga picha na kufikiria ni jinsi gani alikuwa anashiriki tendo hilo na huyo mtu.
Baadhi naona walitaka nifanye tukio baya zaidi kama kupiga, kuua au kumfukuza papo kwa papo kitu ambacho kingeleta madhara zaidi kwa familia zote mbili(hapa waliopo kwenye ndoa wataelewa)
Kuna watu wanasema amejifanya ameigiza, sizani kama ni kweli yaani aigize pressure na moyo kushtuka?, Hapa ninapoandika hali yake bado ni mbaya muno.
Kwa kumalizia kuna watu wamelaumu kumsamehe, kama nisingeweza kufanya hivyo haraka uhenda angekunywa Sumu kweli na kufariki, kwahiyo kuepusha yote hii imebidi nifanye hivyo maana hamna haja ya kuua wakati uwezekano wa kumrudisha kwao na kila mtu akaendelea na maisha yake upo pia.
Vile vile pamoja na adhabu hii na msamaha niliyompa, bado kuna hatua kadhaa zitafuata baada ya yeye kuwa ameruhusiwa kutoka hospitalini, so niko well organized kupambana na hii changamoto.
Ushauri ninaouchukua kutoka kwenu ni ule ambao una lengo la kuleta suluhisho la kudumu, na siyo ule wa kuchochoea mgogoro zaidi, nimefarijika kuna baadhi wanatoa ushauri wa maana zaidi.