Mke wangu anasumbuliwa na tatizo la uke mkavu na kukosa ute wa mimba

Mke wangu anasumbuliwa na tatizo la uke mkavu na kukosa ute wa mimba

Loading failed

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2023
Posts
2,603
Reaction score
7,501
Ndugu zangu salaam

Kama kichwa cha habari kinavyosema ni kweli mke wangu anasumbuliwa na tatizo la uke mkavu hata akiwa kwenye siku za hatari, pia anakosa ute wa mimba.

Kuna kipindi ukimuaandaa analoa kidogo na ukiloweka haiishi dk 5 ameshakauka kabisa..kipindi cha siku za hatari ule ute wa kutungisha mimba hamna kabisa zaidi utamhisi kwa ndani ni mbichi kidogo na ukipump dk chache anakauka tena.

Amejaribu kutumia maji ya bamia, chai ya mdalasini, karafuu na tangawizi bila kuweka sukari, pia juice ya beetroot bila mafanikio.

Mzunguko wake inshort haueleweki anaweza akawa na siku 25,26, 27 ( na hata ukitafuta wastani huwezi kupata maana ni random), miezi mingine anaweza akawa hivi 27,27,26 , mingine 25,27,25, mingine 26, 25, 25. Hata ukijumlisha kutafuta wastani kila baada ya miezi mitatu zinapishana.

Siku zake za kuona damu ni 5.

Dalili anazokuaga nazo.

  • Punic na hasira sana kupita kiasi
  • Kuumwa matiti
  • Kichefuchefu
  • Kuumwa kichwa mara chache
  • Kuumwa Tumbo chini ya kitovu na wakati mwingine juu ya kitovu
  • Kuumwa upande wa kushoto karibu na kiuno
  • wakati mwingine mara chache Kuumwa upande wa kulia karibu na kiuno
  • Kizunguzungu
  • Mwili kuchoka sana mara kwa mara kiasi cha kujisiki hali ya uvivu

;: Hana fungus, UTI, PID wala mimba hana.

Nb; miaka ya nyumba background yake aliwahi kuwa mpenzi wa madawa ya hospital sana kutibu maradhi mengine kama Typhoid, Fungus ukeni, UTI za mara kwa mara. Alikua anabugia dawa huko nyuma kama njugu.

SIFIKIRII ATUMIE DAWA ZA HOSPITALI KUTOKANA NA HISTORIA YAKE MBAYA YA KUTUMIA SANA MDAWA HOVYO,

NAOMBENI USHAURI WA KINA SANA

ASANTENI
 
Atumie juisi ya bamia mkuu!!
Unakatakata vipande unaloweka kwenye glass kwa muda wa nusu saa alafu anakunywa! Tatizo liataisha kwa muda mfupi sana.
Hii ametumia sana ila alikua analoweka kwa muda wa masaa 12. Vipi hii nusu saa na masaa 12 ipi ni bora zaidi. Mana hii ya masaa 12 naona bado haileti nafuu?
 
SHIDA MNAOA WANAWAKE HAMFANYI UCHUNGUZI KUHUSU MAISHA YAO, MAGONJWA, MAHUSIANO YALIYOPITA, NA FAMILIA ZAO... Halafu badala ya kuinjoi ndoa mnatumia muda mwingi kuwatibia kuhangaika hospital na kutumia pesa nyingi...
Embu rudia kusoma ulichoandika, maana ndipo tatzo lilipo kwa mkeo 👇👇

Nb; miaka ya nyumba background yake aliwahi kuwa mpenzi wa madawa ya hospital sana kutibu maradhi mengine kama Typhoid, Fungus ukeni, UTI za mara kwa mara. Alikua anabugia dawa huko nyuma kama njugu.
 
Back
Top Bottom